Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 1, 2018

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongomano la Wakulima

juu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la siku tatu la wakulima takribani 2,400 kutoka mikoa yote nchini.

Kongamano hilo ambalo ni la maadhimisho ya  miaka 25 tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) litafanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Oktoba 3, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 1, 2018 juu ya ujio wa Majaliwa pamoja na kuadhimisha miaka hiyo 25 ya Mviwata, mkurugenzi mtendaji wa Mviwata, Stephen Ruvuga amesema waziri mkuu atafungua maadhimisho hayo pamoja na kuzungumza na wakulima hao.

Ruvuga amesema kongamano hilo pia litaambatana na  kongamano la kitaifa la wakulima kuhusu Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda nini nafasi ya wakulima wadogo, pamoja na mkutano mkuu wa 23 wa Mviwata.

Amesema watu wa kada mbalimbali  na mashuhuri wakiwemo mawaziri, wabunge, viongozi na watendaji waandamizi wa Serikali, wawakilishi wa balozi, washirika wenza, marafiki wa Mviwata na wadau toka ndani na nje ya nchi wanategemewa kuhudhuria akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ambaye atakuwa mtoa mada mkuu katika kongamano hilo.

Ruvuga amesema kongamano hilo litajadili jinsi gani wakulima wanaweza kujipanga na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuangalia viwezeshi muhimu vya kufanikisha ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa uchumi wa viwanda ambao ndio mkakati wa Serikali ya awamu ya tano.

Wengine watakaoshiriki ni kamishna wa ardhi, mkurugenzi wa NDC, Profesa Damian Gabagambi pamoja na Profesa Issa Shivji.

Naye Ofisa Sera na Utetezi wa Mviwata, Thomas Laiser amesema mustakabali wa wakulima upo kwa wakulima wenyewe hivyo ujio wa waziri mkuu wa kuzungumza na wakulima utainua ari mpya na kuona namna Serikali inavyoendelea kuwathamini.

Laiser amevipongeza vyombo vya habari kwa namna ambavyo vimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wakulima wanapata manufaa kutoka kwa Serikali yao, huku akiviomba kutochoka kuhabarisha wananchi.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )