Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya Wema Sepetu Kusambaza Video ya Ngono

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Januari 28, 2019 imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi wa kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu unakamilika kwa wakati.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mitandao ya kijamii.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Awali, wakili wa Serikali, Mosia Kaima amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi wa shauri hilo utakuwa umekamilika ama la.

Baada ya wakili huyo kueleza hayo, wakili wa Wema, Ruben Simwanza aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imeshatajwa mara nne mahakamani hapo huku upelelezi wake ukiwa bado.

"Naomba upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati kwa sababu shauri hili limeshatajwa kwa mara ya nne sasa, bila upelelezi wake kukamilika," amedai Wakili wa Utetezi.

Hakimu Kasonde baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 itakapotajwa tena na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.

Katika kesi ya msingi, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )