Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 22, 2019

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Yaja Kimkakati Kuzuia Upotevu Wa Mahindi Baada Ya Kuvuna

adv1
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa wito kwa wakulima na wasindikaji wa zao la mahindi kuwekeza katika teknolojia za kisasa kwa lengo la kuzuia upotevu wa mahindi baada ya kuvunwa ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha wakati akizungumza na wawekezaji katika usindikaji wa zao la mahindi mara baada ya kuzindua mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo.

“Natoa wito kwa wasindikaji kutumia fursa za mradi huu ili kuongea tija katika shughuli zao,” amesema.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando amesema kuwa mfuko huo umelenga kuwajengea uwezo wasindikaji wa ndao kuwa sehemu ya uongezaji wa thamani wa mnyororo wa zao hilo.

“Tunaamini Mradi huu utasaidia kuzuia upotevu wa mahindi hivyo kuleta tija kwa wakulima wa zao hili,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wasindikai walioshiriki katika uzinduzi wa Mradi huo, Bw. Savior Chanay kutoka Kampuni ya Real World ya mkoani Ruvuma ameishukuru Serikali kupitia TADB kwa kuja na Mradi huo ambao utaongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mahindi.

“Mradi huu utaleta tija katika shughuli zetu za kila siku hivyo kuongeza uwezekano wa kuongeza kipato kwa wakulima wa mahindi,” amesema
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )