Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 15, 2019

Rugemarila , Seth waendelea kusota Rumande

juu
Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha inayowakabili wafanyabiashara Herbinder Seth na mwenzake James Rugemarila, bado unaendelea na washtakiwa wanaendelea kusota rumande.

Washtakiwa hao kwa pamoja walisomewa mashtaka 12 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Swai alidai mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka hayo 12 ya uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Washitakiwa hao bado wanasota rumande kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )