Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 24, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 17

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       

Nilizungumza huku nikiendelea kulia kwa uchungu. Watu washuhuri na wafanya biashara kutoka maeneo mbali mbali wakafika katika jumba hili la mzee Ethan na ulinzi ukazidi kuimarishwa.
‘Ethan’
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu katika ufahamu wangu wa akili.
‘Vipi?’
Nilimjibu kimoyo moyo pasipo watu wengine kuweza kufahamu ni nini ninacho kizungumza.
‘Kuna watu wana mpango wa kukuua usiku huu, kuwa makini la sivyo jua la asubuhi huto weza kuliona’
Maneno ya Ethan yakanistua sana kwani watu walio fika nyumbani hapa ni wengi sana hadi sujui nani ni mzuri au nani ni mbaya, jambo lililo anza kunipa wasiwasi moyoni mwangu.

ENDELEA
‘Mungu wangu, ni kina nani hao Ethan’
Niliuliza huku nikiendelea kutazama watu waliomo katika eneo hili.
‘Kuna mameneja sita wamejiunga ili kuhakikisha kwamba wanakuangamiza na mali zote zinakuwa chini yako’
‘Nionyeshe basi Ethan niweze kuwajua’
Niliendelea kuzungumza huku wasiwasi ukizidi kunitawala moyoni mwangu.
‘Ethan dada yako ametekwa’
Sauti ya Ethan ikanistua sana na kujikuta nikianza kukimbia kuelekea chumbani kwake, nikaingia na sikumkuta.
‘Ametekwa wapi?’    
 
Nilimuuliza Ethan mwenzangu ila hakunijibu chochote.
‘Niambie basi’
‘Chungulia dirishani’
Kwa haraka nikakimbilia dirishani na kuona gari aina ya BWM X5 ikitoka getini.
‘Wale ndio watekaji, wanaondoka’
Niliisikia sauti ya Ethan huku nikishuhudia jinsi gari hilo linavyo tokemea kwenye upeo wa macho yangu. Kabla sijatoka ndani humu mlio wa simu ya mezani katika chumba hichi ukanistua sana. Nikaitazama kwa muda huku jasho likinimwagika usoni mwangu.
 
“Ethan”
Sauti ya Camila ikanifanya nimtazame mlangoni alipo simama.
“Yaaa”
“Kuna mzee anahitaji kuzungumza na wewe huku chini”
“Ninakuja”
Camila akanitazama kwa unyonge kisha akatoka chumbani humu, nikaichukua simu hii na kuipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Haloo”
“Hatuna muda wa kukuelezea, tunacho hitaji ni kufanya mabadilishano. Tunahitaji uweze kuwaambia wana sheria wako wabadilishe mali zote zitaandikwa kwa jina tunakalo kutajia la sivyo dada yako anakwenda kufa umenielewa”
“Yupo wapi dada yangu”
“Ethan usifa…..”
Niliisikia sauti ya dada Mery akizungumza huku akilia kwa nguvu sana.
“Naamini kwamba ume msikia”
“Munacho hitaji ni mali tu si ndio”
“Ndio”
“Mumezipata, niambieni ni wapi na saa ngapi niwapatie mali hizi”
Usikae mbali na simu, tutakufahamisha na ole wao uweze kumueleza mtu wa aina yoyote juu ya hili tuta kuua”
“Nimekuelewa”
 
Nilizunguza huku mwili wangu mzima ukinitetemeka kwa hasira, nikairudisha simu hii sehemu nilipo itoka kisha nikatoka ndani humu huku nikiwa nimevimba kwa hasira. Nikasimama katika ngazi za sebleni huku nikitazama watu hawa walio kusanyika huku wengine wakionekana wakiwa wameguswa sana na kifo cha mzee Klopp.
‘Ethan nahitaji kufanya kitu juu ya hili’
‘Kitu gani rafiki yangu’
‘Niambie ni nani na nani wanahusika katika mauaji utekaji wa dada yangu?’
‘Unamuona huyo mzee mwenye shati jeusi na shingoni ana kola nyeupe, na mkononi mwake amashika biblia?’
‘Ndio’
 
‘Huyo ni adui namba moja wa mzee wako na yeye ndio amekuja na hao vijana wakiwa kama mashemasi, ndio maana ili wawia urahisi kumteka Mery’
Nikaanza kushuka huku nikimkazia macho mzee huyu
‘Unataka kufanya nini, subiri sijamaliza maelezo ya swali ulilo niuliza’
‘Ethan nahitaji hadi kuna pambazuka hii kazi niwe nimesha imaliza’
‘Nimekuelwa rafiki yangu. Umemuona yule jamaa aliye bana nywele zake kwa nyuma?’
‘Ndio”
“Yule naye ni miongoni mwa wapangaji wa mpango huo. Sasa unaona wale mameja pale walio simama?’
‘Ndio’
Wale ndio wanatumikishwa na hao watu wawili nilio kuonyesha’
 
‘Ethan niwafanye nini?’
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu kwa hasira iliyo changanyikana na msiba mzito sana ambao nimeupata wa mzee huyu.
‘Waite wote na omba ukutane nao kwenye ofisi ya baba yako’
‘Sawa’
‘Ila usitumie hasira, kuwa mpole’
‘Sawa’
“Ethan”
Camila aliniuongelesha huku akinipa kitambaa cheupe.
“Nashukuru, muda ule ulisema nina itwa na nani?”
“Ni yule mzee mchungaji alihitaji kuzungumza na wewe”
Camila akanionyenyesha mchungaji huyo ambaye niliambiwa na Ethan.
“Sawa, kuna kikao kimoja nahitaji kufanya nao hawa watu, ila ninakuomba ukakae chumbani na mama yangu”
 
“Sawa, ila mama yangu yupo chumbani ana mfariji mama”
“Poa ila nakuomba ukakae naye”
“Sawa mpenzi wangu”
Camila akanibusu shavuni mwangu, kisha akapandisha ngazi za kuelekea gorofani. Nikaanza kutembea huku nikimtazama mchungaji huyo, ambaye baada ya kuniaona akatabasamu kwa bashaha.
“Ethan, tumsifu Yesu kristo”
“Milele amen askofu, samahani kwa kuchelewa kuitikia wito wako”
“Wala usijali mwanangu katika kristo, tunaweza tukapata muda na kuzungumza?”
“Sasa hivi”
“Ndio, ila ninakuomba tukazungumzie kwenye ofisi ya baba kule si unaifahamu”
“Yaa ninalifahamu lile lengo”
“Basi nakuomba utangulie ninakuja”
“Sawa mwanangu”
 
Mchungaji huyu akanibusu kwenye paji langu la uso, kisha akatoka sebleni hapa, huku nyuma yake akiongozana na mwanaume ambaye Ethan pia alinitajia. Nikaangaza angaza humu ndani, nikamuona mwanasheria wa makampuni akizungumza na mmoja wa mameneja. Nikamfwata na kumuomba nizungumze naye pembeni kwa sekunde.
“Ndio bosi”
“Kuna wageni wameelekea kule kwenye ofisi ya baba, ninakuomba ukake nao kwa muda kidogo mimi nina kuja na wageni wengine”
“Kuna kikoa mkuu?”
“Ndio, naokuomba unisaidie kuzungumza nao kwa muda”
“Sawa”
 
Mwanasheria akanielewa, kisha niwafwata hawa mameneja walio simama kikundi, walipo niona wakakatisha mada walio kuwa wakiizungumza huku dhairi inaonyesha kwamba ni mada ya siri, na mbaya zaidi yule meneja niliye msimamisha kazi masaa machache yaliyo pita naye ni miongoni mwao hawa wasaliti.
“Samahani wazee wangu, nathamini uwepo wenu na ninawashukuru sana. Tafadhali ninawaomba tukazungumze kitu kidogo kwenye ofisi ya baba”
“Sawa sawa mkuu”
“Mkuu hata mimi uliye nisimamisha kazi?”
“Ndio mzee wangu, hilo pia tutalizungumzi huko, unajua muda ule nilikuwa nina hasira na samahani kwa kukujibu vibaya na halikuwa lengo langu kufanya hivyo”
“Nashukuru sana muheshimiwa”
Mzee huyu alizungumza huku akitabasamu sana. Wakaanza kutoka ndani humu, nikashusha pumzi taratibu huku nikifikiria ni kitu gani ambacho ninakwenda kuzungumza nao.
“Ethan Klopp”
Dada mmoja aliniita huku akisimama mbele yangu
“Ndio”
 
“Mimi ni muandishi wa BBC hapa nchini Ujerumani, ninaweza kukuhoji maswali mawili matatu?”
“Naomba unipe kama nusu saa, nakuhidi nitakuja kwa ajili ya mahojiano yako”
“Sawa nashukuru”
“Karibu”
Nilijaribu kujikaza ili kuificha hasira yangu ambayo kusema kweli imenijaa kifuani mwangu. Nikaanza kutembea kuelekea katika jengo lenye ofisi ya mzee Klopp ambalo lipo mbali kidogo na jumba lake hili, ila vyote vipo katika eneo moja.
‘Ethan’
‘Ndio’
‘Ninakwenda kuzungumza nini?’
‘Kabla ya kuingia ofisi,nenda katika stoo’
‘Nikafanyaje’
‘Wewe nenda’
Nikabadilisha njia na kueleka katika stoo iliyopo katika jengo la ofisi.
 
‘Haya ninafanyaje sasa humu ndani’
‘Kuna bastola kwenye hiyo droo, ina risasi za kutosha na pembeni kuna kiwambo cha kuzuia risasi ifunge’
‘Weee unataka niende kuwaua?’
‘Sijasema uende kuwaua je wakitaka kukuua wewe utasemaje?’
‘Sawa’
Nikafungua droo, niliyo elekewa na Ethan na kweli nikakuta bastola, nikaichukua, kisha nikaichomeka nyuma ya kiuno changu na kufunika shati langu vizuri. Nikaona fimbo moja ya kuchezea mchezo wa gofu, nikaichukua huku nikiitazama vizuri, kisha taratibu nikaanza kutembea kuelekea katika ofisi ya baba.
“Mkuu niwewaweka katika ukumbi wa mkutano”
Mwanasheria aliniambia huku akinitazama mkononi mwangu.
“Naomba unisubiri hapa na hakikisha hakuna mtu ambaye anakuja humu ndani”
 
“Ila mkuu kazi yangu ni sheria na si ulinzi”
“Fanya hivyo kwa ajili yangu na kwa leo tu, haito jitokeza tena kwenye maisha yako sawa”
“Sawa mkuu”
Nikaondoka eneo hili na kumuacha mwanasheria akinishangaa sana. Nikafungua mlango wa ukumbi huu na kuwakuta watu wote wakiwa wamekaa huku wakiwa wameizunguka meza kubwa iliyopo humu ndani. Kila niliye muhitaji yupo ndani humu.
‘Funga mlango kwa code namba’
‘Sizifahamu’
‘Tisa ziwe tatu na ziro mbili na moja’
Nikaminya batani hizo kama Ethan alivyo niambia, nikatembea hadi kwenye kiti kilichopo mbele kabisa ya meza hiyo. Taratibu nikaa huku nikiatamana na watu hawa. Baadhi yao wanaonekana kujawa na dharua kubwa sana.
 
“Naamini sote tunafahamu ni kwa nini tupo hapa?”
“Wewe ndio umeitisha kikoa”
“Mwanangu katika kristo, mimi nilihitaji kuzungumza na wewe binafsi, ila si kwa kukaa na watu hawa”
“Mchungaji katika bwana tulia. Jamani mimi ni mdogo sana kwenu nina miaka hata kumi na nane sijafikisha. Jambo la kuachiwa makampuni makubwa ni kitu kilicho nistusha sana na kunichanganya kwa kweli”
“Nimeona niwaite wachache nyinyi ili niweze kuwasikia maoni yenu munasemaje juu ya mimi kuachia madaraka ya uangalizi wa kila kitu kwa mmoja wenu hmu ndani, au muna semaje?”
 
“Ni kweli mkuu ni maamuzi mazuri”
Meneja mmoja alizungumza huku akikenua meno yake kiasi cha kunifanya nitabasamu, ila moyoni nina ugulia kwa hasira kali sana.
“Ni kweli kiongozi ukituachia makampuni tunayo yaongoza na sisi tukawa tunakuletea asilimia, fulani labla kwa mwenzi hivi mambo yanaweza kuwa mazuri”
“Samahani wewe una simamia kampuni ya nini?”
“Mimi ninasimamia kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, kama mipira, viatu, jezi na kadhalika”
“Wastan wa mwaka kampuni yako ina ingiza kiasi gani?”
“Dola zaidi ya bilioni nne”
 
“Nashukuru, siwezi kuwauliza wote kwa maana nitawapoteze muda. Ila nina jambo moja muhimu sana naamini mchungaji utanisaidia kwenye maombi”
“Zungumza tu mwanangu katika kristo”
“Ni nani aliye mteka dada yangu MERY?”
Watu wote wakastuka huku wakinitazama kwa umakini sana.
‘Ethan nafanyaje’
‘Ninakupa nguvu, hakuna atakeya kuweza’
Nikasimama kwa haraka huku nikihema mihemo mizito kana kwamba nicheza mpira kwa muda mrefu sana pasipo kupumzika.
“Nimewauliza?”
Nilizungumza huku nikiigonga meza hii na hii fimbo ya kuchezea mpira wa gofu.  Mchungaji akatoa bastola yake na kuninyooshea.
 
“Dogo unahisi hii vita utaiweza kati yako na sisi. Baba yako aliweza kufanya ujinga ndio maana ametufikisha hapa tulipo. Tena muite mwanasheria wako aje hapa asainishe makubaliano ya kubadilisha mali zote na kuziingiza kwa majina tutakayo kuambia”
Nikamtazama mchungaji huyu, nikajikuta nikiruka mezani hapa hadi katika shemeu aliyo simama, kitendo hicho kikamuacha mdomo wazi. Nikamtandika konde zito la kifuani lililo mfanya arushwe mita kadhaa hadi ukutani na akaanguka chini. Mameneja walivyo ona hali imebadilika ndani ya chumba hichi wakanyanyuka na kutamani kukimbilia mlangoni, ila wakashindwa kutoka tayari nimesha ichomoa bastola yangu na kuwanyooshe.
 
“Anaye hitaji kufa akaguse ule mlango pale. Haya kila mmoja arudi kwenye kiti chake”
Mameneja wote wakarudi kwenye viti vyao na kukaa huku miili yao ikitetemeka.
“Kila mmoja aweke mikono yake juu ya meza”
Wote wakatii amri hadi mwanaume ambaye naye anahusika na mpango huu wa kumteka dada Mery na kuhitaji kuchukua mali kiurahisi. Nikaanza kuwapiga fimbo za mikono kwa kutumia fimbo hii ambayo imetengezwa kwa chuma. Mamenaja hawa wakazidi kulia kwa uchungu sana ila hapakuwa na hata mmoja wao ambaye alithubutu kufanya ujinga wa kunishambulia kwani kilicho tokea kwa mchungaji feki kila mmoja amekishuhudia, kwani ni jambo ambalo binadamu wa kawaida hawezi kulifanya na tukio kama hilo nahisi walisha liona kwenye baadhi ya filamu za Kimarekani kama Spider Men.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )