Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 16, 2018

Serikali Yatoa Waraka MPYA wa kukariri darasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini

juu
Serikali imetoa waraka unaoelekeza utaratibu mpya wa kukariri darasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kuanzia Januari mwakani.

Waraka wa Elimu Namba 2 wa Mwaka 2018, kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, umetokana na kukithiri kwa malalamiko kutokea kwa wazazi na walezi wakilalamikia kutoshirikishwa ipasavyo katika kufanya uamuzi wa mwanafunzi kukariri. Pia kukosekana kwa uwazi na ushirikishwaji madhubuti kwenye maamuzi ya kukaririsha darasa wanafunzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Edicome Shirima, maombi ya kukariri darasa la kwanza, pili na tatu yatashughulikiwa na halmashauri husika. Dk Shirika alieleza kuwa kukariri darasa kwa wanafunzi wa darasa la nne, tano na sita na wenzao wa kidato cha kwanza, pili, tatu na tano yatashughulikiwa na mkoa.

Aidha, kupitia waraka huo, Dk Shirima ameelekeza kuwa maombi ya kukariri darasa kwa wanafunzi wa darasa la saba na wale wa kidato cha nne na sita ambayo hayo ni madarasa ya mitihani ya mwisho ya kitaifa, maombi yao yataendelea kutumwa  kwenye ofisi yake.

Alisema iwapo mwanafunzi akikubaliwa kukariri darasa kwenye ngazi hizo atapewa fursa ya kukariri mara moja na endapo mamlaka inayohusika ikiona kuna umuhimu wa kukariri kwa mara ya pili ndio atapewa fursa hiyo.

Waraka huo umeelekeza kuwa mzazi wa mwanafunzi wa darasa la kwanza, pili na tatu ili mtoto wake akariri darasa atatakiwa kuandika barua ya maombi ya kukariri darasa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika. Kwa wanafunzi wa darasa la nne, tano na sita na kidato cha kwanza, pili, tatu na tano mzazi au mlezi atatakiwa kuandika maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Kuhusu wanafunzi wa darasa la saba na wale wa kidato cha nne na sita, Dk Shirima alisema mzazi anatakiwa kupitisha maombi kwanza kwa mkuu wa shule na mkurugenzi wa halmashauri husika kabla ya kuyawasilisha kwenye ofisi yake.

Aliongeza kuwa kwenye maombi yao hayo kila barua inapaswa kuwa na picha mbili za mwanafunzi husika aina ya pasipoti saizi, namba ya kuandikishwa shule pamoja na nyaraka zozote muhimu kulingana na sababu ya ombi la kukaririshwa darasa kwa mwanafunzi. 

Pia kwenye waraka huo ameelekeza kuwa kukariri darasa kwa wanafunzi wanaoshindwa kufikia viwango vya ufaulu vilivyowekwa na shule hasa kwa wanafunzi wa darasa la nne na kidato cha pili, bado wanakuwa na sifa ya kumaliza ngazi husika ya elimu bila ya kukariri.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )