Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 13, 2019

Zitto Kabwe Kuweka Hadharani Majibu Aliyojibiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Kuhusu Sakata la CAG Kuhojiwa na Bunge

juu
Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, ameahidi kuwa leo ataweka hadharani majibu aliyopatiwa baada ya kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA).

Zitto aliandika barua hiyo akipinga hatua iliyochukuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya, Kinga na Haki ya Bunge kuhojiwa.

Mbunge huyo na Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, aliwatumia barua hiyo maspika wa mabunge yote ya Afrika kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali wa Afrika katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola pamoja na wale wa nchi za Jumuiya ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC).

Hatua hiyo imekuja baada ya Spika Ndugai kumtaka Prof. Assad kufika mbele ya kamati hiyo Januari 21, mwaka huu, kujieleza kuhusu kauli yake aliyoitoa akiwa nchini Marekani kuwa ‘Bunge ni dhaifu’.

Kwenye barua hiyo aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Zitto alieleza kuwa amewaomba viongozi hao waongee na Spika Ndugai ili aachane na uamuzi wake wa kumwita CAG kuhojiwa na Kamati ya Bunge.

Sehemu ya barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CPA, Akbar Khan, ilieleza:

“Kwa kuwa Bunge la Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola, naiomba ofisi yako ifanye mawasiliano ya kidiplomasia kwa kuwasiliana na Spika wa Bunge la Tanzania kumweleza hatari ya uamuzi anaotaka kuuchukua,” alisema na kuongeza:

“Ninaamini suala hilo linaweza kumalizwa kwa ustaarabu na kuimarisha uhusiano kati ya taasisi hizo mbili, yaani Bunge la Tanzania na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambao wote wanategemeana katika ufanyaji kazi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )