Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Jeshi La Polisi Jijini Mbeya Lakamata Watuhumiwa Mbalimbali wa Makosa ya Wizi, Kuingiza Bidhaa Nchini Kinyemela...Tazama Hapa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne [04] kutokana na tuhuma mbalimbali kama ifuatavyo:-
 
KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KULIPIA USHURU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja dereva Bodaboda na Mkazi wa Boda Matenkini Wilayani Kyela aitwaye MUSA MAULID [23] akiwa ameingiza nchini bidhaa aina ya Uyoga – Soya Gold paketi 750 na mifuko laini ya rambo bello tatu [03] toka nchini Malawi bila kulipia ushuru.
 
Mtuhumiwa alikamatwa Januari 24, 2019 saa 06:45 asubuhi huko katika Road Block Kayuki iliyopo Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Bidhaa zilizokamatwa zimekabidhiwa idara ya forodha kwa hatua zaidi za kisheria.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KULIPIA USHURU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja Mkazi wa Lwangwa – Busokelo Wilayani Rungwe aitwaye BAHATI KASUNGULA [35] akiwa na vitenge doti 36 toka nchini Malawi akiviingiza nchini bila kulipia ushuru.

Mtuhumiwa alikamatwa Januari 25, 2019 saa 16:30 jioni huko katika Road Block Kayuki iliyopo Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Bidhaa zilizokamatwa zimekabidhiwa idara ya forodha kwa hatua zaidi za kisheria.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja JUHUDI KASYUPA [25] Mkazi wa Majengo Wilayani Chunya akiwa na mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi.
 
Mtuhumiwa alikamatwa Januari 27, 2019 saa 13:30 mchana katika msako uliofanyika huko katika Kijiji cha Majengo, Mtaa wa Pili, Kata ya Nkung’ungu, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Vitu alivyokamatwa navyo mtuhumiwa ni:-
 1. Box moja la Daftari ndogo,
 2. Radio moja muundo wa sub woofer aina Aborder na Spika zake mbili, spika moja aina ya sony,
 3. Deki moja aina ya Samsung,
 4. Betri moja ya Sola aina Sundar,
 5. Screen moja ya Computer Dell,
 6. T.V moja aina Tandar,
 7. Kopo moja la rangi Cream,
 8. Stablizer moja,
 9. Solar inveter moja,
 10. Waya wa cable mmoja,
 11. Solar panel moja aina ya oceanic wat 4o
Aidha baada ya mtuhumiwa kupekuliwa alikutwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia ambavyo ni nondo, bisibisi moja vitu vyote hivyo vilikutwa ndani kwake Mtuhumiwa alipohojiwa kuhusu umiliki wake alishindwa kuelezea. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JUMA ADAMSON [23] Mkazi wa Mbozi Mkoa wa Songwe akiwa na copper plate tatu [03] mali idhaniwayo ni ya wizi.
 
Mtuhumiwa alikamatwa Januari 27, 2019 saa 10:00 asubuhi katika msako uliofanyika huko mlima Reli, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya. Baada ya mahojiano imebainika kuwa mtuhumiwa ni kati ya wahalifu sugu wanaofanya wizi wa kushusha mizigo katika milima Songwe, Iw ambi, na mlima nyoka pindi magari ya mizigo yanapokuwa yakipanda mlima kwa mwendo mdogo. Upelelezi wa ushauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
 
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )