Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 16, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 192 na 193 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
“Dany hii ni hii ni gemu kuna kushinda na kushinda na kushindwa. Tumtumie Osma kama ufungou wa kumfungua K2 uliye shindwa kukutana naye kwa miaka sasa na umeshindwa kulipiza kisasi chako. Tufanye hivyo kisha utanipatia majibu”
Maneno ya Magreti yakaanza kiniingia akilini mwangu, taratibu. Kwa maana endapo Osama atahitji kuonana na K2 na mimi nipo katika sura ya bandia ni ngumu sana kwa K2 kunitambu na itakuwa ndio nafasi yangu ya mwisho kuhakikisha kwamba ninamtia mikononi na kumuondoa dunia na nitakuwa nimemaliza asilimia kadhaa ya kazi yangu.
   
ENDELEA
“Poa nimekuelewa”   
“Ila unaoenekana kama hujaridhiana na mimi?”
“Hapana nimeridhika, ila fikiria na uupange vizuri huo mpango ulio nieleza kw amaana sihitaji kufeli tena kwenye maisha yangu”
 
“Nimekuelewa”
“Hakikisha kwamba unamdhibiti”
Baada ya kuzungumza maneno hayo nikatoka chumbani humu na kuwaacha wawili, nikatoka nje na kuzunguka upande mwingine wa nyumba. Nikafungua geti kubwa lililopo na kuingia katika ukumbia ambao kuna vitu vingi ambavyo mama alivihifadhi humu ndani. Nikawasha taa, na nikabaki nikiendelea kutazama hivi vitu vilivyomo humu ndani huku kukiwa na magari kadhaa yaliyo funikwa na maturubai. Kila ninapo tazama vitu hivi vya umu ndani ni kama ninamuona mama yangu jinsi siku ya kwanza nilivyo kuwa akinielekeza baadhi ya vitu. Simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kupokea.
“Upo wapi Dany ninakutafuta sikuoni?”   
“Zunguka huku nyuma”
“Wapi?”
“Upande huu wa kulia”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni mwangu. Magreti akaingia humu ndani na kuonekana kushangaa snaa kwa kile anacho kiona.
 
“Umemuweka wapi?”
“Nimemuweka mule ndani?”
“Umemfunga na kitu chochote?”
“Ndio, nimekuta kamba ya manila, nimemfunga na nimehakikisha kwamba hatoki”
“Ila kumbuka huyo sio kuku ni gaidi, tena sio gaidi mchwara ni gaidi mkubwa”
“Hawezi kutoka sehemu nilipo mfunga”
“Sawa”
Nikafungua kabati moja ambalo linahifadhia silaha.
“Mmmmmm hii nyumba yenu imekamilika sana”
“Ndio ipo vizuri”
Nikawasha computer iliyopo humu ndani. Nikakuta inahitaji kuiingiza neno la siri ili iweze kufunguka, nikajaribu kukumbuka ni namba zipi za siri ambazo mama alikuwa mama alikuwa akizitumia, nikajaribu kuingiza jila lake ila haikufunguka, nikaingiza jina langu kwa bahati nzuri ikafunguka. 
 
“Hii computer alikuwa anaitumia mama yangu”
Nilizungumza huku nikifungua faili moja linalo onyesha video zilizo rekodiwa na  kamera zilizipo eneo la nje ya hii nyumba. Nikamuona Mariam akifika katika hili eneo na kupokelewa vizuri na mama.
“Huyu si Mariam?”
“Ndio unamfahamu?”
“Ndio alikuwa ni miongoni mwa mwezetu.”
“Yeye alihusika katika mauaji ya familia yangu”
“Weeeeeeee!!!”
“Ndio”
 
“Sijui yupo wapi?”
“Nimemsamehe kwa maana yeye aliagizwa kufanya hivyo na K2”
Nilizungumz akwa sauti ya upole huku nikitazama picha ya Mariam, niliyo inatisha kwenye hii computer.
“Pole sana Dady”
Simu yangu ikaingia ujumbe mfupi meseji, nikaitoa mfukoni mwangu na kufungua ujumbe huu.
‘YEMI AMAPETIKANA’
Baada ya kuusoma ujumbe huu, kwa haraka nikaipiga hii namba, ikaita kwa muda kisha ikapolekewa na Livna.
“Ni kweli amepatikana?”
“Ndio amepatikana niamini mpenzi wangu, ngoja nielekee chumba cha daktari uzungumze naye”
“Hembu fanya hivyo”
Baada ya dakika mbili, nikaisikia sauti ya Yemi kwenye simu hii.
 
“Dany”   
“Yemi upo hai?”
“Ndio nipo hai mpenzi wangu”
Yemi alizungumza huku akilia.
“Upo salama sasa, mpe simu Livna”
“Eheee”
“Sasa ninahitaji kuimaliza kazi  iliyo nilete huku, Osama nahitaji kumtumia Osama kunikutanisha na K2”
“Dany huo sio mpango ulio kupelekea huko mume wangu, utajiingiza matatizoni”
“Ninaelewa mke wangu, ila itanibidi kufanya hivi nahitaji nikurudi huko nirudi mazima tuishi nikulee”
 
“Dany utaniua kwa presha mwenzio”
“Nina sura ya bandia hakuna kitakacho haribiki, tutaendelea kuwasiliana”
“Sawa, muvae hivyo vipaza sauti”
“Usijali”
“Poa kuwa makini”
“Sawa mke wangu”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni mwangu, nikasogelea meza yenye computer kubwa, nikaiwasha na kukuta ikinihitaji kuingiza namba za siri.
“Inahitaj namba za siri”
Nilizungumza huku nikimtazama Magreti anaye tazama tazama baadhi ya vitu vilivyomo humu ndani.
“Unazifahamu hizo namba za siri?”
“Sikukumbuki kwa kweli  kwa maana mtumiaji alikuwa ni mama”
Nikaanza kujaribu majina tofauti tofauti ya wana familia wangu, ila yote yakakataa.
 
“Majina yote yamekataa”
“Jina lako umelikumbuka?”
“Eheee ngoja niingize jina langu”
Nikaanza kuingiza jina langu kwa herufi ndogo, cha kumshukuru Mungu computer ikafunguka. Nikaanza kutazama tazama mafaili  pamoja na mfumo mzima wa kamera ambazo zimefungwa mbali na eneo la kuingilia katika eneo la karibu la hapa nyumbani. Nikaanza kupitia matukio ya nyuma yaliyo rekodiwa na kamera zote, nikakarudi mika mitatu nyuma na kuona tukio la Mariam alivyo karibishwa nyumba hapa na mama. Sikuweza kuona ndani kwa mana ahakuna kamera yoyote kwa ndani, nikapeleka mbele na kumuona Mariam akitoka humu ndani peke yake. 
 
“Hembu rudisha nyuma huyu dada kama ninamfahamu”
Magreti alizungumza mara baada ya kuja hapa nilipo na kutazama kitu ninacho kitazama. Nikafanya kama anavyo hitaji.
 
“Huyu si Mariam?”
“Ndio ni Mariam ndio mtu aliye niulia familia yangu”
“Weeee?”
“Ndio ila alipewa kazi hiyo kwa shinikizo la kutekwa kwa mama yake”
“Masikini weee, sasa umemsamehe?”
“Ndio nimemsamehe, sikuwa na haja ya kufanya hivyo ikiwa maisha yangu ya kujitegemea nilianzia kwao”
“Ahaaa, hiyo ndio sababu ya kumsamehe?”
“Kuna sababu nyingine nyingi ambazo sihitaji kuzizungumza kwa sasa ila sina sababu ya kuunyanyua mkono wangu na kumtafuta Mariam ikiwa kuna mambo mengi aliweza kunisaidia.”
“Ahaaa sawa”
Macho yangu yakatazama kifuani mwa Magreti na kutatazama maziwa yake jinsi yalivyo nona na yanatamanisha kwa kweli.
 
“Unatazama nini kifuani mwangu?”
“Kwani dhambi kukutazama?”
“Hapana sio dhambi ila umenikodolea macho hado ninaogopa”
“Una maziwa mazuri”
“Asante”
Magret alizungumza huku akiyarudisha maziwa yake ndani, taratibu nikasimama mbele yake huku nikimtazama machoni mwake.
“Dany ninakuheshimu wewe ni mume wa mkuu wangu kwa hiyo siwezi kumsaliti”
“Maneno hayo yametokewa wapi ikiwa nimesimama tu mbele yako na sijakufanya kitu chochote”
“Dady mancho yako yanaonyesh dika kwamab umevutiwa na mimi”
“Yaaa nimesimama kama mume boksi kwa masaa mengi mbele za watu, sasa ninahitaji kuwa mume wa kweli”
“No Dany huwezi ku……”
Nikamshika Magreti kiuno chake na kumvutia karibu yangu na kusababisha miguno ya vifua vyetu.
“Da….n…y una, una…..”
“Nina nini?”
Nilizugumza huku nikianza kuyatomasa maziwa yake, Magreti akayafumba macho yake akionekana kuogopa sana kwa kihi kitu ninacho kifanya kwenye mwili wake.
“Dany utaniletea matatizo na bosi wangu, tafadhali ninakuomba niachieee”
 
Magreti alizungumza kw amsisitizo huku akijitoa mikononi mwangu kwa nguvu, nikamuachi na akasimama mbali kidogo na sehemu nilipo huku akihema kwa woga. 

Nikatabasamu kwa muda kisha nikatoka humu ndani pasipo kumsemesha Magreti kitu chochote, nikarudi sebleni, nikatazama eneo zima na hakuna mabadiliko yoyote, nikapandisha hadi kwenye chumba ambacho Osama yupo, nikausukuma mlango wa chumba hichi taratibu huku bastola yangu nikiwa nimeishika vizuri mkononi mwangu. Nikamkuta akiwa amekaa kwenye moja ya kiti cha humu chumbani huku akiwa amefungwa kamba mwili mzima. Nikatao simu yangu mfukoni na kumpiga picha kadhaa, kisha nikamtumia Logate kwenye simu yake ya mkononi. Hazikupita dakika hata mbili Logate akanipigia.
 
“Nimezipata picha unahitaji nizifanyaje?”
“Zitunze, hakikisha kwamba unazirusha kwa niaba yangu kwenye mtandao”
“Unataka nizurushe ukiwa bado upo nje ya ngome hii?”
“Nitakuambia”
“Sawa, ila kusema  kwelis sinto weza kuzirusha ukiwa mbali na hapa”
“Nitakujulisha, ila kuna video ambayo ninahitaji mtumie K2”
“Video gani?”
“Au basi nitajua nini cha kufanya”
 
“Sawa”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni mwangu, nikamtazama mzee huyu ambaye kwa kukadiria miaka yake kwa sasa inaweza kufika sabini na kitu hivi. Nikatoka humu ndani na kurudi zangu sebleni, nikamkuta Magreti akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia humu sebleni huku ukiwa umefungwa kwa ndani. Sikumsemesha kitu chochote zaidi ya kuelekea jikoni, nikafungua friji kubwa na kukuta soda nyingi pamoja na matunda yaliyo pangiliwa vizuri, soda hizi zimeganda kwa ubaridi mkali ambao upo ndani ya friji hili na isitoshe limekaa mika mingi likiwa linafanya kazi pasipo kufunguliwa.
“Una njaa?”
Niliisikia sauti ya Magreti nyuma yangu.
“Sijui”
Nilizungumza huku nikichukua chupa moja ya soda pamoja na tunda, nikachukua jagi na kukinga maji kwenye bomba, kisha nikadumbukiza vitu hivi ili viyayuke.
 
“Dany?”
“Nini?”
Nilimtazama Magreti kwa macho makali sana hadi akaonekana kuogopa.
“Samahani kama nimekuudhi”
“Hujaniudhi”
Nikasikia mlio wa chupa hii ya cocacola inavyo vunjika ndani ya maji haya, nikaitazama kwa muda na kukuta imekatika vipande vipande.
“Ungeiacha ipigwe na hewa kidogo ndio ungeiingiza kwenye maji”
“Shukrani”
Majibu yangu ya ufupi fupi si kwamba nimekasirika, ila ninamtega Magreti ambaye kusema kweli nikiwa kama mwanaume ambaye sina kasoro ya aina yoyote kwenye mwili wangu, basi ni haki yangu na mimi kuweza kutamani. Nikalingiza mkono wangu wa kulia ndani ya jagi hili kwa bahati mbaya kipande kidogo cha chupa kikanichana katika kidole changu cha mwisho.
 
“Fuc****”
Nilizungumza kwa hasira hadi Magreti akastuka, alipo niona kidole changu kina vuja damu kwa haraka akanikumbilia na kunishika mkono huu.
“Dany umefanya nini jamani?”
“Niachie”
Nilizungumza kwa sauti nzinto huku nikifungua moja ya kabati lilipo humu jikoni, nikatoa kibokisi cha huduma ya kwanza.
 
“Dady jamani, naomba nikusaidie”
“Ili  iweje?”
“Dady kwani kukasaidia kwangu kunahusiana na nini na mapenzi jamani, kwa nini unakuwa hivyo jamani, unahisi kwamba sina hisia na wewe, unasi kwamba sijisikii maumivu ya majibu yako nasikia ila umewahiwa, sina haki ya kuwa na wewe, sina haki ya kuwa na mwanaume mwengine. Mimi ni bikra il……”
Magreti alizungumza kwa ukali huku machozi yakimwagika usoni mwake. Kwa haraka nikamsogela na kumgandamiza ukutani, nikaanza kumnyonya midomo yake jambo lililo mfanya Magreti kuipitisha mikono yake kwa haraka kwenye shingo yangu huku akiyafumba macho yake kwa raha ya kupata denda langu.
 
“Kidole”
Magreti alizungumza kwa sauti laini iliyo jaa mahaba, huku macho yakiwa yamemlegea sana.
“Achana nacho”
“Noo Dany angalia kina mwanga damu”
Nikakitazama kidole changu na kweli kina mwaga damu nyingi. Magreti akakishika na kukuiingiza mdomoni mwake na kuanza kuinyonya damu yangu.
Tukaseoge hadi sehemu nilipo kiweka kiboksi cha vifaa vya huduma ya kwanza. Akatoa dawa ya maji na kuanza kunisafisha kidonda changu, japo dawa hii inanipa maumivu makali ila siyatilii maanani kwani maumivu ninayo yatilia maanani ni ya jooo wangu ambaye amesimama kiasi kwamba anatamani hata kuchana suruali yangu. Magreti akanifunga kidonda hichi kwa kutumia plasta.
“Hapo kitakaa sawa”
“Shukrani, ni kwa nini umenyonya damu yangu”
“Ni kiapo nilicho kiweka, nipo tayari damu yangu imwagike ila nisikupoteze wewe”
“Kweli?”
“Ndio Dady, sijawahi kupenda wala kuvutiwa na mwanaume ila wewe umenipa kitu cha tofauti, ninakuomba uwe na mimi”
“Usijali”
Nilizungumza huku nikiuingiza mkono wangu kwenye mpasuo wa gauni la Magreti nikaanza kutaminya minya maka yake ambayo kusema kweli yanabonyea mithili yam to mlaini.
 
“D….aa..aa”
“Yeah”
“Nakupenda”
Magreti akaanza kugombana na mkanda wangu wa suruali hii niliyo vaa huku akijitajid kuufungua, akafanikiwa kuufungua.
 

nikatamani kuzungumza kitu ila gafla nikasikia kishindo kizito kilichotufanya tustukea na kutazamana usoni na hakuna kati yetu anaye jua ni kitu gani kimetokea hadi kusikika kwa kishindo hicho kizito. 

AISIIIII……….U KILL ME 193


Kwa haraka tukaaachiana na kunza kuziweka nguo zetu sawa. Nikachomoa bastola yangu moja na nikiwa wa kanza kutoka humu chumbani humu. Sikuamini macho yangu, kwani eneo zima la sebleni limechanguka huku nusu ukuta ukiwa umetoboka.
“Ohoooo my God”
Magreti alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Shiiiiii”
Kwa kupitia shumo hili kubwa tukaona wanajeshi wawili wakikatiza kwa haraka wakionekana kwamba wanawahi kitu falani. 
 
“Shitiiii OSAMA”
Nilizungumza humu nikikimbilia katika chumba ambacho tumemuacha Osama Bin Laden. Kile nilicho kiwaza ndicho hichi ninacho kiona kwani sikuweza kumuona Osama wala kiti chake tulicho mfunga ikimanisha kwamba wanajeshi hawa wamembeba Osama kama vile walivyo mkuta. Nikakimbilia dirishani na kujibanza, nikachungulia nje, nikakutana na pigo jengine, kwani ninamshuhudia wanajeshi hawa wenye mavazi mavazi ya Kimarekani wakiwa wamemmbeba Magreti aliye sinnzia juu juu, wakamuingiza katika moja ya gari walilo kuja nalo kisha wakaondoka kwa kasi sana.
 
*Fuc*****”
Nilizungumza huku nikiwa nimeyang’ata meno yangu kwani shambulizi hili wamelifanya katika muda mfupi sana, nikatoka chumbani humu kwa kasi sana, nikachungulia nje, nikaziona gari hizi zikitokomea, nikakimbilia hadi gari lilipo, nikajikuta nikizidi kupatwa na hasira mara baada ya kuona mataoiri yote yakiwa yameng’olewa yote. Nikatoa simu yangu mfukoni cha kushangaza zaidi nayo haina signal na mtandao ninao utumia umeandika emergency. Nikakimbilia kwenye chumba alichokuwa anakitumia mama, nikakimbilia kwenye computer, nikatazama wanajeshi hawa wapo wangapi, nikaona gari sita zilizo ongozana zikiondoka kwa kasi katika eneo hili.
 
“Wapi wapi?”
Nilizungumza huku nikitafuta sehemu ambayo mama alikuwa anaitumia katika kuongoza silaha ambazo amezifunga katika eneo zima la msitu unao zunguka hii nyumba. Sikuweza kutambua ni sehemu gani, kwa haraka nikaanza kufunua gari moja baada ya jengine, nikaona gari moja aina ya Rangerover Sport, niakimbilia kwenye kabati la kihifadhia fungua, nikatazama kwa haraka nikaiona funguo yake, kabla sijarudi kwenye gari nikafungua kabati la kuhifadhia silana nikachukua magazine za kutosha na kurudi kwenye gari nikafungua mlango na kuingia, nikawasha gari hili, cha kumshukuru Mungu lina mafuta ya kutosha, nikatoka ndani humu kwa kasi kubwa, nikaanza kufukuzia gari hizi zilipo elekea kwani  kazi niliyo ifanya kwa kumteka Osama na kumleta eneo hili ni sawa na bure kabisa. Uzuri wa hizi gari zina mwendo wa kasi sana na zipo juu, hata huku kwenye barabra ambayo haina lami ila linahimili mashimo mashimo yaliyopo katika hii barabara.
 
Kwa mbali nikaanza kuona gari hizi za jeshi zinavyo jitahidi ktoka katika msitu huu, nikatao simu yangu mfukoni na bado tataizo la kutokuwepo kwa mtando linaendelea, nikazidi kusonga mbele huku huku nikiandaa bastola yangu hukuakikisha kwamba ninaweza kuwashambulia. 

Nikafunga breki za gafla na kutazama mgawannyiko wa barabara hizi tatu zilizopo mbele yangu huku ramani inayo onekana kwenye screen ndogo ya gari langu inaonyesha barabara ya kushoto kwangu, inaaonyesha ni fupi na inaweza kuwazungukia wanajeshi hawa, sikuw ana hata muda wa kupoteza zaidi ya kuifwatisha njia hii huku nikizidi kujitahidi kuogeza mwendo kasi wa gari langu kuhakikisha kwamba ninatokea mbele yao. 

Ikanichukau dakika kumi kufika katika njia ambayo wao wanatarajia kutokea, nikalisimamisha gari hili katikati ya barabara, nichomoa bastola zangu zote mbili na kushuka, nikasimama kwenye upande wa pili ambao haya wakitokea sio rahisi kwa wao kuniona. 

Hazikupita hata dakika tano gari hizi za jeshi, zikafika eneo hili na kuwafanya wanajeshu hawa kusimamisha magari yao. Kwa haraka niikaanza kuwashambulia wale wote wambao wametoka nje ya magari yao. Mashambulizi yakaanza kutawala katuka eneo hili, humu mimi nikiwa peke yangu na wanajeshi hawa wakiwa ni wengi, ila akili ninayo itumia inanifanya niweze kuwapunguza kila kadri mudu unavyo zidi kwenda.
 
Gari langu wakazidi kulishambulia sana kwani ndio gao yangu niliyo jificha, moshi mwingi ukaanza kutawala angani ikiashiria kwamba gari hili sekunde yoyote litalipuka, kwa haraka nikaanza kukimbilia kwenye moja ya mti japo ni hatari sana kwangu ila sina jinsi ya kufanya, sikufikisha hata hatua tano nikajukuta nikirushwa hewani kutokana na mlipuko mkubwa wa gari langu.  
 
Nikatamani kusimama juu ila nikajikuta nikizungukwa na wanajeshi zaidi ya wanne walio ninyooshea mitutu yao ya silaha. Wakaniamrisha kusimama juu, huku bastola zangu wakinipokonya, wakazidi kuongezeka katika kunizunguka kwa maana bado wana hasira kali sana na mimi.
“Tumuue”
Mmoja alizungumza kwa lugha ya kingereza ninayo ielewa vizuri.
“Hapana tunatakiwa kumfikisha kwa raisi K2, kwa manaa huyu mtu ni hatari sana”
“Mkuu ametuulia wezetu kule, kwa nini tumuache?”
“John nimekuambia kwamba hii sio ombi ni amri”
Mzee huyu wa kimarekani alizungumza kwa ukali huku akimtazama kijana huyu anaye onekana kujawa na uchungu mkubwa na anahasira na mimi.
 
“Mpelekeni kwenye gari”
Mkuuw wao alizungumza, nikashikwa mabega yangu na wanajeshi wawili, nikafungwa pingu kwa nyuma cha kumshukuru Mungu ambacho kinawafanya wasiniue kwa haraka ni kutokana na na sura yangu ya bandia ambayo sio rahisi kwa mtu kuweza kunigundua kwa haraka.
“Hei”
Ilisikika sauti ya msichana ikitokea kwenye moja ya kichaka, ikawabidi wanajeshi wote kuzielekezea bunduki zao kwenye kichaka hicho. Tukaona mkono wa msichana ukinyooshwa kwa juu. Akanyanyuka msichana aliye valia suruali nyeusi pamoja tisheiti nyeusi, chini amevalia buti aina za amerikani boot.
 
“Musiniusee jamani”
Msichana huyu  alizungunza kwa lugha ya kingereza huku akiendelea kutusogelea eneo hili.
“Huyu ku** naye ametokea wapi?”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akiwa amejawa na hasira kali sana kwani anaona kama anapotewa muda.
“Hei kaka mimi sio ku**”
“ILa?”
“Unahitaji nini malaya wewe?”
Mwanajeshi mwengine alizungumza kwa hasira huku  akimtazama msichana huyu.
“Nihamuhitaji huyo muliye mshikilia”
“Hahaaaa”
Binti huyu akendelea kunyoosha mikono yake juu akionekana kwamba hana silaha yoyote, kitu ambacho kunanishangaz ni ujasiri wa msichana huyu mwenye sura ya kirembo sana.
 
“Shikeni naye”
Mkuu wa hawa wanajeshi alizungumza huku akiwaruhusu wanajeshi wake kumsogelea huyu msichana, wanajeshi wawili walio msogelea msichana huyu tulistukia wakianguka chini, sote macho yakazidi kututoka baada ya kumuona msichan huyu akiwa ameshika miooyo ya wanajeshi hawa ambayo sijui hata amewaua vipi.
‘Ohoo MUNGU wangu’
Nilijikuta nikimkumbuka Mungu kwani, ninacho kiona ni kitu ambacho kinaogopesha na kinashangaza kwa maisha ya kawaida ya kibinadamu. Wanajeshi wa marekani wakaanza kumshambulia msichana huyu aliye anza kukimbilia kwenye miti iliyopo humu misitu.
 
Kama ilivyo kawaida, yao kwamba hawahitaji kishindwa na kitu wakanza kumkimbiza msichan huyu na kuniacha hapa na mwanajeshi mmoja anaye shangaa wezake walio nyofolewa miili.
Sikuhitaji kuwa mzembe kwa haraka nikaanza kupelekea mateke mazito yaliyo mfanya mwanajeshi huyu  kuanguka chini huku akiwa emaichia bunduki aliyo ishika.
Nikafanikiwa kumdhibiti mwanajeshi huyu na akazimia kutokana na mapigo mazito niliyo mpoa, nikaanza kuchungulia gari moja baada ya jengine, nikafanikiwa kumuona Osama kwenye moja ya gari akiwa amelala. Nikalifwata gari jengine na kumkuta Magreti akijitahidi kunyanyuka, nikageuka na kufungua kitasa hichi cha mlango kwani nikono yangu imefungwa pingu kwa nyuma. Mlango ukafungua na kumkuta Magreti akifumbua macho yake.
“Dany”
“Heii, heiii amka”
“Kuna nini kinacho endelea?”
 
“Shuka kwenye gari kwanza unifungua hii pingu”
Magreti akajikongoja hivyo hivyo na kushuka kwenye gari huku akionekana kwamba alichomwa sindano ya usingizi iliyo mfanya kulala na kulegea kabisa mwili wake.
“Eheeee hawa nao imekuwaje?”
“Chukua funguo ya pingu hapo unifungue”
Magreti akafanya kile nilicho muelekeza kwa haraka akanifungua pingu, nikaokoya moja ya bunduki za wanajehsi hawa, nikachomoa magazine yake na kukuta ina risasi za kutosha.
“Mungu wangu, hawa imekuwaje?”
Magreti alizungumza huku akiwatazama wanajeshi hawa walio chomolewa mioyo yao.
“Kuna msaada nimepata kutoka kwa msichana mmoja ambaye sifahamu ametokea wapi?”
“Ndio  amewachomoa mioyo yao?”
 
“Yaaa na wanajeshi wote wamikimbilia huko msituni kumkimbiza masichana huyo”
“Mmmmmm”
Nikasikia milio ya risasi nyuma yangu, nikageuka kwa haraka na kumkuta Magreti akiwa ameshika bastola moja huku amemuelekezea manajeshi niliye mzimisha dakika kadhaa zilizo pita.
“Alitakak kukushambulia”
“Asante”
Nikafungua gari alilopo Osama, bado amelala hajitambua, tukamkagua na kumuona hana jeraha lolote mwilin mwake.
“Mfunge pingu”
“Poa”
Magreti akachukua  pingu ambayo nilikuwa nimefungwa mimi akamfunga Osma Bin Laden mikononi mwake.
“Tuondoke eneo hili kabla hawajarudi”
Nilizungumza huku nikiingia kwenye gari hili, Magreti naye akaingiana kukaa siti ya nyuma alipo Osma, nikarudisha gari hili nyuma kidogo, nikakunja kona na kuanza kuondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi sana.
 
“Wamejuaje sisi tupo huku?”
“Hata mimi ninashangaa cha kumshukuru Mungu binto huyo ametokea”
“Ila Dany ngoja, hivi huyo msichana amewezaje kuwachomoa mioyo wanajeshi wale”
Gafla nikajikuta nikifunga breki za gari hili mara baada ya kumuona msichana huyu amesimama mbele ya barabara na kuninyooshe amkono mmoja ambao unavuja damu kwenye kiganja chake.
“Mungu wangu, msichana mwenyewe ndio huyo”
“Mbona anaonekana wa kawaida sana”
“Huo ukawaida ndio uliwaponza wale wanajeshi walio chomolewa mioyo”
Kwa ishara msichana hoyo akaniomba nishuke kwenye gari, nikashusha pumzi nyingi sana kwa mana kitu ambacho nimeweza kukigundua kwa msichana huyu kwamba sio mtu wa kawaidani zile risasi ambazo alikuwa anashambuliwa ila aliweza kutokomea msitini pasipo kuanguka wala kuonyesha dalili kama kuna silaha ambayo imeingia mwilini mwake.
 
“Dany usishuke bwana”
“Tulia huyu ndio aliye nisaidia, ninahitaji kumjua”
“Utamjuaje wakati mwenyewe umemuona katika mazingira ya kutatanisha”
“Tulia”
Nikafungua mlango huku nikishuka nikiwa na bunduki yangu mkononi ili likijitokeza la kujitokeza nisife kizembe kama wale wanajeshi wawili na wengine walio  salia wala sifahamu ni kitu gani ambacho kimewapata huko walipo.
“Usiniogope Dady…..ooohhh samahani kwa kukuita jina lako”
Msichana huyu alizungumza hukua kishusha mikono yake chini na kuonekana akiwa na furaha sana kuonana na mimi.
“Wewe ni nani?”
 
“Ahahaa…..mama aliniambia kwamba wewe ndio unipatie jina. Nilikuwa kwenye huu msitu nikilinda makazi ya hapa kwa maana hapa ndipo kwenye na hapa ndipo kwenye asili ya baba yangu”
“Baba yako yupi?”
Nilizungumza huku nikimdadisi sana huyu msichana.
“Wewe”
“Mimi?”
“Ndio, wewe ni baba yangu. Mama yangu ni OLVIA HITLER”
Nikapatwa na kigugumizi nikashindwa kabisa kumjibu msichana huyu ambaye ninakumbuka nilizaa na mama yake ambaye ni jini miaka mingi ya nyuma na alisha wahi kuniahidi kwamba ipo siku mwanangu ninaye mpatia atakuja kunisaidia na hichi ndicho kilicho tokea kwa siku ya leo, ahadi ambayo hata akilini mwangu sikuwahi  kuifikiria kwamba inaweza kuja kutokea ila leo imetimia.
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa DANY kwa mara ya kwanza amekutana na mwanaye aliye zaa na Olvia Hitler je ni nini kitatokea? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )