Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 8, 2019

Serikali Yapiga Marufuku Kusafirisha Wanyama Hai Nje ya Nchi

juu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kuanzia sasa Serikali ya Tanzania haitaruhusu usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi.

Kauli hiyo imefuta agizo la Wizara hiyo ambayo iliweka zuio la miaka mitatu na Mei, 2019  ilikuwa ndiyo mwisho wa zuio hilo.

Kigwangalla ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Februari 8, 2019 wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Muheza (CCM),  Balozi Adadi Rajabu.

Mbunge huyo alitaka kujua Mei, 2019 Watanzania wataanza kusafirisha wanyama hai ikiwemo akina mama wa kijiji cha Fanusi wilaya ya Muheza ambao husafirisha vipepeo.

"Niseme wazi kuanzia sasa hatutaruhusu wanyama hai kusafirishwa kwenda nje ya nchi na  wale waliokuwa wanafanya biashara hiyo watafute njia nyingine," amesema Kigwangalla.

Katika swali la msingi Rajabu aliuliza ni lini wananchi wa kijiji cha Fanusi wataruhusiwa kusafirisha vipepeo nje ya nchi kwa kuwa si wanyama.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )