Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maadhimisho Ya Siku Ya Kimataifa Ya Kupinga Ukeketaji Duniani

juu
Maadhimisho ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto uadhimishwa kila ifikapo tarehe 6 Februari kila mwaka. Historia ya siku hii ilianza mwaka 2003 Jijini Adis Ababa Ethiopia kwenye mkutano wa kimataifa ambao ulitoa tamko la kutenga siku maalum ya kikomo cha uvumilivu kwa ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike.

Baraza la Umoja wa Mataifa lilifikia uamuzi huu baada ya kutathimini na kuona athari kubwa zitokanazo na vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike. Madhumuni ya maadhimisho haya ni kupinga ukeketaji ambao ni kitendo cha kikatili na kinyume na sheria lakini pia kinyume na  haki za binadamu.Tanzania kama nchi mwanachama wa umoja huo inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hii ya kupinga ukeketaji.

Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali, Mashirika na Taasisi mbalimbali bado ukeketaji umeendelea kutekelezwa katika baadhi ya jamii hapa nchini.

Kwa mujibu wa Takwimu za Taarifa ya Demographia na Afya ya 2015/16 zinaonyesha kuwa pamoja na jitihada za kutokomeza vitendo hivyo, bado kuna mikoa mitano inayoongoza kwa ukeketaji nchini ikiongozwa na Manyara wenye asilimia (58) ukifuatiwa na Dodoma (47), Arusha (41), Mara (32) na Singida yenye asilimia (31),Tanga( 14), kilimanajaro (10), Mororgoro (9), Iringa (8) na Njombe (7).

Ziko sababu nyingi zinazosababisha, kuendelea kwa ukeketaji moja kati ya hizo ni usiri mkubwa uliopo katika jamii husika. Jamii kwa kuamini kuwa kukeketa ni mila na desturi zao, wameendelea kuhifadhi na kutunza siri za wale wanaoendeleza vitendo hivyo, ili kuwaepusha wahusika na mkono wa dola. Hali hii hupelekea watoto wa kike na wanawake kuendelea kunyanyasika bila msaada.

Mwaka huu wa 2019 maadhimisho haya ya siku ya kupinga ukeketaji yanafanyika katika mikoa yote Tanzania kulingana na mazingira husika Kauli mbiu ya mwaka huu ni: Acha mila zenye madhara: tokomeza ukeketaji”.

Kauli mbiu hii imezingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 inayolenga kuondoa umaskini, kukuza mafanikio ya kiuchumi, maendeleo ya kijamii na ustawi wa watu.

Aidha kauli mbiu hii imejikita zaidi katika lengo namba 5 linalosisitiza suala la kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana. Katika utekelezaji wa Malengo ya maendeleo Endelevu jamii ina wajibu wa kulinda haki na utu wa mwanamke kwa kupinga ukatili  na vitendo vyovyote vinavyodhalilisha utu wa mwanamke na mtoto wa kike.

Yapo madhara mengi yanayosababishwa na ukeketaji; madhara hayo yanaweza kuwa ya kiafya au hata kisaikolojia. Madhara yanayosababishwa na ukeketaji yanaweza kuwa ya papo kwa papo kama maumivu makali wakati wa ukeketaji, mshtuko, homa kali, kumwaga damu nyingi na mara nyingine hata kupelekea kifo, kuambukizwa magonjwa kama Virusi Vya UKIMWI na msongo wa mawazo. Yapo pia madhara ya muda mrefu kama vile; kuathirika kisaikolojia, ulemavu/kovu la kudumu katika uke, fistula, kupata shida wakati wa kujifungua na muda mwingine kupelekea kupata ugumba.

Wizara naiomba jamii kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika utoaji taarifa wa matukio ya ukeketaji yanayofanywa katika maeneo yenu lakini pia familia hasa wazazi/walezi kuwa mstari wa mbele kupinga wanawake na watoto wa kike kufanyiwa vitendo vya ukeketaji.

Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kushugulikia tatizo la ukatili  kwa wanawake na watoto kwa kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto 2017/18-2021/22, uliozinduliwa mwaka 2016 na kupitia mpango kazi huu serikali imedhamiria kupunguza vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji kutoka asilimia 15 ya mwaka 2010  kufikia asilimia 7 ifikapo 2022.

Serikali imeanzisha jumla ya kamati za ulinzi wa mama na mtoto 10,988 katika ngazi mbalimbali kwa lengo la kulinda wanawake na watoto dhidi ya ukatili nchini.Aidha serikali imeanzisha madawati ya jinsia  na watoto katika vituo vya polisi kutoka 417 mwaka 2015 hadi 600 mwaka 2017.

Serikali imeendelea kuboresha sheria na sera mbalimbali ili kupanua wigo wa adhabu kwa wale wanaoendelea kutekeleza kitendo hicho cha kikatili. Kwa mfano mabadiliko ya Sheria ya Mtoto (2009) yamelenga pamoja na mambo mengine kupanua adhabu na kutengeneza mnyororo mpana wa washiriki. Maboresho ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu (2002) nayo yamepanua uwanda wa kutoa adhabu na kubaini kipimo cha ushiriki wa mtuhumiwa katika kufanya ukeketaji.

Sera mbalimbali za kitaifa ikiwemo Sera ya Elimu ya 2015 inapinga kila aina ya unyanyasaji kwa mtoto wa kike na inaweka na kutambua misingi ya haki na usawa kwa watoto wote wa kike na wa kiume. Sera hii pia imelenga kuondoa ubaguzi na unyanyasaji kwa mtoto wa kike.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )