Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 1, 2018

Watu 1,300 kuzikwa kaburi moja Indonesia

juu
Maandalizi  ya kuizika miili ya takribani watu 832 waliofariki baada ya nchi ya Indonesia kukumbwa na tetemeko la ardhi pamoja na Tsunami yameanza.

Hapo awali kikosi maalumu kilielekezwa kuandaa kaburi la miili 300 lakini maelekezo mapya yametaka kaburi hilo liwe kwa ajili ya watu 1,300

Aidha serikali imesema kuwa idadi ya waliofariki na kujeruhiwa huenda ikaongezeka kutokana na kutoonekana kwa watu wengi huku juhudi za kufukua vifusi zikiendelea.

Uduni wa vifaa vya uokoaji unaelezwa kuchangia kuchelewesha kutoa miili ya watu 60 iliyokwama kwenye vifusi vya jengo moja la hoteli iliyoanguka katika Jiji la Palu lenye watu wapatao 300,000 ambapo watu wengi zaidi wamepatikana wakiwa wamekufa.

Rais wa Indonesia, Widodo, amekubali kupokea misaada kutoka nje baada ya kutembelea eneo hilo Jumapili ambapo ametaka zifanywe juhudi za usiku na mchana kukabili madhara ya tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa ‘magnitude’ 7.5.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )