Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Awahamasisha Wabunge Kutembelea Vivutio Vya Utalii

juu
Na Lusungu Helela-Iringa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wabunge wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chachu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi wanawaongoza  kwa kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
 
Imeelezwa kuwa hamasa ya wananchi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini imekuwa na mwitikio mdogo ukilinganisha na idadi ya watalii wa kutoka nje.
 
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku mbili ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.
 
Amesema endapo kila Mbunge kwa nafasi yake ataweza kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii mapato yataweza kuongeza maradufu kupitia Utalii wa ndani tofauti na ilivyo sasa.
 
“Tengeni muda wa kupumzika baada ya pilikapilika ya kuwahudumia wapiga kura wenu, unakuja huku Ruaha unapumzisha akili huku ukijipanga  mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu” alisema.
 
” Tusisubiri tuje kikazi kama tulivyokuja hivi, Panga njoo na familia yako ufurahie maisha mara moja moja sio mbaya” Alisisitiza Kanyasu.
 
Pia, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao  kila wanapopata nafasi ya kukutana na wananchi majimboni mwao wawahamasishe kutembelea vivutio vya utalii ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa jitihada anazofanya za kutaka kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii.
 
Amesema ufufuaji wa kampuni la usafiri wa ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege saba achilia mbali mradi wa reli ya Standard Garge ni juhudi wazi za  Rais John Magufuli kuona sekta ya utalii inagusa maisha ya kila wananchi kimapato.
 
Katika hatua nyingine, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa za utalii kwa kujenga Hoteli au kwa kuanzishavituo vya  utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na watalii wengi wa kutoka nje.
 
Aidha, Mhe.Kanyasu aliwaeleza Wabunge hao kuwa baada ya kufungua utalii Kusini, Serikali inakusudia kufungua utalii katika kanda nyingine ikiwemo ya kanda ya  ziwa na kanda ya Kaskazini Magharibi, Hivyo wawaandae wananchi wao kuchangamkia fursa za utalii badala ya kubaki walalamikaji.
 
Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alisema kufunguliwa mapema kwa utalii Kusini kutatoa picha halisi kwa wananchi katika kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo katika kanda nyingine
 
Pia, Mhe, Nape aliishauri Serikali kulifanyia kazi suala la  tozo ya kuingia ndani ya hifadhi (single entry) kutokana na  malalamiko ya muda mrefu wanayoyatoa wananchi kwanaoishi Katibu na Hifadhi kuwa imekuwa ikiwabana watalii kutoka nje ya Hifadhi kuwatembelea wananchi hao.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )