Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Jamhuri yakata rufaa kupinga Tido Mhando kuachiwa huru

Upande wa Jamhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha serikali hasara ya Sh.milioni 887.1, umekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kuachiwa huru Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Leonard Swai alidai kuwa Jamhuri haujaridhika na hukumu hiyo kwamba pamoja na kwamba mikataba inadaiwa kuwa haikufuata sheria lakini mawakili walilipwa fedha,hasara  ambayo imesababishwa na na mshtakiwa.

Rufaa hiyo inasubiri kupangiwa jaji na tarehe ya kusikilizwa.

Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )