Upelelezi wa kesi ya kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Bilioni 188.9 kupitia mashine ya risiti za kielekroniki (EFD) inayomkabili mfanyabiashara Mustapha Kambangwa (34), bado haujakamilika.
Kambangwa, mkazi wa Mbagala Kongowe anakabiliwa na mashtaka manne Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, likiwemo la kutakatisha fedha .
Kwa mara ya kwanza, Kambangwa alifikishwa mahakamani hapo Desemba 7, 2018 kujibu mashtaka manne katika kesi ya uhujumu uchumi namba 19/ 2018.
Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai jana Alhamisi Desemba 20, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa utetezi kuwasilisha hoja za kupinga shitaka dhidi ya mshtakiwa.
Hata hivyo, hoja hizo hazikuwasilishwa mahakamani hapo baada ya Ester kudai kwamba wakili mwenzake Christopher Msigwa, ambaye ndio mwenye jalada halisi la kesi hiyo ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa.
Baada ya upande wa mashtaka kueleza hayo, wakili wa utetezi Shamo Shadrack, alidai ofisi ya waendesha mashitaka ina mawakili wengi na kuhoji sababu za kuumwa kwa mtu mmoja kuzuie kesi kuendelea.
" Kuumwa kwa mtu mmoja kusizuie kuendelea kwa kesi, kwani mawakili wote wanafanya kazi ofisi moja hivyo tunaomba tarehe ijayo ambayo ni Desemba 24, 2018 tuweze kuwasilisha hoja zetu, " alidai Shadrack.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Janeth aliwataka upande wa mashitaka kuhakikisha shauri hilo linaendelea hata kama yule wa awali bado anaumwa aendeshe mwingine.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 24, 2018 na mshtakiwa kurejeshwa rumande.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )