Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 20, 2019

Rais Magufuli ateua Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani. https://t.co/HTTBSEEB4H

juu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Michael Wilfred Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania – OUT)

Dkt. Ng’umbi amechukua nafasi ya Dkt. Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Jaji Stephen Mrimi Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT)

Jaji Magoiga amechukua nafasi ya Jaji Barke Mbaraka Sehel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 19 Februari, 2019.
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )