Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 29, 2019

Ofisa wa TRA anayedaiwa kumiliki mali za Milioni 721 Kusomewa Maelezo ya Awali February 20

juu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  imepanga Februari 20, 2019, kumsomea maelezo ya awali ofisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Godfrey Mapuga anayekabiliwa na shtaka moja la kumiliki mali zenye thamani ya Sh721milioni zisizoendana na kipato chake cha sasa na cha zamani.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Januari 29, 2019 na hakimu mkazi, Salum Ally baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Wakili wa Serikali mwandamizi,  Vitalius Peter amedai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo umeshakamilika.

Baada ya maelezo hayo hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 20, 2019 siku ambayo upande wa mashtaka utamsomea maelezo ya awali mshtakiwa.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 13/2019, Mapunga amedaiwa kumiliki viwanja vitatu pamoja nyumba  moja ya ghorofa, ambavyo haviendani na kipato chake.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Aprili  Mosi, 2011 na Julai 19, 2016 eneo la  Ubungo.

Mapuga akiwa mtumishi wa umma, anadaiwa kumiliki nyumba  moja ya ghorofa iliyopo Goba manispaa ya Ubungo yenye thamani ya Sh698.9milioni  ambayo haiendani na kipato chake.

Pia katika kipindi hicho, mshtakiwa anadaiwa kumiliki kiwanja kimoja ambacho hakijasajiliwa kilichopo eneo la  Mbezi Juu, manispaa ya Ubungo chenye thamani ya Sh 7milioni.

Vile vile, anadaiwa kumiliki ardhi ambayo haijasajiliwa iliyopo eneo la Kigamboni yenye thamani ya Sh 6milioni.

Mapuga anadaiwa kumiliki kiwanja ambacho hakijasajiliwa kilichopo Goba chenye thamani Sh 9.5miloni na kufanya idadi ya mali anazodaiwa kumiliki ambazo haziendani na kipato chake cha sasa na cha zamani kufikia Sh721.4milioni.

Mshtakiwa ambaye anatetewa na wakili,  Mluge Fabian  baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili alikana ya yupo nje kwa dhamana.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )