Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 6, 2019

Wajasiliamali Wadogo Mihambwe Wamshukuru Rais Magufuli

adv1
Na Emmanuel Shilatu, Mihambwe
Wajasiliamali wadogo wa Kata ya Kitama wamemshukuru Rais Magufuli kwa Kuja na majawabu ya changamoto zao hususani suala la kutozwa Kodi kubwa isiyoendana na mitaji wala mauzo yao.
 
Wajasiliamali hao wameyasema hayo mbele ya Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu wakati alipoenda kutoa elimu na hamasa juu ya vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo.
 
”Naomba Afisa Tarafa utufikishie salamu zetu kwa Rais Magufuli, mueleze sisi Wajasiliamali wadogo hatuna cha kumlipa kutokana na kuendelea kutupigania tufanye biashara zetu kwa amani na kwa faida. Hivi vitambulisho tumevipokea kwa mikono miwili maana ni mkombozi wetu” alisema Mjasiliamali mdogo mmojawapo.
 
Akizungumza kwenye mkutano huo Gavana Shilatu alipiga marufuku Wafanyabiashara wakubwa ama Watu wasio wajasiliamali kuchukua vitambulisho hivyo.
 
”Hivi vitambulisho havitolewi kwa Wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa zaidi ya Tsh. Milioni 4 ama kwa Watu wasio wajasiliamali, Ni marufuku kabisa. Hivi vitambulisho tuwaachie wajasiliamali wadogo wenye mitaji midogo ili nao wapate fursa ya kukua wawe wajasiliamali wakubwa” alisema Gavana Shilatu.
 
Jana Jumamosi Januari 5, 2019 Gavana Shilatu alitoa elimu na hamasa kwa Wajasiliamali wadogo wachukue vitambulisho hivyo kwa kata za Kitama na Miuta na mwitikio ulikuwa mkubwa sana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )