Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 16, 2018

Barabara ya Morogoro kwenda Dodoma kujengwa upya

juu
Barabara ya Morogoro-Dodoma yenye urefu wa Kilomita 259 inasanifiwa upya ili ijengwa kwa viwango vya ubora unaoendana na mahitaji ya sasa.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema mpango huo unafanywa katika mwaka wa fedha 2018/19 na mara baada ya usanifu kumalizika watapa michoro na kufahamu gharama halisi za ujenzi.

Naibu Waziri alisema hayo hivi karibuni mjini Morogoro alipofanya ziara ya ukaguzi wa matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali kutoka Dodoma hadi Moropgoro yakiwemo ya Kibaigwa, Gairo na kuangalia shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara ya Morogoro- Dodoma.

Alisema licha ya kuendelea kuihudumia barabara hiyo kuu serikali imekuja na mpango mwingine wa kufanya usanifu kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 ili kupata michoro ambayo itaelezea gharama halisi ya kujenga barabara mpya katika kiwango cha ubora na mahitaji ya sasa.

Kwandikwa alisema serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu mbalimbali ikiwemo hiyo ya Morogoro-Dodoma ili ziweze kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo na kwamba babrabara hiyo ni ya zamani kwani imejengwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na sasa imechakaa na kuzeeka.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )