Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 24, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 200- MWISHO )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
     
Ndani ya muda machache nikaoiona sura ya K2 kwenye Tv ya mbele yangu, uso wake baada ya kuniona mimi akastuka sana, wasiwasi mwingi ukamjaa, kigugumizi kikampata kwani ninaona jinsi kinywa chake kinavyo jaribu kuzungumza neno ila kinashindwa.
 
“K2 baada ya Marekani wewe ndio unafwata. Jiandae”
Nilizungumza kwa sauti nzito sana ambayo tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuitoa kinywani mwangu. Baada ya kuzungumza maneno hayo nikaipiga ngumi tv hii na ikapasuka pasukua, nikiashiria kwamba ni muda wa kwenda kuonana na K2 uso kwa uso.

ENDELEA
Nikawageukia Logate na Magret wakabaki wakinitazama, nikatazama chini maiti ya Ester na wasichana wengine. Kisha nikaanza kutoka humu ndani pasipo kuzungumza kitu chochote na kuwafanya wanifwate kwa nyuma. Wakaokota silaha za wasichana wezao ambao wameuwawa, kila mmoja akaokota silaha yake kwa muda wake. Tukaanza kupambana na wanajeshi tunao kutana nao hadi tukafanikiwa kutoka nje. Tukamkuta Jojo akiwa amewaua wanajeshi wote, hakuna  hata helicopter moja inayo katiza hewani.
 
“Mupo salama?”   
Jojo aliwauliza Magreti na Logate.
“Ndio”
“Tuondokeni”
Tukaingia kwenye moja ya boti ya jeshi na kuondoka eneo hili la meli kwa kasi sana.
“Hawa, na Yemi wapo wapi?”   
“Wamechukuliwa wote wanne”
Logate alinijubu huku akinitazama usoni mwangu.
“Wamechukuliwa na nani?”   
“Wanajeshi wa Marekani, wamechukuliwa, Livna, Yemi, Babyanka na Hawa”
“Baba hao wapo sehemu salama”
“Sawa”
Tukazidi kusonga mbele, huku Jojo akiwa ndio muendeshaji  wa boti hii. Tukafika Pemba katika nyumba tunayo ishi. Tukashuka  sote wanne na kuingia ndani.
 
“Hapa ndipo ninapo ishi karibuni sana”
“Asante”
Magret alijibu huku akishangaa shangaa eneo hili.
“Inabidi kwenda sasa hivi kumvamia K2?”
“Muda huu sio mzuri baba?”
“Kwa nini?”
“Muache ajipange yeye na jeshi lake kwa maana kama tunahitaji kukata mti inabidi tung’oe na mizizi yake”
Jojo alizungumza huku akivua shati lake la jeshi na akabakiwa na sidiria. Akaingia jikoni na kuridi akiwa ameshika jagi kubwa la juisi ya maembe, akawamiminia Magret na Logate kila mmoja kwenye glasi yake.
 
“Jojo K2 anaweza akatoroka?”
“Hana pa kukimbilia kwa maana hakuna nchi duniani kwa sasa ambayo inahitaji kumfadhili K2, kama Marekani mwenyewe tumrmfanya hivyo ulivyo mfanya hivi unahisi ni nani anahitaji kutiwa hasara ikiwa yeye mwenyewe hajajipanga vizuri”
Jojo alizungumza kw amsisitizo, nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaingia chumbani kwangu. Haikupita hata dakika moja Jojo akaingia.
“Baba najua una hasira ya K2 ila kuna kitu ninahitaji kukisubiria kikikamilika ndio tutakwenda?”
“Lini tutakwenda?”
Nilizungumza kwa ukali kidogo huku nikimtazama Jojo usoni mwake.
 
“Ni leo baba, bado muda mchache tu nitakuambia twende tukamvamie K2, ninakuomba unielewe baba yangu”
“Ni jambo gani hilo ambalo unahitaji likamilike?”
Jojo akaka kimya kwa muda huku akinisogela karibu yangu, akasimama futi chache sana kutoka hapa nilipo simama.
“Damu ya Magret itakufanya wewe uishi miaka yote ukiwa kijana na nguvu zako zote na hotokuwa na haja ya kunywa damu tena maishani mwako”
Jojo alizungumza kwa sauti ya chini sana, nikaka kimya huku nikimtazama usoni mwake.
 
“Unataka kumaanisha nini?”
“Ninamanisha kwamba, ninahitaji umuue Magret kwa mikono yako wewe mwenyewe na kuinywa damu yake. Ukiweza kufanya hivyo hakuna ambalo litanshindikana kwenye maisha yako baba yangu”
“Jojo siwezi kumuua Magreti hana hatia yoyote kwenye hili tunalo lifanya?”
“Nalijua hilo baba yangu, sasa hivi ukisema uende kupambana na K2, ana wanajeshi zaidi ya laki mbili wameizingira ikulu, unahisi baba wote watakukosa hata kwa risasi eheeee. Na hapo wakikupiga risasi nilazima ufe, sihitaji kukupoteza baba yangu. Ninakupenda baba, ukifa wewe mimi nitabaki na nani huku duniani, ikiwa wewe ndio mtu wa pekee ambaye unaweza kuishi na mimi na kujua yale yote niliyo kuwa nayo”
 
Jojo alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, nikaka kimya kwa sekunde kadha huku nikimtazama Jojo usoni mwake.
“Hivi Logate akifahamu kwamba nimemua magreti unahisi itakuwaje?”
“Logate ni wangu, nitammaliza mimi mwenyewe. Kumbuka baba kuna malengo mengi unayo takiwa kuyakamilisha kwenye maisha yako pia unatakiwa kuyakakimilisha kwenye hii nchi, tafadhali baba nakuomba ufanye hivyo kwa maana kuna miaka zaidi ya isirini na kitu hivi hadi uje kukutana na raisi ambaye ataipeleka hii nchi kwenye malengo ulio achiwa na babu Hitler”
Jojo aliendelea kuongea kwa msisitizo huku akinitazma usoni mwangu. 
 
“Naomba muda wa kufirikia hili”
“Sawa baba, leo ni lazima tumuua K2 ila lazima ufanye nilicho kuambia baba yangu”
“Nimekuelewa Jojo ninakuomba nipumzike kwanza nifikirie hili”
Jojo akanibusu kwenye paji langu la uso kisha akatoka chumbani humu na kuniacha peke yangu. Nikajitupa kitandani mwangu huku nikifiria ni mbinu gani ninaweza kumuua Magret ambaye kusema kweli roho yangu inaniuma sana katika kutekeleza swala hili.
 
‘Siwezi kumuua Magreti, acha nife mimi ila nilazima nimuue K2 kabla ya mimi kufa’
Niliwaza kimoyo moyo, nikakaa kitako kitandani, hata kabla sijanyanyuka, mlango ukafungulia na nikamuona Magret akiingia akiwa katika sura ya huzuni. Akaufunga mlango kwa ndani na taratibu akaanza kunisogelea nilipo na akakaa pembeni yangu.
Ukimya ukatawala katikati yetu, nikamtazama Magret kwa jicho la kuiba na nikamuona akimwagikwa na machozi usoni mwake.
 
“Unalia nini?”
Nikamuuliza Magreti huku nikimgeukia.
“Dany, sina familia sasa hivi. Wanafamilia wangu wote nimeshindwa kuwalinda na wote wamekufa. Nina haja gani ya mimi kuendelea kuishi kwenye hii dunia.?”
Maneno ya Magreti yakaanza kuufanya moyo wangu kuanza kunienda kasi sana kwa maana ni muda mchache tumetoka kuzungumzia juu ya kumuua.
“Kwa nini unazungumza hayo maneno?”
“Dany, nilisha zoeza kuishi kwenye ile meli, unahisi kurudi huku uraiana na tunaishi sehemu hii ambayo kusema kweli sijazoea Dany, nasikia kufa, nahitaji kufa”
 
‘Masikini weee’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazam Magreti usoni mwake, taratibu akanikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia kwa uchungu. Taratibu akausogeza mdono wake hadi kwenye mdomo wangu, tukaanza kunyonyana midomo yetu huku ndimi zetu zikwa na kazi ya kuchezeana mdomoni.
Hisia za mapenzi zikazidi kupamba kwenye mmili yetu na kujikuta tukianza kuvua nguvo zetu na ndani ya muda mchache sana tukajikuta tukiwa kama tulivyo zaliwa. 
 
Nikaanza kumshuhilikia Magreti ambaye yeye mwenyewe amedhamiria kwamba anahitaji kufa kwenye mikono yangu. Kila muda unavyo zidi kwenda na ninavyo itazama shingo yake, ninajikuta nikianza kuingiwa na roho inayo nishawishi nimng’ate kwenye shingo yake hii.
Ili kuto kuipata tamaa hii, nikamgeuza Magreti na yeye akawa juu yangu huku akiwa amenikalia kisawasawa
 
“Naumia Dany”
“Jitahidi”
Magreti akaanz akuzungusha kiuno chake huku sura yake akionekana kuyavumialia maumivu anayo yapata
“Da….d….y nina…..nina……kupe……”
Gafla nikastukia kumuona Magreti akilala kifuani mwangu, huku shingo yake ikiwa imevunjika. Nikamuona Jojo akiwa amesimama mbele yetu huku akiwa katika hali ya kukasirika na kutisha sana, mikononi mwake anavuja damu nyingi sana.
“Baba unafaya nini sasa…..”
 
Jojo alizungumza huku akihema mihemo inayo tisha.
“Wewe ndio nikuulize unafanyaje?”
“Baba hiyo sio kazi ambayo nimekuambia. Haya sasa nimekurahisishia kumuua kunywa damu yake”
Jojo aliendelea kuzungumza huku akiwa amenikazia macho, kwa kulidhihirisha hilo, akamsukuma Magreti aliye poteza maisha, pembeni yangu. Jojo hakunionea aibu kumuona jogoo wangu ambaye bado amesimama na anahitaji kuendelea na mechi.
“Siwezi kuionyonya damu yake nikiwa katika hali hii”
“Hiyo ndio hali nzuri baba, fanya”
Jojo alizungumza kwa ukali, akazichomeka kucha zake zilizo chongoka kwenye shingo ya Magreti na damu ikaanza kutoka nje.
 
“Mnyonye haraka kabla damu yake haijakauka”
Nikamtazama Jojo kwa muda kidogo kisha taratibu nikausogeza mdomo wangu karibu kabisa na shingo ya Magret na kuanza kumnyonya taratibu damu yake. 

Sikuweza kuisikia ladha wala harufu ya damu yake zaidi ya kuhisi kama ninakunywa maziwa fulani hivi yaliyo changanywa na choclate. Nikajihisi nikipata nguvu nyingi sana hadi ninamaliza mdomo wangu wote umejaa damu. Jojo akanipa mkono wake wa kulia taratibu nikaushika na akaninyanyua kitandani hapa, akaanza kunilamba sehemu zote za mdomo wangu lilizo jaa damu.
“Tunamiaka mingi ya kuishi baba yangu”
“Kweli”
 
“Ndio, ingia bafuni sasa ukaoge, tujiandae na kazi iliyopo mbele yetu”
Nikamtazama Jojo kisha nikamtazama jogoo wangu ambaye bado yupo kwenye ubora wake wa kusimama kama namba moja.
“Mimi ni mwanao siwezi kukusaidia katika hilo”
Maneno ya Jojo yakaniondoka hapa chumbani na kuingia bafuni, nikaoga baada ya muda nikatoka na kukuta maiti ya Magreti ikiwa haipo kitandani mwangu na kitanda kikiwa kimebadilishwa shuka kabisa.
Nikakuta suti nzuri nyeupe pamoja na shati jeupe na viatu vyeupe vikiwa juu ya kitanda. Taratibu nikaanza kuviva taratibu hadi nikamaliza.
 
“Tunadakika ishirini za kukaa hapa kabla ya kuondoka”
Jojo alizingumza huku akiwa amejifunga taulo kifuani mwake.
“Jiandae sasa tuondoke”
“Dakika chache tu nitakuwa nipo tayari”
“Ok fanya hivyo”
Nikamaliza kuvaa na kutoka chumbani humu, nikakuta bastola kadhaa zikiwa zimepangwa juu ya meza pamoja na majambia mawili yenye urefu mkubwa kiasi. Jojo akatoka chumbani kwake huku akiwa amevalia suruali nyeusi inayo meremeta pamoja na kikoti kinacho fanania na surualia yake. Chini amevalia viatu virefu vinavyo fahamika kwa jina la travota. Mkononi mwake ameshika kitambaa cheusi na nywele zake amezibana kwa nyuma.
 
“Nipo tayari baba mbona unanishangaa hivyo”
“Ninakushangaa mwangu uvaaji wako umependeza sana”
“Eti eheee”
“Yaa umependeza sana mwanangu, sasa kweli utaweza kuifanya kazi iliyopo mbele yetu?”
“Niamini baba nitaweza, nimekuandalia bastola zako ninaimani unazipenda kwenye utendaji wako wa kazi”
“Yaaa umejuaje, mimi kubebe silaha kubwa kusema kweli siwezi kabisa”
“Nimeligundua hilo”
“Yaani labda itokee kama dharura tu, ila nikiwa na bastola chochote kilichopo mbele yangu ni lazima nitahakisha ninakihimili.”
 
Jojo akachukua majambii haya mawili na kuyachomeka mgongoni mwake kwenye sehemu maalumu iliyopo kwenye kikoti chake. Nikachukua bastola nne pamona na magazine za kutosha, tulipo hakikisha kwamba tumekamilika katika maandalizi yetu tukaelekea eneo ambalo lina boti yetu na taratibu tukaaondoka eneo hili, huku moyoni mwangu nikijihisi mwenye furaha kubwa sana kwani ninakwenda kukamilisha kibarua kilichopo mbele yangu japo ni hatari ila moyoni mwangu ni furaha sana.
 
“Baba hii inabidi tuingilie na ufukwe wa baharini, kuna ulinzi mkali, ila inabidi kuhakikisha kwamba tunapambana nao, natambua sasa hivi una hisia za kuweza kusikia kitu chochote cha hatari ambacho kinaweza kuja mbele yako, sasa huu ni muda wa kuitumia”
“Sawa Jojo”
“Baba mbona una furaha hivyo”
“Ahaaa nina imani kwamba leo itakuwa ni kazi yangu ya mwisho kwenye maisha yangu kuikamilisha”
“Yaa ni ya mwisho ila ni badae sana tutakuwa na kazi nyingine”
 
“Badae leo?”
“Hapana, ni miaka mingi mbeleni”
“Ok”
Taratibu Jojo akasimamisha boti hii anayo iendesha tukiwa bado hatujafika mahala husika.
“Mbona umesimamisha boti”
Jojo hakunijibu kitu chohchote zaidi ya kukaa kimya, akaitazama saa yake ya mkononi.
“Sasa hivi  ni saa kumi na mbili jioni inabidi tukae hapa hadi saa mbili usiku”
“Mmmm mbona unapelekea masaa mbele?”
“Baba usiku ndio muda mzuri kwako, ngoja nikuambie udhaifu wako mmoja ambao ninauona kwako”
“Ni nini?”
 
“Kukiwa na mwanga, wa jua, hutoweza kuifanya kazi yako kikamilifu, na maadui zako ni lazima uhakikishe kwamba unakabiliana nao usiku”
“So huo ndio udhaifu wangu?”
“Ndio baba, ni vyema nikakuambia mapema kuliko nikaa kimya alafu likajitokeza tatizo na mwisho wa kisku likatokea tatizo na ukashindwa kulihimili hilo tatizo”
“Sawa mwanangu, ila mbona kama tulikwenda kuvamia kwenye meli kule?”
“Ulikuwa bado hujapata mtu wa kukufanya uishi miaka mingi kama ulivyo, umeipata damu ya Mageti na umebadilika sasa baba”
“Sawa mwanangu”
 
Tukakaa hapa hadi ilipo timu usiku wa saa mbili tukaindoka eneo hili kwa kasi sana. Kwa mbali tukanza kuona boti za jeshi zinazo zingira ufukwe wa ikulu. Jojo hakupunguza mwendo kasi wa boti, wanajeshi hawa walivyo jaribu kutuzuia ikawa ni kosa kubwa sana kwako kwani nikaanza kazi ya kuwashuambulia kwa kasi sana ubora wa mashambulizi kwa upande wangu kusema kweli umeongezeka sana. Kila risasi yangu moja inaua mwanajeshi mmoja.
Tukafanikiwa kufika ukingoni, Jojo kama kawaida yake akazidi kuwashambulia wanajeshi hawa kwa kuwakata kata kwa wanajeshi kila alio wafwaata. Baba  na mwana kwa kazi ikazidi kuwa nzito, hatukuwa na huruma yoyote na mwanajeshi yoyote katika eneo hili.
 
Ndani ya nusu saa tukawa tumewamaliza wanajeshi wote wanao linda nje ya ikulu. Ngou zangu zote zimenijaa damu, Jojo ukimtazama mwili mzima naye amatapakaa damu kwani uuaji wake kusema kweli  ni zaidi ya ukatili. Tukaingia ndani ya ikulu, na kukuta walinzi wengine walio jitahidi kutuzuia ila hakuna ambaye anaweza kutuzuia,  tukazidi kupambanana nao hadi tukafanikiwa kuwamaliza wote. Nikafumba macho yangu, nikavuta hisia kwa kasi sana na kugundua kwamba K2 yupo katika mlango mbele yetu. 
 
Nikaanza kutembea kwa taratibu hadi nikafanikiwa kuufikia, nikausukuma kwa nguvu. Nikawakuta wanajeshi wanne walio simama mbele ya K2 huku mikononi mwao wakiwa wameshika bunduki zao.
“Washambulieni………………”
K2 alizungumza kwa ukali sana, nikajaribu kufyatua risasa, ila bastola zangu zote mbili zimeisha risasi na sina magazine yoyote mifukoni mwangu yenye risasi. Hata kabla hawajanifyatulia risasi mbele yangu kwa haraka nikatukia vichwa vya wanajeshi hawa vikianguka chini na miili yao ikafwata kwa kuanguka na akabaki K2 na mwanae wakiwa wanatetemeka kwa woga sana. Hata bastola aliyo ishika mkonon mwake ameshindwa kabisa kuitumia na kujikuta ikimuanguka chini.
 
“K2 ulihisi hatuto onana eheeee?”
Nilizungumza kwa dharau huku nikivua koti langu lililo jaa damu ambazo unaweza hata kulikamua na ukajaza glasi kadhaa za juisi.
“Watu wote hawa wamekufa kwa ajili yako, familia yagu imekufa kwa ajili yako. Mamilio ya wamarekani wamekufa kwa ajili yako. Umejisikiaje?”
 
K2 akazidi kutetemeka, mwanaye haja ndogo ikamtoka.
“Ulihisi  kwamba unaniweza, mimi ni DANY, DANY HITLER. Nimezaliwa kuwa gaidi na nimekuwa gaidi, ulinifanya kijakazi wako, ulinitumikisha NSS, ukanifanya fala nikutumie ku** yako na m** wako, ukanifanya niwe mbali na wale ninao wapenda. So leo hii nipo mbele yako una kipi cha kiniambia.”
K2 naye akaanza kujikojolea, ujanja na umahiri wake mwana mama huyu ukamuisha wote. Hakuishia katika kujikojolea tuu bali hata kujinyea napo kukamtawala.
“Huyo ni mwanao, Bonge. Hembu niambie nimuuaje?”
“Da….add….ny huyo ni mtoto hana tatizo lolote na wewe naomba umsamhehe maisha yake”
“Mmmmmm eti eheee?
“Malaika wangu ulimchinja kwa ujinga wako alikuwa na haki yoyote”
 
Nilizungumza huku nikimnyooshea mkono Jojo, akanikabidhi jambia lake moja, nikavuta mtoto wa K2 kutoka mikononi mwake kuku nikimtazama K2.
“Maamamaaaaa”
Mtoto wa K2 alilia na kumfanya K2 kujaribu kumshika ila Jojo kwa uhodari akamtandika teke la kifua lililo mkalisha chini.
“Sema kwaheri kwa mpumbavu mama yako”
“Ma……..”
Mtoto wa K2 hakuimalizia sentensi yake nikakikata kichwa chake na kumfanya K2 kupiga kelele za kulia kwa uchungu sana nikamrushia kichwa cha mwanae jambo lililo mfanya K2 kurudi nyuma akiogopa kichwa cha mwanae.
 
“Nahitaji dunia iweze kujua leo ninamuua K2, so ni…..”
“Kipo baba chumba cha kurushia matangazo”
Nikamnyanyua K2 kwa mkono mmoja na kuanza kuondoka naye hapa ndani huku Jojo akiongoza kuelekea katika chumba cha mawasiliano. Tukafanikiwa kufika katika chumba hichi, Jojo akaanza kuwasha karma moja baada ya nyingine.
“Mambo tayari”
Nikamvuta K2 mbele ya kamera hizi kisha Jojo kama kawaida akaninyooshea dole ngumba.
“Ninaimani kwamba huyu atakuwa ni mtu wa watu kumuua mbele ya macho yenu. Leo hii nipo tayari kuitangazia dunia kwamba chanzo cha mimi kufanya hivi ni kutokana na K2 kuniulia wazazi wangu kwa kuwachinja.”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimepitisha jambia langu shingoni mwa K2.
“Leo ndio itakuwa mara yangu ya mwisho kumuua mtu kwenye maisha yangu na nipo kwa ajili ya kuisaidia nchi,  maraisi wajao musiwe kama K2 kwa maana nitakuwepo na nitaendelea kuwepo kwa ajili ya kuilinda nchi yangu.
 
Baada ya kumaliza kuyazungumza maneno yangu bila ya huruma nikaanza kuichinja shingo ya K2 na kusababisha damu nyingi kuruka hewani na nina imani kwamba watu wanao angalia matangazo haya ni lazima watafumba macho yao kumshuhudia raisi wao anavyo kufa kikatili sana. Nikakishika kichwa cha K2 na kuusukuma mwili wake pembeni.
 
“Nitarudi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wangu, liwekeni hili akilini”
Baada ya kuzungumza maneno haya nikaondoka mbele ya kamera hii huku nikiwa nimekishika kichwa cha K2, kwa haraka Jojo akanikumbatia huku akiwa na furaha sana.
“Baba umefanikisha, umefanikisha baba yangu kumaliza kila kitu”
“Asante mwanangu. Kina Livna je?”
“Wapo mikono salama baba yangu, twende tukaishi maisha ya amani”
Jojo alizungumza huku akiwa ameniachia mkono wangu, tukaondoka eneo hili la ikulu huku nikitazama maiti za wanajeshi hawa wengi. Tukaingia kwenye boti yetu na kuondoka eneo hili huku tukiwa na furaha na amani sana kwani tunakwenda kuanza maisha mapya yasiyo na tabu wala kutafutana, nikakitazama kichwa cha K2 kwa sekunde kadhaa. Nikakipiga busu kwenye mdomo wake.
“Kwa heri mpenzi wangu K2”
Taratibu nikakitupa kichwa cha K2 baharini na kuanza kushangilia kwa furaha sana kwani sasa amani ipo moyoni mwangu.
                                                                                           MWISHO
Ninamshukuru Mungu kwa kuweza kunisaidia kumaliza stori hii ambayo imenigarimu niezi 9 .Ni stori ambayo kusema kweli imeweza kunipa hatua kubwa ya uandishi kwenye maisha yangu. 

Ninamshukuru Mama yangu kwa kunisupport katika kazi zangu, washabiki zangu, wapendwa wangu na watu wote ambao mumekuwa nami bega kwa bega .

Majina  yote yaliyo tumika kaika stori hii ni ya kutunga. MUNGU ibariki kazi ya mikono yangu, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Ninawapenda sana.

Endeleeni Kufatilia hadithi kali ya POWER inayoendelea kupitia mtandao huu pendwa wa Mpekuzi .

Ndani ya muda mfupi ntawaletea kitu kingine ili kiungane na POWER
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )