Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 31, 2018

RC Makonda Ataja Majina ya Mashoga Maarufu Nchini....Aunda Tume ya watu 17

juu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameunda kamati maalum ya watu 17 itakayoshughulika na masuala ya mapenzi ya jinsia moja jijini Dar es salaam kwa kile alichokieleza ni kukomesha biashara hiyo ndani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Majukumu mengine ya kamati hiyo iliyoundwa na Makonda ni kushughulika na waigizaji wa filamu za ngono nchini, wamiliki wa nyumba zinazotumika kuigiza video za ngono, pamoja kuwatafuta watu wanaotumia mitandao kutapeli.

“Tumefikiria tuunde kamati, kamati itakayokuwa kwenye makundi manne, moja itakayojihusisha na kundi lote la mashoga, wanaojitangaza na wale wasiojitangaza lakini wanajulikana ni mashoga na nimeshapata taarifa nyumba takribani 24 wanazofanyia kazi, wanachukua wakina dada, wanawanywesha madawa na kuwafanyia vitendo hivyo wakiwarekodi”, amesema Makonda.

Katika mkutano huo, Makonda amezitaka mamlaka zinazohusika na haki za binadamu nchini kutoingilia suala hilo kwa kile alichokisema suala hilo ni kinyume na taratibu na sheria za Tanzania.

“Ndugu zangu wa haki za binadamu nafahamu hili jambo nilishawahi kuligusa kipindi cha nyuma, na mataifa mengine ambayo mataifa yao yamepokea na kukubali ushoga, sisi tuna utamaduni wetu, tuna sheria zetu, msituingilie” Amesema Makonda.

Aidha Makonda ameongeza; “leo zimefika ujumbe 18972 na hawa wote wanalaani na simu zilizokuwa zinapigwa ni nyingi sana niwasihi endeleeni kutuma ujumbe ili tuendelee kukomesha biashara hiyo haramu, lakini kwenye hiyo orodha kuna majina yako 200 lakini kuna baadhi ya watu wamejirudia kwa sababu wameamua kujitangaza watu hao ni James Delicious, Dida Mtamu, Aunty Miliki, Abbasi.”
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )