Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, October 21, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 14

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

“Sasa kwa nini una nidanganya. Hembu niambie ukweli”
Dada Mery alizungumza huku akiushika mkono wangu wa kulia, akakigusisha kiganja changu kwenye kitumbua chake na kuana kikichezesha chezesha. Japo ni baridi kali, ila jasho halikusita kunitoka mwilini mwangu. Dada Mery akafika mbali zaidi mara tu ya kukiingiza kidogo changu cha katikati katika kitumbua chake na taratibu akaanza kukikatikia kiuno huku mkono wake mwengine wa kushoto akiupitisha pitisha kichwani mwangu na kunifanya nijawe na hisia kali sana.
“Nyinyi NGURUWEEE munafanya nini ndani ya nyumba yangu?”
Tuliisikia sauti ya ukali ya mzee Clopp iliyo nifanya nikurupuke kutoka katika tukio nililo kuwa nina lifanya hadi kuanguka chini huku macho yangu yakimtazama mzee Clopp jinsi alivyo vimba kwa hasia kali kama chui aliye uliwa mwanaye.

ENDELEA
Mzee Klopp akaanza kunifwata kwa hasira, ila dada Mery akamuwahi na kumzuia baba yake.
“Ethan nenda nje”
Dada Mery alizungumza na kunifanya ninyanyuke kwa haraka na kukimbilia sebleni. Bibi Jane Klopp akabaki akinishangaa jinsi ninavyo hema.
“Kuna nini?”
Bibi Jane aliniuliza huku akinitazama machozi mwangu, kwa jinsi nilivyo jawa na woga nikajikuta hata nikshindwa kabisa kumjibu bibi Jane Klopp. Kelele za kufoka za mzee Klopp zikamfanya bibi Jane Klopp kuanza kupandisha ngazi kuelekea gorofani. Kwa haraka nikatoka katika mlango wa kutokea humu ndani na nikaanza kukimbia kuelekea getini.
“Ethan vipi mbona una kimbia kuna nini?”
 
Mlinzi aliniuliza huku akinitazama.
“Kuna mtu ninakwenda kuonana naye hapo mbele tafadhali ninakuomba unifungulie geti”
Mlinzi akaminya batani ya kufungua geti hili, iliyopo ndani ya kibanda chake. Nikaanza kukimbia kuelekea mtaani, kutokana mji huu nimeufahamu kwa asilimia kubwa, hakuna hofo ya mimi kuweza kupota. Nikazidi kutokomea mtaani huku nikiamini kwa kufanya hivi kutasaidia yale mabaya ambayo Ethan alinieleza juu kuuwawa kwa mzee Klopp basi hayato tokea tena. 
 
“Ethan naomba unisaidie”
Nilizungumza huku nikizidi kusonga mbele, nikikatiza katiza kwenye mitaa japo kuna baadhi ya watu ambao walinikodolea macho, nina hisi wengi wao watakuwa wakinifananisha kwa maana katika umri wangu huu mdogo nimeweza kuwa maarufu sana.
‘Hei’
Nilimuona Ethan pembeni yangu akitembea pamoja nami.
‘Nimeondoka nyumbani kwa ajili ya lile tatizo lisitokee’
‘Natambu hilo, pia ni maamumuzi mazuri’
‘Sasa natakiwa kwenda wapi?’   
‘Wewe unataka kwenda wapi?’
‘Sijui na siwezi kurudi kwa yule mzee kwa maana ni aibu kubwa sana mimi kukuta nikifanya vile na yule dada’
‘Hata dada yako hakutarajia kufanya vile ila nilimtuma jini mahaba, kumuingia na kujikuta akikutamani na kufanya vile.
‘Haukuona njia nyingine ya kuweza kufanya hadi unifanyie vile?’
 
‘Ni njia gani nyingine ya kufanya sasa?’
‘Ethan hembu niambie basi maisha yangu ya mbeleni yatakuwaje?’
‘Siwezi kukuambia na mimi sio mtabiri wako. Ninakueleza pale unapo kuwa na tatizo kubwa ambalo litakuhatarishia maisha yako, ila kwa sasa siwezi kukuambia chochote’
Maneno ya Ethan yakanikatisha tamaa kwa kweli. Nikasimama na kutazama majengo mengi yaliyo tuzunguka katika eneo hili.
‘Ili kufanikiwa ni lazima uweze kuitambua shida, shida itakayo kujenga kiakili, kimaarifa na utaweza kuwa makini na mafanikio yako kwa maisha yako ya baadae’
‘Mmmmm’
‘Ndio’
 
Ethan akapotea kwenye uwepo wa macho yangu. Nikatazama nilipo nikashusha pumzi nyingi kisha nikaendelea na mizunguko katika jiji hili la Berlin. Hadi inaitimia usiku wa saa moja sikuweza kupata chochote tumboni mwangu na wala sifahamu ni wapi nitalala katika usiku huu. Nafsi moja ina nishauri niweze kurudi kwa mzee Klopp, ila nafsi nyingine ina nishauri nisiweze kurudi kabisa nyumbani kwa mzee Kloop kwani kwa hasira aliyo nayo juu yangu ni lazima atania. Baridi kali ikazidi kunitesa na kuusumbua moyo wangu, hakika katika hali ngumu ya maisha niliyo ipitia moja wapo ni hii. Nikatamani kuyafuta japo kibanda cha simu niweze kumpigia mpenzi wangu Camila aweze kunisaidia, ila nikaona sio jambo la burasa kwa mimi kuwa omba omba na pia atahitaji kufahamu ni sababu gani ambayo ilinifanya mimi kuweza kuondoka katika nyumba ya mzee Klopp na endapo ataifahamu ni sababu ya kimapenzi nahisi hata msaada wake kwangu naamini unaweza kubadilika. Nikiwa katika moja ya godauni kubwa ambalo lina watu wengi omba omba wanao lala, nikaona kundi kubwa la vijana walio nizidi umri wakinisogelea. Woga ukanijaa na nikaanza kurudi rudi nyuma, ila kwa wingi wao wakafanikiwa kunizunguka na kuniweka katikati.
 
“Hei umefwata nini hapa wewe mtu mweusi?”
Mmoja wao alizungumza huku akinisukuma.Nikashindwa kuwajibu chochote zaidi ya kuendelea kutetemeka kwani katika maisha yangu kitu nisicho kipenda ni kupigana na wala sina ujuzi wowote katika swala la kupigana.
“Hujibu si ndio?”
“Mi…..”
 
Nikastukia ngumi nzito ikitua kwenye shavu langu la upande wa kulia na kunifanya niweweseka na kuona maruwe ruwe mengi sana ambayo hakika yakanipotezea hata uwezo wa kuweza kuona vizuri. Nikastukia mtama mzito ulio niangusha chini mzima mzima. Wakaanza kunivua viatu, wakafwatia surualia yangu pamoja na tisheti niliyo ivaa na wakaanza kunipiga mateka mfululizo. Nikaendelea kujikunyata ili wasiniumize uso wangu, galfa nikahisi kitu chenye ncha kali kikinichoma kwenye mbavu zangu, jamgo lililo nifanya nipige kelele kali sana za maumivu kwani maumivu yake ni makali kupita hata mateke na ngumi wanazo nipiga.
“Hei muna mfanya nini mwenzenu”
Vijana hao mara baada ya kusikia kelele hiyo, wakatawanyika na kukimbia na kuniacha nikiwa nimelala chini huku nikilia kwa uchungu sana. Nikajaribu kuuepeleka mkono wangu wa kulia kwenye mbavu zangu, nikajikuta nikiwa na kisu kikiwa kimezama kwenye mbuvu zangu jambo liilo nifanya nichanganyikiwe sana na kuzidi kulia, hadi nikapoteza fahamu.
                                                                                                                             ***
“Hei ume amka?”
Nilisikia sauti ya kime ikipenya vizuri masikioni mwangu. Nikamtazama mwanaume anaye nisemesha, nikamuona ni mwanaume mwenyea asili ya kiafrika kama mimi. Mwanaume huyu kichwani mwake ana rasta nyingi na defu. Mkononi mwake ameshika msokoto mkubwa wa bangi na katika chumba hichi nilicho lala kimejaa mapicha picha mengi ya mwanamziki Bob Marley.
“Nipo wapi?”
 
Niliuliza kwa upole sana huku nikimtazama jaa huyu, kabla ya kunijibu akapiga fumba moja la bangi aliyo ishika kisha akapuliza hewani na kukohoa kidogo huku akipiga piga kifua chake.
“Dogo upo kwa rasta Man Bob….Wooo, Wooo”
Mwanaume huyu alizungumza huku akirusha rusha nywele zake, nikajitazama nilipo lala. Ni kitanda kimoja kidogo na kina mashuka yanayo nuka kwa uvundo wa kuto kufuliwa kwa siki ningi. Eneo la tumboni mwangu nimezungushiwa bandeji moja kubwa sana.
“Unajisikiaje?”
Aliniuliza huku akivuta kistuli na kukaa pembeni yangu. Taratibu nikanyanyuka na kukaa kitako huku nikimtazama.
“Ninajisikia maumivu”
“Ohoo vuta kitu hichi kidogo, utajisikia poa kabisa”
“Hapana asante”
 
Mwilini kitu nilicho baki nacho ni boksa tu.
“Nipo hapa toka lini?”
“Jana usiku, nilikuokoata kuna madogo walikuwa wanakushambulia”
“Nahitaji kurudi nyumbani”
“Nyumbani?”
“Ndio”
“Kwenu ni wapi?”
Nikajikuta nikishindwa kumjibu rast man huyu mara baada ya kuona taarifa ya kutafutwa kwangu kwenye tv ndogo ya chogo iliyomo ndani humu na endapo mtu atatoa ushirikiano wa kupatikana kwangu atapatiwa dola elfu hamsini na familia yangu. Rasta Man huyu akanitazama vizuri, kisha akarudisha macho yake kwenye tv ili kunifananyisha na kile alicho kiona.
“Ahaa wewe ndio Ethan Klopp?”
 
Nilimjibu rasta man huyu kwa kutingisha kichwa kwamba ndio mimi. Akaruka juu kwa furaha, kwa haraka akata simu yake mfukoni na kuanza kupiga namba za mzee Klopp zinazo onekana kwenye tv.
“Woo wooo rasta mana Bob hapa nina ongea na mzee Klopp mgongoni namba saba machachari”
Rasta man huyu alizungumza kwa shauku kubwa, naamini akili yake hapo ina furahia donge nono lililo ahidiwa na familia ya mzee Klopp.
“Kijana wenu nipo naye, na hali yake sio nzuri. Ila hakikisheni kwamba muna kuja na mpunga wangu kumchukua la sivyo hamta muona”
“Sijamteka mimi, ila nilimsaidia, mikiwa tayari nipigieni simu muje kumchukua”
 
“Poa poa, wooo wooo rasta mana weeeee”
Alikata simu huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Mawazo mabaya juu ya adhabu ambayo ninaweza kupewa na mzee Klopp, yakaanza kunitawala kichwani mwangu. Rasta man huyu akazidisha makeke ya kunisaidia, ili maradi niweze kumuona mwema. Baada ya dakika kama kumi hivi simu yake ikaita kwa haraka akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Ndio, nipo naye hapa. Chukua uzungumze na mama yako”
Rasta man akanikabidhi simu yake taratibu nikaipoke na kuiweka sikioni mwangu.
“Ethan”
Niliisikia sauti ya bibi Jane Klopp akiniita huku analia.
“Naam mama”
 
“Ohoo asante Mungu, unaendeleaje mwanangu?”
“Naumwa mama”
“Ohoo Mungu wangu tunakuja sasa hivi sawa”
“Sawa mama”
Simu ikakatwa, nikamrudishia rasta man. Kwa haraka masta man akaanza kufanya usafi ndani kwake humu, huku mifuko ambayo imejaa misokoto ya bangi akiitoa nje na wala sifahamu ni wapi alipo iweka. Baada ya muda rasta man akaingia ndani humu huku akiwa ameongozana na bibi Jane Klopp pamoja na askari wawili. Bibi Jane Klopp kwa haraka akanikimbilia na kunikumbatia, alipo liona jeraha lililopo kwenye mbavu zangu kwa haraka akapiga simu hospitali na haukupita muda mrefu gari la wagonjwa likafika. Madaktari wakaniweka juu ya machelea maalumu huku waandishi wa habari nao wakijitahidi kuchukua tukio hili. Rasta man akaninyooshea dole gumba, ikiwa ni ishara ya kunitakia safari nje. 
 
Njia nzima bibi Jane Klopp anasali huku machozi yakimwagika usoni mwake. Madaktari wakaanza kunihudumia jeraha langu upya kabisa. Tukafika hospitalini na nikashushwa kwenye machela hii kwa haraka nikakimbizwa kwenye chumba cha upasuaji huku bibi Jane Klopp akizuiwa kuingia ndani ya chumba hichi. Nikachomwa sindano ambayo ndani ya muda mchache nikajikuta nikiishiwa nguvu mwilini mwangu na kulala usingizi fofofo.
                                                                                                                ***
    Cha kumshukuru Mungu upasuaji umefanyia vizuri na kisu nilicho chomwa hakikuni athiri sana katika pamvu zangu. Watu mbalimbali ndani ya nchi hii ya Ujerumani, hawakusita kufika hospitalini hapa kunijulia hali kwani tayari nimezidi kuwa maarufu. Camila na wazazi wake nao hawakuwa nyuma kunitembelea kila siku huku wakionyesha dhairi kwamba wamenikubali kama mkwe wao japo mimi na mtoto wao bado tuna umri mdogo ambao hatupaswi kuingia kwenye mahusiano.
 
“Ethan”
Mzee Klopp aliniita huku akiwa amekaa pembeni ya kitanda changu.
“Naam baba”
“Ninakuomba unisame kwa kila kitu ambacho kimetokea kwenye maisha yangu. Natambu hasira yangu na kung’ang’ania kwangu uwe mchezaji kutokana na tamaa ya kipesa ndio kumekufanya leo hii uwe hapa kitandani. Naomba unisamehe sana”
Mzee Klopp alizungumza kwa unyonge na kwa upole sana na kumfanya Bi Jane kunitazama usoni mwangu.
“Nimekusamehe baba naombeni na mimi munisamehe, nimewapa hasara ya kifedha”
“Hapana hapana Ethan, pesa sio kitu, ila uhai wako ndio kitu muhimu kwenye maisha ya hivi sasa”
Bibi Jane Klopp alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia. 
 
“Kwa sasa tutakuacha uendelea na mashomo yako na endapo hadi utakapo maliza elimu ya msingi basi unaendelea na hili swala la kufikiria kucheza katika timu kubwa”
“Nashukuru sana baba kwa kuelewa”
Muda wa mzee Klopp na mkewe kukaa ndani humu chumbani kwangu ukaisha na wakaondoka na wakaniacha mimi peke yangu kama siku zote na uangalizi wote hufanywa na madaktari.
‘Za masiku’
Niliisikia sauti ya Ethan, nikatazama kwenye kona moja ya chumba hichi nikamuona akiwa ameiegemea huku akinitazama.
 
“Siku zote ulikuwa wapi?”
“Kwani nilikueleza kitu gani?”
“Sawa, kunieleza kutu hichi ndio kukufanya uondoke na kuniacha peke yangu kwenye matatizo na ona sasa jinsi nilivyo jeruhiwa”
Nilizungumza kwa jazba kidogo huku nikimtazama Ethan. 
“Wooo sasa kwa nini usipambane na wale vijana?”
“Ethan hembu acha kunitania bwana. Uliniambia kwamba utanipa nguvu sasa nguvu zenyewe mbona sizioni?”
“Kwani umesha kuwa?”
“Hata kama, ila nahitaji wale vijana nao niwafanye kitu kibaya”
“Kweli?”
“Ndio”
“Twende”
“Wapi?”
“Si sehemu walipo ukawafanyie kitu kibaya”
“Si unaona kabisa nina jeraha”
“Huniamini au?”
Nikamtazama Ethan kwa muda kidogo, kisha nikachomoa sindano inayo ingiza maji kwenye mishipa yangu. Nikashuka kitandani, Ethan akanikumbatia kwa kasi ya ajabu tukatoka katika eneo hili la hapo hospitalini na kuanza safari ya kwendaeneo walipo vijana amabo walinipiga na kunichoma kisu changu katika mbavu zangu.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )