Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 22, 2019

Mahakama Yasogeza Mbele Hukumu ya Mgogoro Wa Lipumba na Maalim Seif Ndani ya CUF

juu
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kutoa hukumu ya mgogoro wa uongozi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) na badala yake imeisogeza mbele hadi Machi 17, 2019.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa leo Ijumaa, Februari 22, 2019 na Jaji Benhajj Masoud aliyekuwa akiisikiliza kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini  wa chama hicho. Hukumu hiyo imeahirishwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Sharmillah Sarwatt.

Akiahirisha hukumu hiyo Naibu Msajili, Sarwatt amesema Jaji Masoud ambaye alitarajiwa kuisoma anakabiliwa na majukumu mengine.

“Hivyo nina ahirisha usomaji wa hukumu hii hadi Machi 17 mwaka huu,” amesema Naibu Msajili Sarwatt akitaja tarehe hiyo baada ya kuwasilishwa na karani wa Jaji Masoud.

Hata hivyo, tarehe hiyo itakuwa ni siku ya Jumapili siku ambayo huwa hakuna shughuli za kimahakama.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )