Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Asasi zataka muswada vyama vya siasa urekebishwe

adv1
Asasi za Kiraia zimesema licha ya muswada wa Sheria wa vyama vya siasa kuwa na baadhi ya vipengele vizuri, kuna haja ya vile vyenye upungufu kufanyiwa marekebisho kabla ya Bunge kuupitisha.

Viongozi wa asasi za kiraia walisema juzi Dar es Salaam kuna haja ya wabunge kuupa muswada muda wa kutosha kuuchambua kwa kina kabla ya kuupitisha kwani waathirika ni wao, wanasiasa na jamii.

 Fulgen Masawe kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) alisema baadhi ya maeneo mazuri kwenye muswada huo uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba 16 mwaka jana una kipengele cha kukataza vyama vya siasa kuanzisha vikundi vya ulinzi, kutoa mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi, kiulinzi au yanayofanana na hayo kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani kwa siku za baadaye.

Pia wamesifu uwazi katika matumizi ya fedha, mapato na matumizi na uwazi katika maamuzi ya vyama vya siasa kwa kuzingatia maamuzi yanatolewa na viongozi wa ngazi ya juu bila kushirikisha wanachama. 

Akiorodhesha upungufu kwenye muswada huo, Masawe alisema kifungu cha 5A kinataka Msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yoyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika.

Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali, taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka Sh milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume na kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani. 

Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa ya chama chochote cha siasa. 

“Ofisa wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya Sh 1,000,000 mpaka Sh milioni 10 au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12,”alisema Masawe.

Alisema hata baada ya adhabu hiyo, ofisa huyo au chama hicho kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kuminywa, basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili. 

Akinyumbulisha zaidi vipengele hivyo, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Ayakuze alisema Msajili ni mteule wa Rais ambaye analipwa mshahara na serikali hivyo ni vigumu kutofungamana na upande mmoja. 

“Nchi ilikuwa na maslahi kipindi cha chama kimoja lakini tangu vyama vingi, wabunge wanaangalia maslahi yao na vyama vyao kuliko umma, wanaangalia hoja imetolewa na upande gani wanapinga.

“Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda Msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: “Shauri halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi au maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya au kutolifanya kwa nia njema chini ya sheria hii,” alisema.

 Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Fatma Karume alisema “Wabunge wa CCM wanadhani wanalindwa na muswada huu, wanasahau sheria ni msumeno, wanaenda kwenye uchaguzi, wanapaswa kujua kuna kura za maoni ni rahisi kukatwa watu wasiopendwa bila demokrasia hivyo wawe makini,” 

Wakati asasi hizo za kiraia zikiendelea kukazia msimamo wake wa kutaka kufanya marekebisho kwenye muswada huo, tayari CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi, Humphrey Polepole wameuunga mkono.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )