Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 30, 2018

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Akaunti Halali Za Mitandao Ya Kijamii Ya Instagram Na Twitter Za Kangi Lugola, Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ya Nchi

adv1
Baada ya kuwepo kwa akaunti feki ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambao ulikua unatoa taarifa mbalimbali kwa jamii kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ujumla, kuanzia leo Disemba 30, 2018, Wizara inatangaza rasmi kwa jamii, akaunti halali zilizosajiliwa kwa jina la Mheshimiwa Waziri Kangi Lugola, kama ifuatavyo;

    officialkangi_lugola (Instagram)
    @kangi_lugola (Twitter)

Taarifa zote zitakazotolewa katika kurasa za akaunti hizi zitakua sahihi.

Kwa hatua hiyo, Wizara inaendelea kutoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha kwa kutumia jina la Kangi Lugola kusajili akaunti yoyote na kutoa taarifa za Waziri huyo kupitia akaunti feki hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Wizara inawaomba Watanzania waendelee kupata taarifa zake zaidi kupitia tovuti yenye anuani; www.moha.go.tz na twitter ya Wizara kwa akaunti ya Msemaji Mambo ya Ndani.  
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )