Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 10, 2018

Baada ya Kupongezwa na Ikulu, BASATA Nao Wampongeza Msanii Diamond Planumz

juu
Baraza la sanaa Taifa (BASATA) limechukua uamuzi wa kumpongeza msanii wa muziki nchini Tanzania Naseeb Abduly alimaarufa Diamond Platnumz kwa kuonyesha moyo wake wa kujitolea. 

Baraza hilo limetumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwa msanii Diamond na kuchukua nafasi hiyo kuwaomba wasanii wengine kuiga mfano wa Diamond kuweza kuwa msaada katika jamii inayowazunguka.

“Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), linampongeza msanii Nasibu Abdul maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ kwa moyo wa kizalendo aliouonesha wa kujitolea shilingi milioni 68 kumalizia ujenzi wa shule iliyopo Wilayani Sumbawanga.

"Kitendo hiki kinazidi kuishawishi jamii kuithamini, kuilinda na kuipenda sanaa yetu nchini. Aidha Baraza linapenda kutumia nafasi hii kuwasihi wasanii wengine nchini kuiga moyo huu ili tuweze kuisaidia jamii yetu inayotuzunguka. SANAA NI KAZI, TUIPENDE NA KUITHAMINI.#HongeraDiamondPlatnumz”
-Wameandika BASATA

Hatua hii imekuja baada ya akaunti ya Ikulu Mawasiliano kumpogeza msanii huyo kwa kuamua kujitolea kujenga shule ambayo ilipewa jina lake la Diamond Platnumz Shule ya Msingi.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )