Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

Katika kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, kanisa la Shekinah Presbyterian Madale Lajitolea kufanya usafi katika jiji la Dar es Salaam

adv1
Waumini wa kanisa la Shekinah Presbyterian Tanzania wamezindua rasmi zoezi la kufanya usafi kwa kujitolea katika mtaa wa Madale mahali kanisa lilipo. 

Katika kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi, walizindua zoezi hili katika serikali ya mtaa wa Madale. Wakiongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mch. Daniel John Seni asubuhi na mapema walianza usafi katika kituo cha daladala cha Madale mwisho, baadaye Kisauke shule, na kisha Madale sokoni.

 Baada ya kusafisha katika maeneo hayo waliondoka moja kwa moja mpaka kwenye serikali ya mtaa wa Madale ambapo katibu/Msaidizi wa kanisa ndugu George Shiganga alitoa maelezo kwa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo.

Wakiongozwa na Kauli mbiu ya  “USAFI WA MAZINGIRA NI SEHEMU YA UTAKATIFU,” mchungaji Daniel alifafanua kwamba “hakuna kitu ambacho kilianzia kwenye imani kikashindikana.” 

Mchungaji huyu alielezea kuwa “Siyo kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ndugu Makonda ameshindwa kwenye zoezi la usafi, tatizo ni wapi alianzia.” Alikaza kwamba “sisi katika kumuunga mkono mkuu wetu wa mkoa; tumekuja na mbinu mpya ambayo tunapenda watu wa dini zote katika Mkoa wa Dar es salaam waige, na mbinu hiyo ni kuwafundisha waumini wetu kwa vitendo na kuwabadilisha katika mawazo.” 

Aliendelea kusema kuwa “Katika kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanya na serikali ya awamu wa tano, tunapaswa kupunguza maneno na tuongeze kwenye vitendo zaidi, ifike mahali wachungaji tuwaambie wazi waumini wetu kwamba uchafu ni dhambi! Na kama uchafu ni dhambi, maana yake wakristo wote wanapaswa kuwa wasafi kuanzia rohoni hadi nje (mazingira). 

Alisisitiza kwamba kanisa lazima liwe na athari chanya katika jamii. Kazi ya mchungaji siyo kukemea pepo tu, bali ni kuwafundisha waumini pia waweze kujitolea kwenye jamii inayowazunguka. 

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale bwana Mberwa aliwashukuru sana waumini hawa, na kuomba watu wa dini zote kuhubiri habari za usafi katika makanisa na misikiti yao, ili kujenga fikra mpya kwao. Katika kuhakikisha kwamba zoezi hili linakuwa ni endelevu, waumini hawa wamekubaliana kwamba watakuwa wanafanya usafi mara moja kwa mwezi kwa kujitolea.

Mchungaji Daniel aliwakaribisha watu wa Madale ambao wangependa kuunga mkono zoezi hili la usafi kuwasiliana naye kwa 0769080629 ili kupata ratiba kamili ya zoezi zima.

Imetolewa na ofisi ya kanisa la Shekinah Presbyterian Church
Madale Dar es salaam.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )