Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 25, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 60

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
“Sawa, muunge mkono mama.”
“Acha basi nieeleke nyumbani kwake. Tutawasiliana mume wangu”
“Nashukuru”
Biyanka akanipiga busu na kutoka ndani humu. Majira ya saa sita usiku nikaondoka hotelini hapa na kwenda kwenye hoteli Ramada, nikawatarifu Qeen na Latifa waweze kufika katika hoteli hii na nikawapa maelekezo ya chumba nilichopo. Baada ya kama dakika aruboini hivi wakaweza kufika hotelini hapa.
“Mkurugenzi umetuita usiku sana vipi kuna tatizo?”
“Hakuna tatizo, ila tunakwenda kuianza kuianza kazi ya kumuangusha mgombea wenu munaye mpenda bwana Poul Mkumbo katika uchaguzi huu”
Qeen na Latifa wakabaki wakiwa wameduwaa, kwani wanafahamu uhusiano wangu wa kimapenzi na Biyanka na mtu ninaye hitaji kumfanyia ukatili ni baba yangu mkwe mtarajiwa.

ENDELEA   
“U..nataka kuniambia kwamba mtu tunaye hitaji kumuangusha katika hii kazi ni muheshimiwa Poul Mkumbo?”
Qeen aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Ndio.”
“Ethan huoni kwamba huu unaweza kuwa ni mtihani mkubwa sana?”
 
“Kila mtihani una majibu yake na kila mtihani kuna kufaulu na kufeli. Ukiweka asilimia nyingi za kufeli ndivyo utakavyofeli na ukiweka asilimia nyingi za kufaulu ndivyo utakavyo faulu. Mumenielewa warembo?”
“Ndio Ethan”
“Kaaeni pale, nina kikao kidogo na wafanyakazi wangu”
“Kikao?”
“Ndio mbona muna shangaa?”
“Kikao si tupo wachache kiasi hichi?”
“Sio nyinyi mutawaona”
Nikafungua laptop yangu na kufanya mawasiliano na wakurugenzi nilio waachia kampuni zangu ninazo zimiliki. Ndani ya dakika tano wakurugenzi wote tukawa tunaonana kwenye mtandao huu. 
 
“Habari zenu?”
“Salama mkuu”
“Nahitaji uwakilishi wa maendeleo  ya kila mmoja katika kampuni yangu. Wakurugenzi hawa ambao nikikutana nao mimi ndio raisi wao wakaanza kuwakilisha ripoti ya maendeleo kama nilivyo waagiza waweze  kuwakilisha. Kila ripoti ya kila mmoja ina maendeleao makubwa, na kampuni zimepata faida kubwa toka nilipo anza kuziongoza na ubadhilifu wa mali za kampuni zangu umepungua kwa asilimia kubwa sana.
 
“Kazi nzuri kwa kila mmoja wenu. Ila kwa sasa tuna kazi ambayo nina hitaji muweze kunisaidia”
“Kazi gani raisi?”
“Nahitaji kuunga mkono juhudi za chama cha upinzani hapa nchini. Nahitaji kuangusha chama kilocho madarakani”
“Ahaa muheshimiwa raisi, kumbuka sisi ni wafanya biashara na endapo tukiingilia siasa za nchi fulani itaweza kutuletea matatizo hapo baadae”
“Ninalitambua hilo. Kila kitu kitakwenda kwa siri sana, na endapo raisi wa upinzani ataongoza nchi, hiyo pesa tunayo kwenda kuiwekeza, ndani ya miezi sita itarudi mikononi mwetu kwa maana kuna migodi mingi na mali nyingi ambazo watatupatia”
 
“Hapo sawa raisi, nini unahitaji tufanye?”
“Kila oda ya nguo za siasa ambazo wahahitaji mkurugenzi Jong utashuhulika katika kiwanda chako cha kutengeneza nguo. Kuna kiasi cha dola za kimarekani bilioni mbili, nitakihitaji kutoka kwenu, kila mmoja atafahamu anatoa kiasi gani sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Kikao kikamalizika na nikazima laptop yangu na kuwageukia Qeen na Latifa.
“Hivi hao wazee wote wapo chini yako Ethan?”
“Ndio wote ni wafanyakazi wangu. Kuna wachina humu, waingereza, warusia, wajerumani, waspain, wabrazil na Wamarekani”
“Aisee unajua sisi tulikuwa tunahisi kwamba kampuni unayo imiliki ni hii moja?”
“Mumesahau nili waambia ni kampuni ngapi ambazo nina miliki?”
 
“Mimi nimesahau.”
“Tuachane na hilo, hembu wasiliana na yule shemeji yako”
“Usiku huu?”
“Ndio, kila kitu kitakuwa kinafanyika usiku usiku tu, hatuna muda wa kupoteza zimebaki wiki mbili kampenzi zianze”
Latifa akawasiliana na shemeji yake, kisha akanipatia simu niweze kuzugumza naye.
“Ndio boss”
“Nahitaji kuonana na viongozi wako. Vipi ulisha lipanga hilo jambo?”
“Ndio nilisha lipanga na nilisha waeleza”
“Basi kesho majira ya saa nane usiku nitawalekeza ni wapi tuweze kuonana.”
 
“Sawa sawa muheshimiwa”
“Namba yako nitaichukua kwa huyu binti hapa”
“Sawa kiongozi”
Nikakata simu na kumrudishia Latifa simu yake.
“Kesho latifa nahitaji namba ya simu mpya ambayo sio ya kampuni yetu pamoja na simu ndogo sana. Umenielewa?”
“Sawa sawa mkuu”
“Qeen fikiria ni eneo gani la siri ambalo kesho sote tunaweza kuonana na kupanga mpango  wa kujua ni jinsi gani tunaweza ninawasiaida”
“Nimekuelewa mkuu”
“Kwa leo ni hayo, sijui muna mpango wa kurudi nyumbani kwenu au kwa maana sasa hivi ni saa kumi kasoro dakika kumi”
 
Nilizungumza huku nikiitazama saa ya mkononi mwangu.
“Hapana ni hatari kwa mtoto wa kike”
“Sawa nimewaelewa, jambo jengine la msingi. Hakikisheni kwamba muna tunza siri hii. Hii ni vita ambayo mmoja wetu atakapo kuwa na domo la kubwabwaja maneno. Ninawaahakikishia kwamba atakufa, siwatishi ila ninahitaji kuwaleza ukweli juu ya hilo”
“Tumekuelewa mkuu”
Nikajitupa kitandani, Qeen na Latifa wakanifwata huku wakinitazama kwa macho ya matatamanio.
 
“Nimekumbuka jambo moja muhimu sana”
Nilizungumza huku nikika kitako kwa maana leo sijisikii kufanya mapenzi na wasichana hawa isitoshe tupo katika wiki ya kufanya kazi, ni lazima akili yangu iweze kupata nafasi nzuri ya kuweza kufirikia mipango yangu muhimu ya kuhakikisha nimpiga adui yangu kimya kimya.
“Ninahitaji mwana sheria mmoja aliye soma, mwenye ujuzi mkubwa sana na anaye weza kuzugumza na bubu”
“Bubu!!?”
“Ndio”
“Kuna nini?”
“Kuna kijana mmoja jana mchana tulikwenda kumtazama pale Central Polisi, alikamatwa kwa kosa la kuiba kuku mtaaani huko ila wao wamebambikia kesi ya kunitishia kuniau. Munaweza kukumbuka juzi nilivyo toka kuchukua pesa, nilisoma meseji moja na nikapoteza amani hadi wewe ukaendesha gari”
“Ndio ninakumbuka”
 
“Sasa sihitaji kijana yule aweze kubeba kesi moja akubwa namna hiyo ikiwa ana hitaji kuwa huru. Yule ambaye amefanya tukio hilo hapo nina mtambua vizuri sana, ila nitahitaji mtu sahihi ambaye anaweza kunifanyia kazi ya kuweza kumtafuta kimya kimya na kumkamata kwa maana ni mtu hatari”
“Boss kama unamfahamu ntu huyo ni kwa nini usitoe ripoti polisi wakamkamata?”
“Siwaamini polisi kwa maana wao wanakula sahani moja kabisa mgombea uraisi. Unahisi kuna nini kitakacho endelea hapo”
“Mmmm na kweli polisi Hawato fanya jambo lolote kwa huyo jamaa”
“Nani muna mjua jua mwenye uwezo wa kupigana pigana”
“Kwa mimi sifahamu”
“Hata mimi kwa kweli sifahamu”
“Basi acheni, nitalishuhulikia mwenyewe”
 
Mazumzo yalivyo  kata, Qeen, akaanza uchokozi wa kunishika shika mapajani, nikatamani kuzungumza jambo fulani ila jog** wangu tayari alisha anza kunyanyuka na kujikuta nikikubaliana nao tu waweze kufanya kile walicho kikusudia kukifanya. 

Ndani ya dakika chache tukajikuta tukizama kwenye penzi zito huku nikihakikisha kwamba kila mmoja nina mpatia haki yake sahihi. 

Tulipo maliza mizunguko mitatu tukajiandaa na kuanza kuondoka majira haya ya saa kumi na moja alfajiri. Nikawapitisha hadi kwenye nyumba wanayo ishia kisha nami nikarudi hotelini kwangu. Sikuhiataji kulala, nikabadilisha nguo na kuelekea ofisini ili niwahi foleni ya jiji hili la Dar as Salaam.
 
“Habari ya asubuhi mkurugenzi”
Wafanyakazi wangu walinisalimia
“Salama”
Niliwajibu huku nikiingia nao kwenye lifti, tukapandisha hadi gorofani ambazo ndipo zilipo ofisi za baadhi ya wafanyakazi wa vingengo mbali mbali pamoja na ofisi yangu.
 
“Mkurugenzi za kuamka”
Sekretari wangu alinisalimi  huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Salama, ehee niambie kuna mpya gani?”
“Ahaa raisi wa TFF, ameomba aweze kukutana na wewe leo saa tatu asubuhi”
“Raisi wa TFF, ndio nani?”
“Ohoo ni raisi wa shirikisho la mpira wa miguu hapa Tanzania. Nahisi jana aliweza kupokea lile pendekezo la kampuni yetu kuanzisha kombe lake”
“Ahaa sawa mkaribishe”
“Sawa mkurugenzi”
 
Nikaingia ofisini kwangu, nikaikagua ofisi hii nilipo jiridhisha na usafi ulio fanywa na sekretari wangu nikaka kwenye kiti changu.Majira ya saa tatu nikapata ugeni huu wa raisi wa TFF, nikamkaribisha ofisini kwangu kwa mazungumzo zaidi.
“Heshima yako mzee”
“Nashukuru. Nafurahi kukutana na wewe Ethan”
“Nashukuru muheshimiwa.”
“Jana nilipo pokea pendekezo la wewe kuanzisha ligi yako. Kwanza nilistuka kidogo kwa maana ni wawekezaji wachache sana wa Kitanzania wanao penda kuwekeza katika soka, tena nchini Tanzania. Nilipo kuja kujua dau ni dola laki moja na nusu, nikasema ahaa hapa si pakupaachia paende bure bure au wewe ndio utufwate”
 
Mzee huyu alizungumza huku akijichekesha chekesha.
“Ndio unajua mimi ni mchezaji”
“Mchezaji?”
“Ndio, inabidi uweze kufwatilia baadhi ya mechi zangu. Ila ngoja”
Nikaingia katika mtandao wa YouTube kwa kutumia simu yangu ya mkononi na kutafuta baadhi ya video zangu na nikamuonyesha mzee huyu. Akaanza kuzifwatilia, uso wake ukazidi kunawiri kwa tabasamu  pana usoni mwake, kwani vitu nilivyo vifanya kwenye mpira ni vya kustajabisha.
 
“Aisee ni kama Messi vile”
“Yaaa nina uwezo mkubwa wa kucheza mpira, hapa nina subiri mambo yangu fulani yakikaa sawa, basi nitachagua moja ya klabu kubwa duniani nitaichezea”
“Kwa nini usichezee Simba au Yanga ili uendelee kuborosha vipaji vya wachezaji hapa Tanzania”
“Hahaa, hakuna timu ambayo ina mchezaji mwenye kiwango changu. Njia nzuri ya mimi kuboresha mpira wa miguu hapa Tanzania ni kuanzisha hiyo ligi. Kingine nitahakiksha kwamba nina miliki timi yangu ambayo itaanzia chini kabisa daraja la chini hadi ipande darala la ligi kuu”
“Ohoo utakuwa umefanya la maana”
“Jambo jengine ninalo weza kufanya ni kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania”
 
“Hivi wewe ni Mtanzania halisi kweli, kwa maana yule jamaa alivyo niletea ripoti yako sikuwa nina amini amnini?”
“Ndio, mimi ni mchaga kabisa”
“Duuu safi sana, niwachaga wachache sana wanao cheza mpira na wengi wao wanapenda biashara biashara”
“Ni kweli. Jambo la kufanya ni wewe kunitengenezea mazingira ya kuanzisha hiyo ligi, na nitafutie eneo moja ambalo nitaweza kujenga kiwanja changu cha mpira”
“Weeee!!!?”
“Mbona una shangaa mzee kwani mimi ndio nitakuwa wa kwanza kujenga kiwanja, si yupo aliye nitangulia mmiliki wa Azam Club”
“Kweli kweli, ila jinsi unavyo zungumza yaani nina piga picha hicho kiwanja jinsi kitakvyo kuwa”
 
“Hakikisha ligi yangu inafanikiwa kuingia kwenye mzunguko wa nchi hii, na pia nina pata sehemu ya kiwanja changu, baada ya hapo nitakupa fungu lako ambalo hadi unakufa utakuwa unalitafuna hata ukiamua kuto kupokea umshahara wako wa uraisi wa TFF”
“Weee, sawa sawa muheshimiwa nashukuru, tena nashukuru sana”
Mzee huyu alizungumza kwa heshima kubwa sana. Nikaagana naye na akatoka ofisini humu, Latifa akaingia ofisini kwangu na kunikabidhi simu niliyo muagiza.
“Qeen amefahamu ni wapi tukutane?”
“Bado anafikiria”
“Muambie akifahamu aniambie. Humu kuna salio la kiasi gani?”
 
“Elfu kumi”
“Itatosha kweli?”
“Ndio muheshimiwa na namba ya shemeji yangu ipo humu”
“Poa nashukuru”
Muda wa mchana, Qeen akanieleza ni eneo gani ambalo tunatakiwa kukutana na watanielekeza kwa simu kuweza kufika huko. Nikamjulisha bwana Samweli ni eneo gani tunaweza kuonana saa nane ya usiku ili tuweze kupanga mipango ya kuweza kuonana. Nikiwa ndani ya gari langu nikielekea ofisini kwangu nikitoka kupata chakula cha usiku, Biyanka akanipigia simu, tukasalimiana kwa furaha sana.
 
“Vipi mipango yenu?”
“Inakwenda vizuri na tunarudi leo by saa nne usiku tutakuwepo Dar es Salaama, baba anatuhitaji mimi na wewe nyumbani anasema kuna kikao muhimu sana cha kuweza kufanya kama wana familia”
Nikajikuta nikiishiwa na furaha yangu, kwani sikutarajia kumuona Biyanka akirudi leo jijini Dae sa Salaam kwani anaweza kuwa kipingamizi kikubwa sana cha mipango yangu niliyo ipanga kwa siku ya leo.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )