Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 29, 2019

Lulu Michael Agoma Kuzungumzia Taarifa za Kupigwa na Mchumba Wake

juu
Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu amesema taarifa za kuwa amepigwa na mchumba wake hataki kuzizungumzia kwa kuwa anaona zinalenga kumtoa katika njia yake anayotaka kwenda kwa sasa.

Akizungumza leo Januari 29 katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio E FM, amesema habari hizo zilianza kuenea baada ya kutangaza kampeni yake ya Save my Valentine wiki iliyopita.

“Kama umeshawahi kutazama filamu za mapigano mwishoni utaona adui anavyojaribu kufanya vitu vya kumhadaa sterling, hivyo ndivyo nilivyochukulia maneno haya,” amesema.

Ameongeza kuwa utakapofika wakati sahihi atalizungumzia hilo na kwamba kwa wakati huu angependa kuendelea na kampeni yake ya kusaidia wasiojiweza.

Akizungumzia kampeni hiyo ya kusaidia wenye uhitaji amesema itaendeshwa kwa fedha anazopata katika mauzo ya nguo zake lakini amewaomba watu binafsi na mashirika wanaotaka kushirikiana naye wajitokeze.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )