Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 12, 2019

JKT Tanzania Yamalizia Hasira Zake Kwa Timu Ya Daraja La Pili,yaipiga 4-0 Asubuhii

juu
Na Roda Kimati.
Baada ya kupigwa bao 1-0 na Yanga Sc katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara inayoendelea kwa sasa , JKT  Tanzania ya Tanga asubuhi ya  leo jumanne Februari 12 imemshushia kichapo cha mbwa Koko Usalama Sports Club ya daraja la pili mkoa wa Manyara  kwa  Mabao 4 bila majibu.

Mchezo huo wa kirafiki umepigwa majira ya saa tatu za asubuhi katika dimba la shule ya sekondari Singe mjini Babati na kuchezeshwa na marefa kutoka Babati, mchezo ambao haukuwa na amsha amsha wala shamra shamra yeyote kwani haukuwa na  watazamaji kutokana na muda ulipangwa mchezo huo wengi wao wapo katika majukumu yao.

Msemaji wa Usalama Sc Elia Kimani amesema mchezo huo haukuwa na faida yeyote kwao lakini wachezaji walijitahidi kucheza kadri wawezavyo.

“JKT  Tanzania walikuwa wanatupima tu nguvu,kwa hiyo mchezo huo wala haukuwa na faida yeyote kwetu sisi Usalama ila tumejifunza kitu na makosa yaliyopo mwalimu atayafanyia kazi,vijana wamejitahidi wameonyesha kiwango kizuri”.

Afisa habari huyo amewaomba mashabiki wa Usalama Sc kujitokeza kuishangilia timu yao na kuishauri na sio kulalamika baada ya kusikia matokeo mabaya kupitia vyombo vya  habari.

Akizungumzia mchezo huo kuchezwa asubuhi,Kimani amesema  ni kulingana na  Ratiba ya Maafande hao , kwani wanahitajika kufika mapema mjini Singida kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC) dhidi ya Singida United wiki hii katika uwanja wa Namfua Singida.

MWISHO.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )