Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 9, 2019

Kamishna Mkuu UNHCR aomba msaada wa kimataifa kwa Tanzania, inayohifadhi wakimbizi 330,000

juu

Dar es Salaam, Februari 8, 2019; Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi Duniani, Filippo Grandi amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku nne nchini Tanzania kwa kuomba uwekezaji katika ulinzi wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya Kaskazini-Magharibi mwa nchi ambako wakimbizi takribani 330,000 wanahifadhiwa. 

Ameitaja Tanzania kama “moja ya nchi muhimu zitoazo uhifadhi kwa wakimbizi Afrika,” Bw. Grandi ameelezea kuridhishwa kwake na hakikisho la serikali kwamba nchi itaendelea kuwa yenye ukarimu kwa wakimbizi.
 
Katika mkutano wake na Mheshimiwa Raisi, Dkt. John Joseph Magufuli, Bw. Grandi ameipongeza Tanzania kwa utamaduni wake wa muda mrefu wa kuwakaribisha wakimbizi wanaokimbia machafuko na mateso katika nchi zao, ikiwa ni pamoja na kuwapa uraia watu 162,000 waliokimbia kutoka Burundi mwaka 1972. Amesema ukarimu wa Tanzania na Watanzania uliodumu kwa miongo mingi kwa watu wanaotafuta hifadhi unastahili kutambuliwa kimataifa.

 Ameahidi kuendelea kukusanya misaada ya kibinadamu na ya maendeleo kwa nchi mwenyeji, kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo ya makambi na kuendeleza miradi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kutafuta nishati mbadala wa kuni. Pia, walijadili wazo la kuanzisha mfumo wa kikanda utakaojikita katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi wa nchi za Burundi na Kongo.
 
Katika kikao chake na maafisa wa serikali, Bw. Grandi alisisitiza kwamba urejeshwaji wa wakimbizi wenye tija unatokea pale wakimbizi wanapoamini kuwa ni salama kurudi makwao na wakipokea misaada muhimu utakaowawezesha kujihudumia mara watakapofika katika nchi zao. Katika miaka miwili iliyopita, wakimbizi 57,865 kutoka Burundi wamesaidiwa kurudi kwa hiari kutoka Tanzania. 

Hata hivyo, baadhi ya wakimbizi wameripoti kuwa shinikizo kutoka kwa maafisa wa serikali linalojumuisha kuzuiliwa kutembea maeneo mengine na upatikanaji wa fursa za kuendesha maisha vimewafanya waamue kurudi makwao. Bw. Grandi amesema kwenye mkutano wake kwamba UNHCR iko tayari kufanya kazi pamoja na serikali katika kuwasaidia wale wote wanaoonyesha utayari wa kurudi nyumbani lakini kwa uzoefu wake, baadhi ya vikwazo vinaweza visiwe na manufaa na kwamba ni pale tu wakimbizi wanapoamini kuwa hali ni salama kwenye nchi zao ndipo watakapochagua kurudi kwa hiari yao.
 
“Katika nchi za Kongo na Burundi bado kuna hali ya sintofahamu,” Bw. Grandi amesema kwenye mkutano wake na vyombo vya habari kufuatia ziara yake katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, huku akisema hata hivyo baadhi ya wakimbizi wako tayari kurudi na wanasaidiwa na UNHCR. “Ni muhimu urejeshwaji ubaki kuwa jambo la hiari na kwamba hakuna anayeshinikizwa kurudi.” Bw. Grandi ameomba msaada wa kimataifa ili kuhakikisha kuwa wakimbizi wanaorudi kwa hiari wanaweza kuanza upya maisha katika nchi zao za asili na kujitegemea, akisema msaada unaotolewa sasa pamoja na fedha havitoshelezi mahitaji ya wale wanaorudi Burundi.
 
Bw. Grandi amerejelea Tanzania kama nchi imara katika kanda isiyo na utulivu wa kisiasa na ameipongeza nchi kwa jukumu lake kama mtunza amani wa kanda, akiuhimiza uongozi wa Tanzania kuendeleza jitihada za amani. Katika mkutano wake Dar es Salaam na Rais mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ambaye hivi karibuni alikuwa
 
Mwezeshaji mwakilishi wa Umoja wa Afrika ya Mashariki katika Mjadala wa Mazungumzo ya Mchakato wa amani wa Burundi, Bw. Grandi alielezea matumaini yake kuwa juhudi za usuluhishaji zitaendelea. Bw. Mkapa alionyesha wasiwasi kuwa mchakato huo umesimama na, ingawa kuna hatua ilipigwa katika eneo la usalama, kikwazo cha kisiasa kinabakia na majadiliano kati ya wadau ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro wa sasa na katika kuwezesha uchaguzi huru, wa haki uliopangwa kufanyika mwaka 2020.
 
Asilimia 74 ya wakimbizi na watafuta hifadhi walioko Tanzania wanatoka Burundi, na asilimia 26 nyingine wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wengi wao wanaishi kwenye kambi karibu na maeneo ya mipaka, na wengi wao wamekuwa hapo kwa miongo mingi sasa.
 
Bw. Grandi aliisifu Tanzania kwa kuuunga mkono jitihada za Muungano wa Pamoja wa Kimataifa kwa Wakimbizi ambao utawezesha kuomba msaada mkubwa kutoka jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kuzisaidia nchi wenyeji. Pia inaomba uwezeshaji wa wakimbizi katika kujitegemea kwa lengo la kukuza uchumi na kutoa fursa kwa wenyeji, alisema Bw. Grandi.

 Wakati wa ziara yake kwenye kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, mkimbizi kutoka Kongo, Selemani Boaz, ambaye ni mfanyabiashara katika soko la pamoja lililoko nje ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, alisema, “soko linatusaidia kuwasiliana na kuonana na watu tofauti tofauti, hata kutoka nje ya kambi, hasa Watanzania .... Tunapata kufahamiana na hii husaidia kutuunganisha.” Bw. Grandi pia alisikia kutoka kwa wakimbizi kuwa soko linawawezesha pia wakimbizi kupata vyakula vya aina mbalimbali, tofauti na mgao wa chakula wa Shirika la Chakula Duniani (WFP).
 
Katika mikutano yake na viongozi wa serikali ya Tanzania, Kamishna Mkuu pia alipata fursa ya kufafanua mkanganyiko wa hivi karibuni kuhusu nguo za msaada, ambapo asilimia ndogo ilitengwa na kukabidhiwa kwa mamlaka ya serikali kwa sababu zilikuwa na mtindo usiofaa. Aidha, ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa tahadhari kubwa itachukuliwa wakati mwingine ili kuepuka kujirudia.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )