Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Zitto Kabwe ahofia usalama wake....Tazama Hapa Alichoandika

juu
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anahofia usalama wake kutokana na taarifa alizozipata, akisema kuna mpango wa kumdhuru.

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia agenda za muungano wa vyama 10 vya upinzani kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, alieleza kupitia mtandao wa Twitter, akionya wale walionuia kumdhuru.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe ameandika: “Tunafahamu kuwa Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ‘ Vita ya Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI( mie huyo). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha. SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslani” alisema katika ukurasa huo.

Alipotafutwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi,  Zitto amesema amepata taarifa hizo kutoka kwa vyanzo vyake lakini hawezi kutoa taarifa  kwa kina.

“Suala la usalama ni suala nyeti sana, kwa hiyo habari nilizotoa ndiyo hizo hizo. Kukiwa na jingine nitaeleza. Ile Tweet inatosha, ndiyo maelekezo niliyopewa na walionipa taarifa. Siwezi kwenda mbali zaidi maana naweza kujikuta nawaharibia maisha walionipa taarifa,” alisema.

Alipoulizwa iwapo amewasilisha au kutoa rasmi taarifa hizo polisi kwa ajili ya kulipa jeshi hilo jukumu la kufuatilia suala hilo, amesema. “Sijatoa taarifa Polisi kwa sababu maalumu” alisema.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )