Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Mahakama Yamwachia Huru Aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu Wa NIDA Na Wenzake Sita

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake 6 waliokuwa wakikabiliwa na kesi  ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh.Bilioni 1.16 kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka' (DPP) hana nia ya kuendelea  na mashtaka dhidi ya washtakiwa

Washtakiwa hao wameachiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo,  mara baada ya vigogo hao kuachiwa  huru na kutoka nje ya chumba cha mahakama, walikamatwa tena na kuwekwa chini ya ulinzi na polisi na baadae kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kati.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )