Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 23, 2018

UDSM Watii Agizo la Waziri Ndalichako....Wanafunzi 682 Waliofutiwa Usajili Warejeshwa Chuoni

juu
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimewarejesha wanafunzi 682 waliokuwa wamefutiwa usajili na chuo hicho.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo Jumanne Oktoba 23, 2018 Naibu Makamu Mkuu -Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Bonaventure Rutinwa amesema wanafunzi wote waliokuwa wamefutiwa usajili wameshapewa taarifa ya kurejeshewa usajili wao.

Amesema huo ni utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichoitishwa jana Oktoba 22, 2018  na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako kikihusisha uongozi wa UDSM na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Amesema kabla ya uamuzi huo wa jana, wanafunzi hao walikuwa wamepewa taarifa kuwa usajili wao umefutwa.

Amewataka wanafunzi ambao hawakupata taarifa za kurejeshewa usajili wawasiliane na chuo ikiwa ni pamoja na kufika chuoni kuchukua barua zao.

“Tumewajulisha TCU kuwa mwaka huu tuna uwezo wa kudahili wanafunzi wapya 14,660 na tukaainisha kwa kila programu,” amesema na kubainisha kuwa  chuo hicho bado kina nafasi 4,000 ambazo ziko wazi baada ya kudahili wanafunzi zaidi ya 7000.

Amesema licha ya leo kuwa ratiba ya kufungwa kwa ajili ya maombi kwa awamu ya nne, UDSM imeongeza muda wa siku tano ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaomba.

Profesa Rutinwa amebainisha kuwa mkanganyiko wa udahili ulitokana na tafauti iliyopo kati ya idadi ya wanafunzi wanaohitajika chuoni na kanuni zilizopo katika kitabu cha mwongozo wa TCU.

‘Mkanganyiko wa udahili UDSM umetokana na mfumo mpya ambao wanafunzi wanapaswa kupeleka moja kwa moja maombi kwa vyuo wanavyovitaka na TCU ikibaki kwenye kudhibiti ubora,” amesema.

“Katika kutekeleza hilo wanafunzi wengi waliomba UDSM sisi tukawachagua lakini baada ya uchaguzi unapaswa kuwapeleka TCU kuwaangalia kama wana vigezo na uwezo.”

Ameongeza, “‘Tulipopeleka wanafunzi wetu katika baadhi ya programu TCU wakasema idadi tuliyowapa  ni kubwa kuliko idadi inayoonekana kwenye kitabu cha mwongozo wa udahili, lakini sisi tukawa tunaona ni suala la tafsiri ya kanuni kwa sababu hizo kanuni ziliwekwa wakati TCU wakiwa wanapokea maombi.”
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )