Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 8, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 41

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
“Ethan ngoja kwanza usimuue”
Ethan alizungumza huku akinitazama.
“Kwa nini?”       
“Kwa kumtumia huyu basi tutahakikisha huyo mwana mama anaenguliwa katika kasi za kugombania uraisi na itazidi kumpa nguvu baba mkwe wako kushinda uchaguzi wa uraisi”
Ethna alizungumza kwa upole, kabla sijafanya chochote simu ya mwanasheria huyu iliyopo kwenye koti lake la suti ikaanza kuita, nikampasa kwa haraka na nikaitoa. Nikakuta namba hiyo ni ya mke wake, nikamuonyesha kisha nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Mume fiki wapi mume wangu. Nipe habari njema”
“SIO HABARI NJEMA, NI HABARI MBAYA MUME WAKO AMEFARIKI DUNIANI”
Nilizungumza kwa sauti nzito na iliyo jaa mikwaruzo mingi sana na kumfanya mwana mama huyo kukaa kimya kwa sekunde kadhaa akisikilizia sauti yangu.

ENDELEA   
“JIANDAE NINAKUJA KWA AJILI YAKO”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikakata simu huku nikimtazama mwanasheria wangu aliye amua kunisaliti kwa ajili ya mke wake.
“Ngoja nikachukue gari”
Ethan alizungumza huku akiondoka katika eneo hili. Mwanasheria hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kuendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake.
“Endapo nitagundua umefanya udanganyifu kwenye kitu chochote ndani ya kampuni yangu. Ninakuapia kwa jina la marehemu yangu. Lazima nitakua, umenielewa wewe mpuuzi”
Mwanasheria akazidi kulia kwa uchungu sana huku akionekana kujutia kwa maamuzi ya kijinga aliyo yafanya.
“Mke wako kwa nini amekuwa na roho mbaya kiasi hichi ehee?”
Camila alimuuliza mwanasheria, ila mwanasheria akaishia kumtazama Camila tu.
“Ila Mungu ni mwema, unakumbuka jana nilikuambia tuondoke pale hospitalini?”
 
“Ndio”
“Na nilikueleza kwamba yule sio mama yangu”
“Ndio”
“Niliustukia mpango wa huyu mzee. Yaani sijui ulikuwa unanichukuliaje. Kumbuka nimebakisha siku kumi tu kuingia umri wa miaka kumi na nane sasa wewe endelea kuleta ujinga wako mzee. Mimi sio mtoto na hata nikiwa katika umri huu huwezi kunidanganya. Mjinga wewe”
Tukamuona Ethan akisimamisha gari katika eneo lenye barabara. Akashuka na kutufwata sehemu hii tulipo. Akamnyanyua mwanasheria wangu na kumfunga pingu za mikononi mwake. Akampeleka moja kwa moja kwenye gari na kumuingiza siti ya nyuma huku nasi tukiwa nyuma yao.
“Mjini kwa sasa kila sehemu ina kaguliwa na askari kuwatafuta nyinyi mulipo, kwani habari ya kutekwa kwenu imesambaa kila mahali. Sawa”
 
“Sawa je wewe uungani nasi?”
Camila alizungumza huku akimtazama Ethan usoni mwake.
“Hapana mimi nitaondoka na hii pikipiki”
“Sawa”
“Ila angalizo, hakikisheni kwamba munampeleka katika sehemu ambayo itakuwa ni salama kwa nyinyi kumshikilia kwa kipindi chote katika kuhakikisha kwamba muna muangusha mke wake katika kumtoa katika kinyang’anyiro cha kuiongoza nchi hiyo.”
“Sawa nimekuelewa”
“Ila nitaendelea kuwalinda kwa ukaribu na sasa hivi Ethan hakikisheni kwamba kila hatua ya jambo linalo watatiza munaipiga na nitakuwa pamoja nanyi. Mumenielewa”
“Sawa”
“Shemeji safari jema”
“Nashukuru”
 
Tukaingia kwenye gari siti za mbele. Camila akaishika bastola yake na kumuelekezea mwanasheria aliye kalishwa siti ya nyuma. Nikawasha gari hili na kuanza kuondoka katika eneo hili kwa mwendo wa kasi. Kutokana gari hili lina GPRS haikuwa tabu kwa sisi kuusaka mji wa Berilin amboa ndipo tunapo ishi.
“Baby”
“Mmmm”
“Yule umesema anaitwa Ethan?”
“Ndio”
“Ni mtu kweli?”
Nikamtazama Camila usoni mwake, kisha nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba sio mtu. Camila akanielewa jibu langu huku akinitazama machoni mwangu.
 
“Ethan”
Mwanasheria aliniita kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyenyekevu, nikamtazama kwa kupitia kioo kidogo kilichopo juu upande wangu wa kulia.
“Ehee”
“Vita ulio ingia ni kubwa sana mwanangu. Ninakuonea huruma kubwa sana”
“Pumbavu wewe nyamaza. Unahisi kwamba ninaogopa. Kama ulishindwa kuniua leo basi tambua kwamba hamuto niweze kuniua hata siku zijazo. Hata mukija watu laki, Mungu yu pamoja nami na hamutoweza kufanya lolote kwangu”
Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikiendelea kuendesha gari hili kwa kasi.
“Natambua hilo ila vita hii amekuachia baba yako mzee Klopp”
 
“Eti ehee?”
“Ndio, mali alizo zulimu, watu alio waua kipindi cha uhai wake. Damu zao zipo mikononi mwako, kwani wewe ndio mrithi wa mali zake. Leo hii umenionyesha na wewe una ukatili kama wa baba yako kwa maana umemuua dereva wangu ambaye hakuwa na hatia yoyote kwenye hili swala”
Nikayafumba macho yangu kwa sekunde kadha kisha nikafunga breki za gafla hadi Camila akashangaa. Nikashuka kwenye gari na kufungua mlango wa siti za nyuma, nimatoa mwana sheria kwa nguvu na kumbwaga chini. Nikaanza kumpiga mateke ya tumboni mwake huku nikimtukana matusi ya kila aina.
 
“Baby baby acha tafadhali”
Camila alizungumza huku akanisogeza pembeni kwani mateke niliyokuwa ninampiga mwana sheri kwa hakika yanaweza kumsababishia kifo.
“Mume wangu tuliza jazba kidogo. Kumbuka huyu mzee tunamuhitaji katika haya mapambano. Unavyo endelea kumpiga hivyo utazidi kumsababishia matatizo na mwishowe atakufa sawa mume wangu”
Camila alizungumza huku akiwa amenishika mashavu yangu. Akanibiga busu moja matata mdomoni mwangu, busu hili taratibu likazifanya hisia zangu za hasira kuanza kushuka taratibu na nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
 
“Tambua nina kutegemea sana mume wangu. Tambua hii vita ni ya kwetu wote. Maisha ya baba yangu yapo hatiana na hata familia yangu kwa sasa ipo mashakani. Tafadhali ninakuomba mume wangu uwe mpole sawa baba”
“Nimekuelewa mke wangu”
Nilizungumza kwa upole kisha nikamnyanyua mwanasheria na kumuingiza ndani ya gari. Tukaendelea na safari hii huku akilini mwangu nikifikiria ni sehemu gani ambayo ninaweza kumpeleka huyu mwana sheria. Taratibu nikapunguz amwendo wa gari na kulisimamisha pembezoni mwa barabara. 
 
“Huyu mtu mjini hatuwezi kumpeleka mke wangu ni hatari”
“Kweli ni hatari mume wangu, nami nilikuwa ninaliwaza jambo hilo ila nikashindwa tu kukuanza”
“Hufahamu sehemu yoyote ambayo tunaweza kupata nyumba ya kumhifahdhi huyu shetani?”
“Mmmmm sifahamu”
Tukiwa katik ahali ya kujiuliza maswali ya hapa na pale, tukaanza kuona helicopter mbili za jeshi la nchi hii ya Ujerumani zikija mbele yetu. Nikakata kuwasha gari ila Camila akanizuia.
“Wamekuja kwa ajili yetu hawa”
“Una uhakika?”
“Ndio mume wangu, naamini kwa kutumia satelaiti wameweza kufahamu sehemu tulipo”
“Umejuaje?”
 
“Kumbuka hata kwa kupitia sura zetu tunaweza kutafutwa na kujulikana ni wapi tulipo na mbaya zaidi pale ulipo shuka kwenye gari na kuanza kumuadhibu huyu mzee nayo pia imechangia”
Camila alizungumza huku tukishuhudia helicopter hizo zikianza kusimama taratibu mita kadhaa kutoka sehemu ilipo gari letu. Wakashuka wanajeshi zaidi ya kumi na mbili, taratibu tukashuka kwenye gari hili. Wanajeshi hawa wakafika katika eneo hili.
“Ninaitwa Camptein Gudluck, kutoka jeshi la anga. Tupo hapa kwa ajili ya kuwaokoa.”
 
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akitupa mikono.
“Mumefahmu vipi kwamba tupo hapa?”
Nilimuuliza mwanajeshi huyu huku nikimkazia macho usoni mwake.
“Kupitia satelaiti”
Mwanajeshi huyu alizungumza huku akinionyesha alama ndogo inayo onekana kwenye simu yake aina ya iphone 6. Mapigo ya moyo yakanistuka mara baada ya kuona chata ndogo kwenye mkono wa mmoja wa huyu mwanajeshi. Chata hii ikanikumbusha vijana wa mwanasheria ambao aliwaagiza kwenda kunitafutia mama yangu nchini Tanzania.
 
‘Ohoo Mungu wangu, tumeingia tena mikono ni mwao’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimkanyaga Camila kwenye mguu wake. Gafla helicopter moja ikalipuka na kutuchanganya watu wote katika eneo hili.
“Rudi kwenye gari”
Nilimuambia Camila kwa sauti ya ukali. Camila hakuhitaji kupoteza muda, kwa haraka akarudi kwenye gari huku nami nikirudi kwenye gari. Nikaliwasha gari hili na kuanza kulirudisha nyuma na kuwafanya wanajeshi hawa kuendelea kutushambulia kwa risasi.
 
“Mungu wangu ni kina nani wale!!?”
Camila alizungumza huku akiwa amejawa na mstuko mkubwa sana.
“Ni watu wa huyu mzee”
“Ohoo samahani mume wangu kwa kukuamisha kwamba ni watu wa serikali. Tukashuhudia helicopter nyingine nayo ikilipuka mlipuko mmoja mkali sana. Wanajeshi wanao tushambulia tukawashuhudia jinsi wanavyo anguka mmoja baada ya mwengine.
 
“Nilikuambia Ethan, hii vita si ndog….”
“Nyamaza nguruwe wewe”
Nilizungumza huku niligeuza gari hili kwa kasi sana, likayumba kidogo ila nikafanikiwa kuliweka sawa.
“Tupa hiyo simu ya huyo mzee”
Tuliisikia sauti ya Ethan akizungumza nasi, tukatazamana na Camila usoni mwetu. Nikaanza kujipapasa mifukoni mwangu na kuipata simu ya mzee huyu, nikashusha kioo kidogo na kuitupa dirishani na kuanza safari ya kutokomea sehemu ambayo kwa kweli hatuifahamu na hatujui ni nini hatima yetu na mwanasheria wangu huyu.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )