Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Tundu Lissu Kuanza Ziara Ulaya na Marekani Kesho

adv1
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia kesho. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, anafanya ziara hiyo siku chache baada ya kutoka katika matibabu nchini Ubelgiji.
 
Katika ziara hiyo mbali na kufanya vikao kadhaa na viongozi wa kiserikali na jumuiya mbalimbali, pia atapata fursa ya kutoa mihadhara ya kitaaluma na kufanya mahojiano na vyombo vya habari.
 
Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilieleza kuwa Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, atakuwa nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali na wabunge wa Bunge la Ujerumani.
 
“Baadaye Lissu atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji ambako atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU,” alisema Makene.
 
Alisema baada ya Ubelgiji, Lissu ataelekea Washington DC, Marekani ambako atakaa kwa siku 10 na kukutana na Watanzania wanaoishi nchini humo, hususan katika maeneo ya Washington, Houston, Texas, Birmingham na Alabama, pamoja na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) na kamati za mabunge yote mawili ya nchi hiyo zinazohusika na uhusiano wa nje (Afrika).
 
“Katika ziara hiyo, Lissu atapata fursa ya kuwasilisha mada juu ya masuala mbalimbali katika taasisi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na Center for Strategic and International Studies (CSIS) na The Atlantic Council and the World Resources Institute (WRI). Lissu ana historia na taasisi ya WRI kwani aliwahi kuwa mmoja wa watafiti wake miaka ishirini iliyopita,” alisema Makene.
 
Alisema akiwa mjini Washington DC, Lissu atakutana na kufanya mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vilivyoko mjini hapo.
 
Makene alisema Lissu atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mhadhara mkubwa wa umma katika Chuo Kikuu cha George Washington (GWU) ambacho ni moja ya taasisi kongwe na kubwa za elimu ya juu nchini humo na duniani kwa ujumla.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )