Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 15, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 190 na 191 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       
Nikaweka upande wa video na kuigeuza simu yangu sehemu alipo Osam Bin Laden na kundi lake, nikajikuta macho yakiwa yamenitoka kwani watu wote walio zifunika sura zao kwa vitambaa ni sura ya Osama Bin Laden.
“Mage umeona hichi kinacho tokea hapa?”
“Mbona wamefanana jamani?”
“Logate hii inakuwaje?”
“Hata sisi tunashangaa huku hatujui Osama ni nani kati yao kwa maana wote wanafanana”
Hatukujua ni nini cha kufanya hadi watu wote tulipo ruhusiwa na muongoza sherehe(MC) tukae kwenye viti vyetu.
   
ENDELEA
Tukaendelea kuifwatilia sherehe hii huku tukijitahidi kuhakikisha kwamba waarabu hawa walio jifunga vitambaa kwenye sura zao tuna wafwatilia nyendo zao hadi katika ukaaji wao.
 
“Tunatakiwa kuwa makini, ninaona jinsi walinzi wanavyo tutazama tazama”
Magreti alizungumza huku akiwa ameniegemea kwenye bega langu.
“Yaaa ninawaona. Logate vipi umefanikiwa kumjua ni yupi Osama?”
“Hapana bado tunaendelea kumtafuta ila tunaomba muda kidogo”
“Sawa”
Tukaendelea kupata vinywaji taratibu. Huku muongozaji wa hii sherehe akijitaidi kuhakikisha kwamba tunafurahia sherehe hii kwa kuzungumza maneno yaliyo wachekesha watu wengi humu ndani.
“Ila tutaangalia muda muda wa chakula ni lazima watasimama sasa kwenye kula hapo ndio tutaweza kuwaona”
 
“Ngoja tusubiri tuangalie”
Muda ukazidi kusonga mbele, ukafika muda ambao  mimi na Magreti tunausubiria kwa hamu. Kama kawaida maharusi wakaanza kutangulia kwenda kuchukua chakula, wakafwata wazazi wa pande zote mbili pamoja na ndugu, ila katika meza waliyo kaa hawa waarabu hapakuwa na hata mmoja aliye nyanyuka.
“Hawali au?”   
Magreti alizungumza huku akiwatazama kwa macho ya kuiba iba.
“Wala sifahamu.”
Ikafika zamu yetu kunyanyuliwa kakika meza yetu pamoja na wezetu walio kaa humu. Tukapanga foleni huku Magreti akitangulia mbele na mimi nikiwa nyuma yake huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimemshika kiunoni. Akachukua sahani mbili na tukaanza kupita kwa kila muhudumu na akatupakulia chakula kisha tukarudi katika viti vyetu.
 
“Logate sisi tunagonga msosi ila hatuelewi hawa jamaa kama wanakula ua hawali kwa maana hawajakunywa kinywaji  wala kula chakula”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikindikiza na paja la kuku lililo kaangwa vizuri na kunona sana.
“Wakinyanyuka nitaweza kumfahamu ni nani Osama kwa kutembea kwao”
“Sawa”
“Ila jamani hatukaribishani”
“Ester karibu”
“Mmmmm hadi niwaambie”
“Livna yupo?”
“Yupo hapa  anawaona jinsi munavyo kandamiza hiyo minyama”
“Ila Dany mpenzi wangu upo vizuri katika kugonga msosi, mmmm chakula chote hicho”
 
“Ahaaa jamani nipo kazini”
“Alafu mkuu, mumeo  alikuwa ananilazimisha kuongeza msosi hadi nikajisikia aibu”
“Hahahaaaaaa”
Mazungumzo yetu tunayazungumz a kwa sauti ya chini sana na ningumu sana kwa mtu kuweza kustuka kama tunazungumza na watu ambao  hawapo ndani ya ukumbi huu.
“Angalieni musije mukavimbiwa”
“Ndugu waalikwa tukiwa tunaendelea kupata chakula kilicho andaliwa kwa ubora wa hali ya juu. Tunawakaribisha muweze kutoa zawadi kwa maharusi wetu, na wazazi watafwatia nyuma”
Muongoza sherehe alizungumza, tukawaona waarabu hawa wakinyanyuka kwa pamoja na kuanza kuelekea walipo simama maharusi.
 
“Mtu wa tatu kutoka mbele ndio Osama Bin Laden,  kutembea kwake na hawa wezake ni tofati. Mguu wake mmoja wa kulia anachechema kiasi, japo si rahisi kumuona”
Tuliisikia sauti ya Logate katika vinasa sauti vyetu tulivyo vivaa masikioni mwetu. Sote tukamtazama mtu wa tatu kutoke mbele. Kweli tukaweza kuona udhaifu katika kumbea kwake.
“Hakikisheni sasa hawatoki kwenye targrt yenu”
“Tumekusoma tuachieni hilo jukumu”
Wakampa mkono wa shukrani bwana harusi pamoja na bibi harusi, hawakuwapa mikono wasimamizi wa harusi hii, hatukulijali sana hilo, wala hawakurudi kwenye viti vyao na moja kwa moja wakaanza kueleleka nje. Walinzi kadhaa walimo humu ndani wakanza kutangulia nje. 
 
“Ngoja watoke”
Nilizungumza huku niikiendelea kumalizia vipande vya vyama katika sahani yangu. Wakatoka watu wawili watatu ambao si walinzi kabisa. Nikachukua tishu na kujifuta mikononi mwangu, nikasimama na Magreti naye akasimama na tukaanza kutembea kwa pamoja huku nikiwa nimemshika kiuno. Watu wengi ndani humu wakabaki wakiwa wametukodolea macho, wengi wao wanamtazama Magreti. Tukafika nje na kuwaona walinzi walivyo wazunguka watu hawa walio valia kanzu, wote wanaelekea katika maegesho ya magari  yaliyopo mbali kidogo na hii sehemu ya ukumbi.
“Samahani wapendwa hamuruhusiwi kueleke huku kwa sasa”
 
Mlinzi mmoja alizungumza huku akisimama mbele yetu.
“Kwa nnini kamanda?”
“Kuna viongozi  wanaondoka, wakiondoka basi ndio tutawaruhusu”
“Sawa kaka asante, baby tusubiri kwanza”
Magret alizungumza huku akinishika kifua changu, tukatafuta sehemu na kusimama huku macho yetu tukihakikisha kwamba gari wanazo ondoka nazo tunaweza kuziona vizuri”
“Logate umesikia tulicho ambiwa?”
“Ndio, ninawatumia picha ya gari aliyo panda Osama”
“Pao, amepanda peke yake?”
“Yupo na mlinzi wake ambaye naye anafanana naye”
“Poa”
Kijimlio kidogo cha simu yangu ikanifanya niitoe mfukoni, kabla ya kuangalia hii picha nikatazama eneo hili tulilo simama kwa juu kuna camera yoyote ambayo inaweza kuchukua kile niitakacho kitazama kwenye simu  yangu. Kwa bahati nzuri hakuna kamera yoyote, nikaifungua picha hii na kuona BMW X6 yenye namba za usajili I86GSW.
“Hii namba ya ni ya nchi gani?”
“Iraque, walikuja na gari zao na zipo gari nne zinazo fanana sasa munatakiwa kuwa makini sana”
“Poa.”
Tukaziona gari hizo zikiondoka katika eneo hili, zikatoka getini na kupotelea kwenye upeo wa macho yetu.
“Kiongozi tunaweza kuondoka sasa?”
“Ndio munaweza kuondoka”
Mlinzi huyu alizungumza mara baada ya kuwasiliana na mwenzake.
 
“Poa poa kaka. Hivi ni kiongozo gani huyo aliye ondoka hapa?”
“Hampaswi  kufahamu, kama munaondoka munaweza kuondoka”
“Samahani mwaya kaka, mume wangu amelewa ana maswali ya ajabu ajabu”
“Hakuna tabu dada”
Tukaanza kutembea kwa hatua za kwaida kuelekea lilipo gari letu, tukaingia ndani, nikaliwasha na kuliweka sawa. Taratibu nikaanza kueleka getini, tukafanyiwa ukaguzi kama tulivyo ingia humu ukumbini, kisha gari zikaruhusiwa kutoka.
“Logate tumewapoteza sijui wameelekea wapi tutumieni ramani ya wanapo  elekea”
“Tayari nimesha tuma kwenye simu ya Mage”
“Mage hembu angali”
Mage akaitoa simu yake kwenye kipochi chake.
“Nimeipata”
 
“Wanaelekea wapi?”
“Wanaelekea……kunja kushoto hapo mbele”
Nikapunguza mwendo wa gari na kukunja kushoto kisha nikaanza kuongeza mwendo wa gari uzuri ni kwamab ni usiku na hakuna foleni ya magari barabarani.
“Kunja kushoto tena. Gari zao zipo kasi sana ongeza mwendo baba”
“Kaa vizuri kwenye siti”
“Mimi nipo vizuri, kazi ni kwako”
Nikazidi kuongeza mwendo hadi nikafika spidi mia mbili na kuanza kuelekea spidi mia mbili na kumi.
“Kuli, kulia”
Kutokana nipo kwenye mwendo kasi na kona aliyo niambia Magreti ipo mita chache kutoka nilipo, ikanilazimu kunyanyua handbrek huku nikikunja kona hii, jambo lililo pelekea gari kuserereka sana, nikajitahidi kuhakikisha kwamba ninahimili mserereko huu, nilipo kaa sawa. Nikaendelea na kasi zangu jambo lililo mfanya Magret kunitazama mara mbili mbili.
 
“Tutakufa?”
“Hatufi niambie wanalekea wapi”
“Nyoosha, kwa sasa wanakaribia Mwenge”
“Watakuwa wanaelekea wapi?”
“Wakinyoosha mazima watakuwa wanaelekea Mbezi Beach”
“Poa poa”
Sikufwata sheria za mataa ya humu barabarani, nilipo pata nafasi ya kupita nikahakikisha kwamba ninapita pasipo kusubiri kuruhusiwa kupita.
“Wanaeleka Mbezi Beachi”
“Hawa tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunawafikia kabla hawajafika katika sehemu wanapo kusudia”
Maneno ya Magreti ayakanihimiza kuongeza kasi yagri hili hadi ikafika hatua nikaanza kuogopa na kuamini kwamba ikitokea bahati mbaya tumepata ajali basi sijui itakuwaje.
Kwa mbali nikaanza kuziona gari hizi zikienda kwa kasi sana, nikazidi kuongeza kasi hadi nikazifika karibu. Gari za mbili za nyuma zikaanza kuzuia nisipite huku nazo zikienda kasi.
 
“Hii mijamaa mijinga kweli kweli”
Nilizungumza huku nikitazama jinsi gari hizi zinavyo tamba barabarani na kuicha gari aliyo panda Osma ikiwa mbele kabisa. Magreti akaanza kutoa bastola zake mbili akazikoki vizuri, akanitazama kisha taratibu akafungua kioo cha upande wake. Akatoa mkono mmoja wa kushoto na kuanza kushambulia gari  hizi zinazo tuzuia.
“Funga kioo”
Nilimuambia Magreti na kumfanya atii nilicho mueleza. Nikapunguza mwendo huku nikitazama kijinjia cha pembeni upande wa kulia wa barabara, nikaanza kuingia kwenye barabara hii ambayo ninaifahamu na inatokea kwa mbele.
“Unakwenda wapi?”
“Tulia”
 
Nikazidi kuongeza mwendo kwenye njia hii ndogo ambayo imetenganishwa na msitu ambao  unatufanya tusizione gari za barabarani wala gari zinazo pita narabarani zisituone.
“Upo tayari?”
“Eheheeee”
Nikaongeza mwendo hadi gari ikaanza kutoa mlio wa tahadhari, tukaingia barabarani na gari nikaanza kuizungusha kwa mfumo wa dura. Gari  hizi za msafara wa Osama Bin Laden zikaanza kutoka barabarani wakihakikisha kwamba wananikwepa mimi kwani kitu walicho kutana nacho ni cha gafla sana. Gari zote zikaendelea kuelekea maporini, nikalisimamisha gari, kizunguzungu tunacho kihisia, sikukipa nafasi ya kunipoteza muda wa kumpoteza Osama Bin Laden. Niachomoa bastola zangu sehemu nilipokuwa nimeziweka.
“Hei upo  poa?”
 
Nilimuuliza Magreti huku nikimtazama tu usoni mwake, hakunijibu nikatamba bado anasikilizia kizunguzungu kwani gari imezunguka zaidi ya mara kumi na tano. Nikafungua mlango na kushuka,  walizni wa Osama wakaanza kushambulia huku wakijitahidi kuhakikisha wanamlinda bosi wao.
Cha kumshukuru Mungu huku nikiwa nina bastola zenye risasi za kutosha huwa sifanyi makosa kabisa ya kuhakikisha kwamba ninawashambulia maadui zangu. Nikaanza kumuangusha mlimzi mmoja baada ya mwengine kwa maana baadhi ya ndio kwanza wanatoka kwenye magari yao ambayo yamebondeka bondeka kwa kugongana wao wenyewe, wengine kwa kugonga miti mikubwa iliyopo pembezoni mwa hii barabara.
Nikafika lilipo gari alipo Osama, nikakuta mlango upo wazi  na ndani hakuna mtu.
“Dany wanakimbilia mbele”
Niliisikia sauti ya Logate masikioni mwangu.
“Mage hakikisha kwamba hushuki kwenye gari, endesha hadi kwenye kona inayo fwata sawa”
“Poa”
Nikaanza kukimbia kuelekea sehemu anapo kimbilia Osama na jeshi na walinzi wake. Nikafanikiwa kuwaona. Wakaanza kunishambulia kwa risasi huku wakijibaza kwenye miti iliyopo mbele. Nikajibanza kwenye mti huku nikisikilizia jinsi wanavyo shambulia.
“Dany nimefika kwenye kona”
“Umeona hicho kijimlima hakikisha  kwamba unakipanda, kwa maana wana bunduku kubwa wameniweka kwenye tageti na kwenye huu mti siwezi hata kushambulia”
“Nimekuelewa mkuu”
Osama na watu wake wakazidi kushambulia kwa fujo. Gafla nikasika vishindo vya watu kuanguka chini. 
 
“Tayari”
Magreti alizungumza na kunifanya nijitokeze kwenye mti huu, nikawaona watu watatu wakiwa wamelala chini.
“Umemua hadi Osama?”
“Hapana, huyu hapa, nimemchoma kile kijisindano”
Magreti akanionyesha sehemua alipo mchoma kisindano. Kwa haraka nikamvua kitambaa kilicho ifunika sura yake na kweli nikakuta sura yake. Nikampiga picha kadhaa na kumtumia Logate.
“Dany ndio yeye”
“Poa”
Kwa haraka nikamnyanyua na kumbeba begani mwangu. Magreti akaanza kuongoza njia hadi sehemu lilipo gari, nikamuingiza siti ya nyuma, tukaingia ndani ya gari. Kitendo cha kuwasha gari tukaona gari karibia sita zikija nyuma yetu kwa kasi sana, huku zikifanya mashambulizi makali sana. Nikawasha gari na kuanza safari ya kuifuta Bagamoyo kwnai siwezi kurudi nyuma kwani gari hizi zinazidi kutukimbia huku zikitushambulia.
 
“Jamani tunashambuliwa tuambieni nini tufanye”
Magretu alizungumza huku akimuweka Osama vizuri kwenye situ huku akiwa amemfunga mkanda wa siti.
“Livna unanisikia?”
“Ninakusikia Dany”
“Ninakuomba unitafutie ramani ya kuelekea katika nyumba ya mama yangu mkoani Tanga?”
“Ile ya Tanga mjini?”
“Hapana ninahitaji ile ya msituni”
“Okay nimekupata dakika moja”
Nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari langu kwani hawa watu wanao tufukuzia ni watu wa Osama ambao wanahitaji kuhakikisha wanamkomboa bosi wao. Tukafanikiwa kufika barabara ya kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha.
“Dany nimeipata nimeituma kwenye screen ya gari hapo umeiona?”
“Ahahaa…….yap yap nimeiona nimeiona”
“Tukutumie msaada?”
“Hapana hawa nitajua jinsi gani ya kushuhulika nao. Ila nikifika kwenye nyumba hiyo nitaomba unitumie msaada”
“Sawa hakisha unakuwa salama mume wangu”
 
“Usijali”
“Vipi niwashambulie?”
“Hapana, hakuna haja hiyo”
“Kwa nini?”
“Tutawaacha njiani mmoja baada ya mwengine, tulia uone”
Nilizungumza huku nikipungaza mwendo wa gari kwani mbele kuna gari mbili kubwa aina ya Scania zinakuja kwa kasi sana. Nikahama upande wangu na kuingia upande wa mgari haya makubwa yanazidi kuja kwa kasi huku dereva wa gari la mbele akiniwashia taa zote kuniashiria nirudi upande wangu.
“Dany unafanyaje jamani?”
Magreti alizungumza kwa sauti iliyo jaa wasiwasi mwingi, sikumjibu kitu chochote zaidi ya kuongeza kasi wa gari huku nikizitazama gari za watu hawa wanao tukimbiza zikinifwata upande huu nilipo huku wakiendelea kunishambulia kwa risasi.
 
AISIIIII……….U KILL ME 191   
                                                                         
Nikazima taa za gari langu huku nikiendelea kuendesha kwa kasi gari, zikiwa zimebaki mita chake kukutana na gari hili kubwa la mizigo, nikawasha taa huku nikirudi katika upande wangu wa gari jambo lililo sababisha gari kadhaa nyuma yetu kugongana uso kwa uso na gari hili kubwa na isitoshe zipo gari mbili zilizo fwatana ni kubwa.
“Waooooooooooooooo”
Magreti alishangilia huku akigeuka nyuma akitazama jinsi gari hizi zinavyo endelea kumabizwa huku gari nyingine zikiacha njia na kuingia kwenye misituni.
“Dany wewe ni genius”
“Eti eheee”
“Yaaaa”
“Siku nyingine usiogope”
Tukiwa hata bado hatujafika mbali, tukaona gari nyingine mbili zikija kwa nyuma yetu kwa kasi ya ajabu.
“Hawa wamesali, wajinga kweli kweli”
“Utawafanyaje?”
“Nawadumbukiza wame wote hawa”
“Utawadumbukiza vipi?”
“Tulia mama”
 
Nikapunguza mwendo kidogo ili kuwangojea hawa jamaa wanao tufwatilia kutukaribia.
“Mbona unapunguza mwendo Dany?”
“Mage unaogopa nini tulia”
Jamaa hawa wakazidi kutusogelea jambo lililo nifanya niwaone vizuri katika kiooo changu cha pembeni. Kila walivyo jaribu kunipita, ninawazuia huku nikihakikisha kwamba hawanipiti, tukaaanza kushuka kwenye mporomoko wa daraja la Wami ammbalo linasifika kwa wembaba wake unao himili magari mkubwa ya kila aina kupita juu yake. 

Jamaa pasipo kutambua ni kitu gani ninacho kiwaza wakazidi kuniandama, kitendo cha kulikaribia daraja, nikafunga breki za gafla huku nikiligeuza gari upande wangu, dereva alite tangulia mbele kwa akili zake fupi akajaribu kunikwepa na mika kwa moja bila hata ya ubishi nikamshuhudia akiingiza gari analo liendesha kwenye mto huu mkubwa sana unao sifika kwa kina kirefu na kuna mamba wengi. Dereva wa pili akafunga breki karibu kabisa na mlango wa upande wangu, nikamtazama kwa muda mwaharabu huyu ambaye anaonekana haifahamu barabara hii. Nikaichomoa bastola yangu sehemu nililipo ichomeka, nikashusha kioo kwa haraka.
 
“Bye”
Nilizungumza na kuanza kufyatua risasi kadhaa zilizo penye kwenye kioo cha mbele cha gari hili na kumpiga dereva wake alite poteza maisha hapo hapo kwani risasi nilizo mpiga ni nyingi wala hazina idadi kamili.
“Nice job”   
“Thanks”
Nikaliweka gari  sawa na kuondoka eneo hili haraka iwezekanavyo na kuacha hili gari likiwa limeziba njia kwa watu wanao toka mkoa wa Dar es Salaam.
 
“Hivi alisema sehemu ya kubadilishia gari rangi ni wapi?”
“Batani hizi”
Magreti alizungumza huku akimya moja ya batani, na pich ya gari hili ikatoka kwenye scean ndogo iliyopo pembeni yangu.
“Niweke rangi gani?”
“Nyeusi”
“Tayari”
Tukazidi kusonga mbele, hadi tukafika katika msitu ambao ndipo nyumba ya mama yangu. Tukaanza kuifwata ramani hii japo ni msitu na njia zake kizogo hazionekani, kirahisi kutokana na kujawa na majani mengi. 
 
“Huku mbona ni msitu tu inaonyesha  haishi mtu yoyote huku”
“Yaa ila kuna nyumba moja tu mbele”
“Ila kuna ogopesha sijawahi kufika eneo kama hili”
“Hii ndio Tanzania, ina maeneo mengi makubwa”
“Mmmm kweli”
Tukafika katika jumba la mama yangu ambalo kusema kweli limezungukwa na majani mengi sana. Nikazichukua bastoka zangu zote mbili na kushuka kwenye gari.
“Kaa na huyo fala sawa”
“Tunashuka wote”
“Mlinde mimi nipo salama”
Magreti akaniangalia, kisha nikafunga mlango wa gari hili. Mwanga wa mbalamwezi unanisaidia kuweza kuona eneo hili lililo izunguka nyumba vizuri sana. Nikaanza kuizunguka nyumba  kuhakikisha kwamba kuna usalama, nilipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha nikazunguka hadi ulipo mlango mkubwa wa kuingilia ndani.
 
Nikauchuguza vizuri kisha taratibu nikaanza kuusukuma na cha kumshukuru Mungu ukaanza kufunguka ikimaanisha kwa kipindi chote haujafungwa. Nikaisogelea swichi iliyopo pembezoni mwa mlango huu na kuwasha ndani.
Mwanga mkali ukaangaza humu ndani, nikaoja jinsi seble hii ilivyo tawaliwa na ukungu wa wadudu wanao  fahamika kama buibui, huku kukiwa na vumbi jingi lililo samba kaa kwenye kila sehemu.
“Nikaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine, nikaingia katika chumba nilicho kuwa ninaikaa mimi, hapa ndipo nikakuta michirizi ya damu nyingi barazani ambayo imekauka. Nikaangalia mandhari ya chumba hichi jinsi yalivyo changuliwa vibaya vibaya.
 
‘Hapa ndipo walipo uwawa’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama mandhari ya hichi chumba. Nikatoka humu na kuingia katika chumba kingine, kisha nikaelekea katika chumba kingine ambacho alikuwa analala mama, sikikuta mabadiliko makubwa zaidi ya vumbi jingi. Nikarudi nje na kumkuta Magreti akinisibiria nje ya gari.
“Kupo salama?”
“Ndio”
Nikafungua mlango wa nyuma ya nikamtoa Osama Bin Laden, nikambeba bageni mwangu na moja kwa moja tukaingia ndani na kumlaza kwenye moja ya sofa.
“Kwa nini usimuue sasa hivi tukarudi zetu kambini”
“Nina mambo mengi ambayo ninahitaji kumuuliza maswali”
“Dany unahisi kwamba hii sehemu ni salama kwa sisi kuendelea kuwepo hadi kupambazuke?”
 
“Ndio ni salama. Logate nina imani kwamba unatuona tulipo?”
“Hapana, hakuna kamera yoyoye ya hapo ndani na hatuwezi kuwaona”
“Eneo la nje je?”
“Eneo la nje tunaona kupitia satelaiti”
“Ulinzi wenu unahitaji kwa muda huu”
“Tupo kwa ajili yenu”
“Sasa hichi kijisindano alicho chomwa, kitachukua muda gani hadi azinduke?”
“Haito mchukua mda kuanzia hivi sasa”
“Poa Livna, unanisikia?”
“Ndio ninakusikia Dany wangu”
“Kazi yangu imekamilika, ninahitaji sasa kuzungumza na huyu mzee mazungumzo yangu sihitaji yasikiwe na mtu yoyote zaidi yangu mimi na yeye”
“Ni mazungumza gani hiyo Dany”
 
“Nitakuambia mara baada ya kumaliza kuzungumza naye, pale atakapo zinduka”
“Mmmmm sawa”
“Una guna nini?”
“Ahaa, ninashangaa ni mazugumzo gani ambayo huhitaji mimi niweze kuyasikia”
“Nitakuambia”
“Kuwa makini na huyo mtu kumbuka kwamba ni gaidi ambaye amefanya matukio mengi sana”
“Alikuwa anaongoza matukio ila yeye hakuwa mtendaji”
“Sawa”
“Mida”
Nikachomoa kinasa sauti nilicho kichomeka sikioni mwangu. Nikamtazama Magreti kwa ishara naye nikamuomba avua kinasa sauti chake.
“Kwa nini?”
Magreti alizungumza kwa sauti ndogo sana ambayo sio rahisi kwa mtu kuweza kuisikia hadi amtazame mdomo wake jinsi unavyo yataja matamshi hayo.
“Vua”
Magreti akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akavua kinasa sauti chake na kunikabidhi, nikatazama tazama hapa sebleni. Nikaona moja ya chupa ya maji ambayo inamaji kiasi nikaichukau na kumwagia nayo Osama usoni mwake, nikadumbukiza hivi vinasa sauti na kuifunga chupa hii.
“Mbona umeniambia unahitaji kuvua hivi vinasa sauti”
“Nina maana yangu, iunaweza kwenda huko nje kukaa peke yako nikiwa ninamuhoji huyu mjinga?”
“Hapana”
“Sasa hiyo ndio maana yangu”
Osama taratibu akaanza kufumbua macho yake huku akinitazmaa usoni mwangu. Kwa nguvu nikamnyanyua na kumkalisha kitano, nikachomoa bastola yangu nilicho ichomeka vizuri kiuoni mwangu. Osama akazungumza maneno ambayo siyaelewi kabisa.
“Anasema wewe ni nani?”
Magreti alizungumza huku akimtazama Osama.
“Mimi ni Dany”
Magret akayazungumza maneno hayo kwa lugha ya kiarabu. Osama akaonekana kustuka sana.
 
“Usistuke babaa, ndio hivyo umeingia mikononi mwangu, nijibu maswali yangu kama vile ninavyo hitaji, la sivyo ninaondoka na kichwa chako”
Magreti akaendelea kutafsiri kile nilicho kizungumza na kukipeleka katika lugha ya kiarabu. Osama hakujibu kitu chochote zaidi ya kunitolea mimacho yake.
“Natambua kwamba ulitangazwa kwamba umeuwawa na Wamarekani na dunia nzima ndivyo inavyo jua hilo, imekuwaje leo umeamua kuungana nao na kunisaliti ikiwa nilikukuomboa kwenye baadhi ya vitu ikiwa ni kushambuliwa wewe na kundi lako”
 
Baada ya Magreti kuyazungumza niliyo yazungumza Osama naye akaanza kuzungumza huku akiwa amejawa na upole wa hali ja juu.
“Anasema kwamba, Wamarekani na K2 walimuhakikishia ulinzi katika nchi hizi mbili, Tanania na Marekani na walipanga kukutafuta wewe na wakitumia mtego wa kukutana nyote waili”
“Haahaaa sasa wewe unajiita gaidi unategemeaje msaada kutoka kwa watu ambao hawaeleweki, watu walio kuulia ndugu zako, rafiki zako na jamaa zako, inakuwaje leo unaungana nao. Je ni kukosa uwezo wa kijeshi au nini?”
“Anasema jeshi lake liemedhohofika na wengi walipo kwenye kundi lake la Al-quida ni watoto wadogo na vijana ndio maana alijaribu kuungana nawe ili mradi aweze kupata nafasi ya kuishambulia Marekani”
Nikamtazama Osama kuanzia juu hadi chini, nikamshika mkono wake wa kulia na kumnnyanyua kwa nguvu, nikaanza kuelekea naye kwenye chumba  cha ilipo uliwa familia yangu.
Sote tukaingia ndani, nikamsukumia Osama chini, kutokana na uzee alio nao hakuweza kunishinda kunguvu.
 
“Hii ni damu, hapa alikufa mke wangu, mwanangu, mdogo wangu na mama yangu. Unahisi hii damu inaweza kunifanya leo na kesho kutwa niweze kuungana na maadui zangu eheeee?”
Nilizumgumza kwa ukali sana huku nikimtazam Osama. Magreti akamatafsiria kile nilicho mueleza, Osama hakujibu kitu chochote.
“Domo lako ndio limekuponza, nilikuwa sina mpango kabisa na wewe wa kukutafuta. Nilihitaji kuonana na wewe kwa wema kabisa, ila sijui ulinichukuliaje?”
Nilizidi kuzungumza kwa hasira.
“Sasa ninakwenda kuishanga dunia na kukuonyesha mbele ya vyombo vya habari kwamba upo hai, mbili nitakufanya kama nilivyo mfanya raisi wa Marekani, ili nizidi kuandika historia kwamba mimi ndio mtu niliye muondosha Osama duniani”
 
Magreti akaka kimya huku huku akinitazama usoni mwangu.
“Muambie unasubiri nini?”
“Dany hayo maneno ni makali sana”
“Hembu niachie ujinga na wewe, ni makali yanaumiza au. Muambie kile niliocho kuambia mimi”
Magreti hakuwa na jinsi akaanza kuzungumza kile nilicho mueleza. Osama taratibu akaanza kupiga magoti chini, na kuanza kuomba msamaha huku machozi yakimlenga lenga. Japo ni mtu aliye sifika kwa roho mbaya duniani na kufanya mambo mengi mabaya duniani, ila kusema kweli ameingia  kwenye kumi na nane zangu na amekutana na mtu ambaye tayari nimesha jipatia nafasi ya kuitingisha dunia kwa kile ninacho kifanya.
 
“Dany anaomba msamehe kwa maana anasema kwamba hilo swala la kuunganishwa na Wamarekani pamoja na K2 halikuwa wazo lake, ila ni washauri wake ndio walimpelekea katika katika muungano huo”
Nikaka kimya huku nikimtazama mzee huyu jinsi anavyo niomba msamaha akionekana amejawa na majuto mengi.
‘Isije akawa anatuigizia huyu?’
Niliwaza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama usoni mwake.
“Dany nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Unaonaje tukamtumia huyu kutukutanisha na K2 ili kama ni kazi tuimalize mara moja na kuondoka zetu huku tukijua kwamba kila jambo tumelimaliza.
 
“Tukio la kutekwa kwa huyu mjinga lazima litakuwa linafwatiliwa”
“Sasa ipi ni njia ya kumpata K2 kama si kumtumia Osama”
“Unahisi K2 atakuwa mpambavu kumsikiliza huyu mjinga?”
“Dany hii ni hii ni gemu kuna kushinda na kushinda na kushindwa. Tumtumie Osma kama ufunguo wa kumfungua K2 uliye shindwa kukutana naye kwa miaka sasa na umeshindwa kulipiza kisasi chako. Tufanya hivyo kisha utanipatia majibu”
 
Maneno ya Magreti yakaanza kiniingia akilini mwangu, taratibu. Kwa maana endapo Osama atahitji kuonana na K2 na mimi nipo katika sura ya bandia ni ngumu sana kwa K2 kunitambua na itakuwa ndio nafasi yangu ya mwisho kuhakikisha kwamba ninamtia mikononi na kumuondoa dunia na nitakuwa nimemaliza asilimia kadhaa ya kazi yangu.
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa Dany amekubaliana na wazo alilo litoa Magret je mpango wao utafanikiwa? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )