Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 21, 2018

China Yatangaza Neema Kwa Wakulima wa Karanga,Ufuta na Maharage......Inataka Tani 10,000 za Mazao Hayo

juu
Ubalozi wa Tanzania Beijing, China umebainisha kuwa kampuni moja nchini China imewasilisha ombi la kununua ufuta, karanga na maharage ya soya kutoka Tanzania.

Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi Desemba 20, 2018 na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) na kusainiwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa mamlaka hiyo, Theresa Chilambo inaeleza kuwa kampuni hiyo inalenga kununua bidhaa hizo kwa vigezo.

Kampuni hiyo inahitaji ufuta tani 3,000 kwa mwezi, karanga tani 2,000 kwa mwezi na maharage ya soya tani 5,000 kwa mwezi

Theresa amesema ufuta unaotakiwa ni wa ubora wa Taifa daraja la pili.Amebainisha kuwa hata karanga na maharage ya soya yanayohitaji  nayo ni katika kiwango hicho cha ubora.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )