Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 3, 2019

Kamati ya Bunge ya Bajeti yatoa angalizo Serikali kuchukua mikopo ya biashara

juu
Kamati ya Bunge ya Bajeti imesema nchi inabeba mzigo mkubwa wa kugharamia mikopo kupitia mapato ya ndani na kuathiri utekelezaji wa bajeti kwa miradi ya maendeleo.

Imesema hali hiyo inatokana na Serikali kujikita katika kukopa mikopo ya biashara ambayo ina riba kubwa kuliko mikopo yenye masharti nafuu ambayo kwa sasa ni migumu kupatikana.

Akizungumza bungeni jana wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika kipindi cha nusu ya mwaka 2018/19, mwenyekiti wake, George Simbachawene alisema, “Kwa sasa Serikali imelazimika kujielekeza kukopa mikopo yenye masharti ya kibisahara (non concessional loans) kuliko yenye masharti nafuu (concessional) kama ilivyokuwa awali.

“Kamati inaona mikopo hiyo ina riba kubwa na hivyo kuwepo kwa mzigo mkubwa wa ugharamiaji wa mikopo kupitia mapato ya ndani.”

Simbachawene alisema hadi Novemba mwaka jana, Deni la Taifa lilikuwa Sh61.8 trilioni ambazo zimetokana na ukuaji wa deni hilo kwa taratibu kutokana na uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Alisema deni la Serikali linaendelea kukua likijumlisha fedha zilizokopwa kutoka vyanzo vya ndani na nje na sekta binafsi kwa ajili ya kugharamia miradi.

“Kamati inatambua kuwa Serikali hukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kupata fedha za kigeni na kukopesha taasisi za ndani za umma kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati,” alisema.

Mbunge huyo wa Kibakwe alisema kutokana na sababu nzuri za ukopaji ikiwamo uhimilivu wa deni, bado kamati yao inashauri Serikali iangalie uwiano uliopo kati ya mwenendo wa upatikanaji wa mapato ya ndani pamoja na ulipaji wa deni la Serikali na athari zake katika bajeti a uchumi.

Kamati hiyo ilishauri kuwa, umefika wakati Serikali ipange bajeti yake ya maendeleo kwa kutegemea mapato yake ya ndani na mikopo ya ndani ambayo upatikanaji wake ni wa uhakika.

Aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa ukopaji wake katika vyanzo vya ndani hauathiri upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi huku akiipongeza kwa kuendelea kufanyia kazi mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na kamati hiyo.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )