Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 3, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 65

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      
 
“Umewaua hawa?”
“Hapana hakuna niliye muua. Ila kuna sumu fulani ya kisindano Dany alinifundisha nimeweza kuwashoma mmoja baada y mwengine na nimeweza kuwaleta hapa”
“Ehee huyu ndio kijana ambaye ameniletea simu yake nizungumza na bosi wake.”
“Simu yake hii hapa ninayo na nimeweza kuangalia muda ule ni nani aliweza kumpigia nimeweza kupata ni nani uliye zungumza naye”
“Ni nani?”
Camila akanionyesha picha ya mwanaume mmoja ambaye kwa haraka sana niliweza kumfahamu kwani ni miongoni mwa watu nilio kutana nao kikao cha siri nilicho fanya na viongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania.

ENDELEA
“Vipi mbona unashangaa mume wangu?”
“Huyu , huyu mtu nina mfahamu”
“Huyu mzee una mfahamu?”
“Ndio”
“Anapatikana wapi?”
“Tumemuacha nchini Tanzania, katika ule mpango wangu wa kulipiza kisasi kwa mzee Poul Mkumbo huyu mzee, nimeamua kudhamini moja ya chama cha siasa ili kiweze kumuondoa madarakani. Sasa huyu mzee ni muhisika”
“Ohoo basi kutakuwa na jambo linalo endelea hapo katikati?”
“Yaa”
“Basi kama ni hivyo, muhusika mkuu yupo Tanzania, itabidi hawa tuwaweke chini ya ulinzi wa serikali?”
 
“Alafu?”
“Tunamfwatilia huyo mwengine?”
“Huoni kwamba hiyo inaweza kuvujisha siri na kumbuka kule Tanzania tumewekeza kwenye kampuni kubwa na kama adui nimeweza kumuweka karibu yangu jambo ambalo ni hatari sana”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Camila usoni mwake.
“Basi tuwaue?”   
“Hilo nalo ni kosa jengine ambalo tutalifanya mume wangu na kumguka kwamba hapa ni Ujerumani na upelelezi ukianza kufanyika haijalishi mimi ni mtoto wa nani, mwishowe nitaishia jela na nitamchafua baba yangu”
 
“Nimekuelewa mke wangu”
“Nampigia baba na ninamueleza juu ya swala hili na akikubaliana tuwashikilie chini ya ulinzi wake basi tunaweza kufanya hivyo”
“Sawa”
Camila akafanya kazi hiyo kama nilivyo mueleza. Baada ya lisaa kikiso maalumu cha makachero ambacgo kina fanya kazi chini ya raisi kikafika nyumbani hapa. Wakawabeba wahalifu hawa kimya kimya pasipo watu wengine walipo kwenye msiba huu kuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea. 
 
Siku iliyo fwata taratibu zamazishi zikakamilika , na maiti ya bi Jane ikapelekwa katika kanisa la Lutheran kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho, wingi wa watu na umaarufu  wa familia hii ukafurika hapa kanisani, watu wengi wakazidi kutoa pole zao kwa mimi na dada Mery. Tulipo maliza ibada tukaelekea katika eneo alilo zikwa mzee Klopp miaka kadhaa ya nyuma iliyo pita. Tukauaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kisha akazikwa. 

Kusema kweli kama ni kubaki yatima basi sasa ni yatima mkubwa, hata ukiwa na pesa nyingi sana duniani, ila umuhimu wa wazazi ni mkubwa na ni wa muhimu kuiko hata pesa. Mazishi yalipo malizika tukarudi nyumbani huku muda wote Camila akiwa pembeni yetu mimi na Mery kwani yeye ndio mtu wa pekee anaye weza kutufariji.
 
Baada ya wiki mbili tukaendelea na shuhuli zetu za kawaida. Nikanza kufanya ziara za kustukiza katika kampuni zangu zote za hapa nchini Ujerumani. Nilipo hakikisha kwamba ziara yangu ya siku tano imekwenda kama nilivyo hitaji, nikanunua ndege yangu binafsi aina ya The Boeing 747-8 VIP private jet ambayo imenigarimu kiasi cha dola za kimarekani milioni mia tatu na sabini. Jet yangu hii ina sifa zote nilizo kuwa nina zihitaji, kwanza ina uwezo wa kusafiri kwa umbali mkubwa sana, pili ina seble kubwa, chumba cha kulala chenye bafu na choo. Pia ina ofisi kubwa ambayo ninaweza kufanya vikao na wafanyakazi wangu baadhi.
 
“Ohoo Mungu wangu”
Camila alizungumza kwa furaha mara baada ya kumfungua kitambaa nilicho kuwa nimemfunga usoni mwake, mara tu ya kuingia kwenye ndege hii kubwa. Kwani katika mipango yangu ya ununuzi ndege hii sikuweza kumshirikisha mtu wa aina yoyote na Ethan pekee ndio aliye fahamu na uzuri yeye si binadamu.
 
“Ethan unataka kuniambia kuanzi hivi sasa hii ni ndege yetu?”
“Yaa ni ndege yetu, popote ambapo tutahitaji kwenda basi tunaweza kwenda”
“Ohoo Mungu wangu nakupenda sana mume wangu”
“Ninakupenda pia mke wangu”
Nikaanza kumtembeza Camila ndani ya ndege hii, kila sehemu aliyo ingia hakuamini macho yake, kwani imetengenezwa katika mtindo mzuri sana ambao umeendana na kiasi cha pesa ambacho nimenunulia.
“Camila fumba macho yako”
“Kwa nini?”
“Wewe funga tu mpenzi wangu”
Camila akanitii na kufumba macho yake. Taratibu nikatoa kisanduku kidogo cha kuhifadhia pete, nikapiga goti moja chini kisha nikamuomba aweze kufumbua macho yake.
 
“Je upo tayari kuwa mke wangu?”
Camila akapatwa na mshangao mkubwa ulio ambatana na furaha kubwa pamoja na machozi mengi sana.
“N…dioo Ethan”
Taratibu nikamvisha pete hii iliyo nigarimu kiasi kikubwa cha pesa. Camila akaninyanyua na kunikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia. Taratibu tukaanza kunyonyana midomo yetu na kutokana tupo ndani ya chumba chetu cha kulala hatukuona haja ya kunyimana haki inayo stahili katika penzi letu
 
Usiku wa siku ya leo tukalala katika ndege yetu siku iliyo fwata tukaelekea ikulu ya Ujerumani ambapo sasa ndipo familia ya Camila inapo ishi. Tukawaleza wazazi wake juu  ya swala zima la mimi kuhitaji kumuao mtoto wao pale nitakapo maliza kufanya kazi yangu ambacho itanirudisha nchini Tanzania.
Wazazi wa Camila hawakuana kipingamizi chochote na mimi, kila mmoja akaonekana kujawa na furaha kubwa sana kwa pendekezo langu kwa mtoto wao.
 
Tukamueleza Mery juu ya mpango wetu wa sisi kufunga ndoa. Mery kwa upande wake hakuwa na pingamizi la aina yoyote kwani naye mapenzi yake na rafiki yangu Ethan yamekoaa na wanapenda sana. Nikaka Ujerumani kwa siku mbili kisha nikaanza safari ya kurudi nchini Tanzania na safari hii nikiwa peke yangu katika ndege yangu hii ya kifahari. Nikiwa angani nikawasiliana kwa njia ya skype na Qeen pamoja na Latifa na nikawaomba waweze kuniandalia hoteli ambayo nitafikizia kwa siri sana.
 
“Tunafurahi sana mkuu kwa kurudi kwako kwa maana katika kipindi hichi cha wiki tatu tumekuwa tunapelekeswaha sana na huyu mwanamke wako”
“Musijali, kila jambo litakwenda sawa na hii ndio safari yake ya mwisho ya yeye kuweza kuumia”
“Sawa mkuu, tunafurahi kuendelea kusikia hivyo”
“Lile swala la yule mzee katika kikundi cha kile chama mume lishuhulikia?”
 
“Ndio mkuu tunakusubiria wewe ufike ili kama ni kumteka aweze kutekwa na kuweka chini ya uangalizu maalumu si unajua tayari watu wamesha anza kampeni?”
“Ndio natambu hilo. Clara je munakwenda kumtembelea?”
“Ndio hata leo tumetoka huko na ameweza kutuulizia”
“Sawa, nahitaji muje kunichukua uwanja wandege”
“Saa ngapi?”
“Sijajua marubani wangu wanaweza kutumia muda gani kufika nchini Tanzania, ila nina ndege ambayo ipo vizuri sana”
“Kuna taratibu za kutua nchini Tanzania kwa ndege binafsi je umezikamilisha?”
“Ndio nimezikamilisha, na nimepewa ruhusa ya kutua nchi karibia ya ishirni barani Afrika”
“Sawa mkuu tukutakie safari njema”
“Nanyi pia”
 
Tumaliza mazungumzo haya, nikaingia kwenye upande wa barua pepe katika simu yangu na nikaanza kupitia ofa kadhaa za timu kubwa barani Ulaya ambazo zinahitaji niweze kucheza mpira. 

Sikuhitaji kujibu  ujumbe hata mmoja kwa maana nina hitaji kuikamilisha ndoto yangu ya kumfilisi bwana Poul Mkumbo na nina imani kwamba hapo akili yangu inaweza kuwa tayari katka kucheza mpira na kuendelea kuishia katika kipaji changu ambacho siku zote mzee Klopp alinihusia niweze kukifanyia kazi. 

Nikawauliza marubani wangu ni muda gani ambao ninaweza kufika nchini Tanzania, walipo nipa muda husika, niwatumia meseji Qeen na Latifa na kuwajulisha kwamba nitaingia nchini Tanzania majira ya saa kumi usiku. 
 
‘Tutakuwepo hapo mkuu’
Niliipokea meseji hii kutoka kwa Latifa. Majira ya saa kumi usiku kwa mara ya kwanza ndege yangu toka nianze kuitumia ikatua katika ardhi ya nchini Tanzania. Nikashauriana na wa marubabi wangu waweze kurudi Ujerumani na ndege yangu baada ya siku mbili kwani sinto weza kuiacha ikae katika uwanja wa ndege wa hapa Tanzania, moja inaweza kutumia na maadui wangu kama moja ya sehemu ya kujipatia kipato kwani endapo  wataamua kuiteka na kudai pesa nyingi basi itanilazimu kutoa kiasi kikubwa cha pesa. 
 
Kwajinsi nilivyo vaa kofia pamoja na jinzi na tisheti ni ngumu sana kwa watu wa kawaida kuweza kunifahamu. Baada ya kukaguliwa begi langu la nguo nikatoka nje ya uwanja huu na kukutana na Latifa pamoja na Qeen. Tukaingai kwenye gari walilo kuja nalo ambapo siku kadhaa za nyuma niliwatumia pesa za kutosha kwa ajili ya kununua gari maalumu kwa kazi ambazo zimetuleta huku.
“Kuna update yoyote kwa masaa haya kadhaa ambayo hatujawasiliana nanyi?”
“Hapana mkuu”
 
“Huyo kijana muliye sema kwamba atakuwa ni mlinzi wangu wa siri je anajiweza katika kila idara ya kunilinda au mumemchukua mbeba vyuma ambaye akipigwa ngumi moja tu anaanguka?”
“Hahaaa hapana ni kijana mmoja smart na hata ukimona huto weza kutegema kama anaweza kuwa ni mpambanaji mzuri sana”
“Nahitaji kuonana naye usiku huu huu”
“Sawa”
Latifa akampigia simu kijana huyo na kumueleza aweze kufika katika hoteli ambayo tunaiendea hivi sasa. Tukafika katika hoteli moja iliyo nje ya jiji la Dar es Salaam. Moja kwa moja tukaeleka hadi katika chumba walicho nikodishia, baada ya muda kidogo kijaan huyo akafika. Ni mwembaba, ana sura nzuri na ya upolea sana na kwa haraka kwa kweli huwezi kufahamu kama ana uwezo wa kuweza kufanya mambo makubwa sana.
 
“Ethan huyu anaitwa Raman kwa kifupi tunamuita Roma. Roma huyu ndio bosi wetu ambaye yeye ndio anatufanya tuweze kuishi hapa mjini naa kupendeza”
“Nashukuru sana bosi kwa kukufahamu”
Sauti ya Roma ni ya upole sana.
 
“Nashukuru pia. Unaweza kunipa sifa ya kazi yako?”
“Ndio. Niliishi South Korea kwa miaka zaidi ya kumi na mbili. NIliweza kuiingia katika vikosi vyao ya kijasusi na nimefanya kazi katika vikosi hivyo kwa miaka zaidi ya saba. Nimerudi nchini Tanzania baada ya mikataba yangu kuisha katka vikosi hivyo”
Roma alizungumza huku akinionyesha picha zake za zamania kiwa katika vikosi hiyo kwa kupitia simu yake ya mkononi mwake. 
 
“Wewe ni Mtanzania?”
“Ndio ni Mtanzania, mama yangu ni mkorea, ila baba yangu ni mtanzania”
“Sawa ndio maana unaonekana kuwa mpole mpole”
“Ndio mkuu”
“Nina imani kwamba unajua jinsi ya kulinda siri za mkuu wako na nina amani kwamba unajua jinsi ya kufanya mission zote nzito na kali?”
 
“Ndio”
“Nashukuru. Tusipoteze muda sana, tuna kazi moja nina imani kwamba mabinti hapa wamekupa maelezo ya juu ya mzee huyo?”
“Ndio nimesha andaa mazingira ninasubiria amri yako”
“Nimekuruhusu, inaweza kufanyika leo hiyo kazi?”
“Kwaleo hapana mkuu ila kabla ya siku ya kesho kuisha nitakuwa nimeikamilisha hiyo kazi”
“Basi fanya hivyo”
“Nashukuru mkuu”
“Basi nikutakie usiku mwema”
“Asante”
 
Roma akatoka ndani hapa na kuniacha na Qeen na Latifa.
“Ehee kampenzi zao zinakwenda vipi?”
“Huwezi kuamini mkuu, yaani ni mafuriko”
“Mafuriko ndio nini?”
“Yaani watu wanajaa, kampenzi ni za nguvu na sasa zinaingia hadi vijijini huko ndani ndani yaani ni raha sana.”
“Tuna video hapa tunaweza kukuonyesha jinsi pesa yako inavyo leta nguvu kwa wananchi. Pia shemeji yangu yaani ananiambia kwa miaka yake yote aliyo fanya siasa hajawahi kuona jinsi mikutano na chama chao kinavyo pendwa kama msimu huu”
“Kwahiyo inatia matumaini?”
“Asilimia mia moja matumaini yanaonekana katika kampenzi hizi”
 
“Watala nao vipi?”
“Yaani wao wana henya henya. Mkuu wao hana sera yaani huyo mke anavyo tukazania tuweze kumuunga mkono baba yek na hapa kesho huwezi amini ametuambia watu wote tuelekee jangwani kwenda kusikiliza kampeni za baba yake hapa Dar es Salaam”
“Yaani wafanyakazi wote, kesho wanao weza kubaki ofisini ni mainjinia tu”
“Munakwenda saa ngapi?”
“Kuanzia saa kumi ndio tunakwenda hivyo kuanzia saa nane mchana hivi magari yote ya kampuni yatatumika katika kuwapeleka wafanyakazi katika kampeni”
 
Nikatoa simu yangu na kuweka laini ninayo itumia nchini Tanzania kwa siri, nikampigia mkuu wa ulinzi wa katika kampuni yangu hii ya simu na kumpa onyo la kuto kuruhusu gari yoyote ya kampuni kutoka nje ya viwanja vya kampuni yangu ikiwa na wafanyakazi. Onyo langu likaeleweka, majira ya saa kumi na mbili alfariji Qeen na Latifa wakaondoka hotelini hapa na nikawahisi kwamba nitafika ofisini muda wowote. 

Nikajipumzisha hotelini hapa hadi majira ya saa sita mchana, nikajiandaa na kuanza safari ya kueleka ofisini kwangu tena kwa kutumia usafiri wa bajaji. Majira ya saa nen kasoro hikafika katika geti kuu na kuwakuta walinzi wa kampuni niliyo wapa dhamana ya kulinda ofisi yangu wakiwa wametanda katika geti hilo huku Biyanka akionekana kufoka sana na kuwaamrisha walinzi hao waweze kuondoka la sivyo atawafukuza kazi. 

Kutokana hakutarajia kuweza kuniona kwa wakati huu, taratibu nikashuka kwenye bajaji hii huku nikiishusha kofia yangu chini kidogo na kufika nusu uso. Watu wa pekee walio weza kunigundua na Qeen na Latifa ambao wapo mbele ya moja ya gari aina ya Costa wakisubiria kuelekea kwenye kampeni za mzee mkumbo. 

==>>ITAENDELEA KESHO
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )