Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 23, 2018

Watoto wa Familia moja wachinjwa Kinyama Huko Bukoba

adv1
Watoto wawili wa familia moja wamechinjwa na miili yao kutupwa kichakani katika kijiji cha Mashule wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera, ikiwa ni baada ya kupotea kwa siku moja.

Mkuu wa Wilaya hiyo,  Deodatus Kinawilo amethibitisha tukio hilo na kubainisha kuwa amewaagiza polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

Amewataja watoto hao kuwa ni Auson Respikius (7) na Alistidia Respikius (5) walioondoka nyumbani Jumapili Oktoba 21 na miili yao kupatikana jana.

Baba wa watoto hao,  Respikius John amesema waliaga wanakwenda kucheza na wenzao, aliwaogesha na kuwaandalia nguo.

Amesema baada ya kucheza walirejea nyumbani jioni na kubadili nguo na kuondoka tena lakini hawakuonekana hadi miili yao ilipokutwa kichakani.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )