Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 7, 2019

Mawikili Waomba Kusogezewa Mahakama Kuu Njombe

juu
Chama cha wanasheria Tananganyika (Tanganyika low society) pamoja na vyama vingine kikiwemo chama cha mawikili Afrika mashariki mkoani Njombe wameiomba serikali kusogeza mahakama kuu mkoani humo pamoja na kuongeza idadi ya watumishi wa mahakama ili kukabiliana na idadi ya ongezeko kubwa la mashauri mahakamani.

Ombi hilo limetolewa na mawakili hao kwa mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA,wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini yaliyofanyika kimkoa katika mahakama ya wilaya ya Njombe.

“Ili kuboresha swala la utoaji wa haki kwa wakati tungependa kupendekeza ongezeko la idadi ya watumishi wa mahakama yaani majaji na mahakimu ili kukabiliana na ongezeko kubwa la idadi ya mashauri mahakamani ambapo waliopo wamekuwa wakilemewa na mzigo mkubwa wa kazi hivyo kufanya haki isitolewa kwa wakati”alisema Tunsumwe katika hotuba ya chama cha mawikili Afrika masahariki

“Lakini pia kusogeza jirani huduma za mahakama, Mfano; katika Mkoa wa  Njombe kuwepo kwa mahakama kuu kutasidia sana  wananchi kupata haki ya kukata rufaa, kwani ni vigumu sana mtu anaye ishi MANDA kukata rufaa mahakama kuu Iringa”aliongeza Tunsumwe

Aidha ameongeza kuwa kilio kikubwa cha wananchi na wadau wa mahakama wengine kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwa mahama ni ucheleweshaji wa utoaji haki, na moja ya sababu za ucheleweshaji ni kukosekana au uhaba wa vitendea kazi, miundombinu mibovu na umbali wa huduma ya mahakama. Na kuruhusu watu wasio na taaluma ya sheria kuaanda nyaraka za kisheria ambazo zimekuwa hazina ubora na kufanya kuwepo na mapingamizi yakisheria yanayofanya ucheleweshaji wa mashauri.

Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya hakimu mkazi Njombe MAGDALENA NANSON MTANDU amesema kuwa,pamoja na mafanikio makubwa yanayotokana na chombo hicho cha mahakama huku kukiwa na changamoto mbali mbali lakini bado wameendelea kuboresha huduma za kimahakama ili kuweza kutoa haki kwa wakati

Mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkoani Njombe ameahidi kufikisha maombi hayo kwa Rais ili kuona namna ya kuyatekeleza maombi hayo.

“Ili tuone namna  ambavyo tunaweza kuharakisha na kupunguza mzigo huu na kutoa haki kwa wakati kwa wadau wetu mimi nitaifikisha huko,na siwezi kusema mimi nitawaongezea  lakini serikali yenu imesikia ningetamka neon leo lakini huku anatamka mmoja tu”alisema Olesendeka

Wakati maadhimisho yakiadhimishwa kimkoa mkoani Njombe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli jana amefunga maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )