Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 24, 2019

Dereva Aliyekufa Ajalini Songwe Kushitakiwa

juu
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Fortunatus Muslim ameagiza dereva wa gari lililosababisha ajali iliyoua watu 19 akiwamo yeye mwenyewe katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoa wa Songwe ashtakiwe.

Aidha, ametoa maagizo matatu ya kutekelezwa haraka ili kukomesha ajali zinazojitokeza mara kwa mara na kuua watu wengi katika eneo hilo.

Alitoa maagizo hayo jana siku moja baada ya kutokea ajali ya lori kugongana na basi aina ya Coaster na kusababisha vifo vya watu 19 katika mlima Senjele Mbozi mkoa wa Songwe.

Akizungumza katika eneo ajali hiyo iliyotokea Februari 21 mwaka huu saa 3:15 usiku, kamanda Muslim alitaja jambo la kwanza ni polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kupata chanzo cha ajali hiyo na hatua kuchukuliwa kwa dereva na mmiliki wa gari hilo.

“Hata kama dereva wa gari hilo amefariki lakini ipo sheria inayotumika kumshitaki na pia mmiliki wa lori hilo amekwishajulikana na askari wa usalama barabarani wanamfuatilia ili naye aje ajibu tuhuma za kuruhusu gari lake kutembea barabarani likiwa bovu,” alisema.

Kamanda Muslim alisema jambo lingine ni kuweka askari wa usalama barabarani kwenye vituo viwili katika eneo hilo ambao watakuwa wakiwasiliana kisha kuyaruhusu malori kwa zamu hatua ambayo alisema imeleta mafanikio katika mlima Iwambi mkoani Mbeya ambako tangu Julai mwaka jana hakuna ajali iliyotokea baada ya kuanza kutumia mbinu hiyo.

Alisema hatua nyingine ni kuanzisha kituo cha ukaguzi wa malori makubwa yanayoingia nchini kutoka nje kwa vile husafiri mwendo mrefu sambamba na madereva kuelimishwa umuhimu wa kuendesha kwa kujihami muda wote.

Wakati huohuo, mganga mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk Kheri Kagya alisema miili 17 ya watu waliofariki katika ajali hiyo hadi jana asubuhi ilikuwa imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao na kwamba miwili bado inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa wa Songwe (Vwawa).


Credit: Mwananchi
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )