Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 10, 2019

Tamasha la Pasaka Dar ndani ya Viwanja vya Kijitonyama

juu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama amesema tamasha hilo mwaka huu litafanyika Aprili 21 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Msama amesema viwanja vya posta ni mahali ambapo pako katikati zaidi na panaweza  kufikiwa na watu wa pande zote za jiji la Dar es salaam na ni eneo ambalo linafikika kirahisi .

Msama ameongeza kuwa mara baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es salaam litafanyika pia katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Simiyu na Iringa na wataongeza mikoa mingine kadiri ya mahitaji yatakavyokuwa ili kuhakikisha watu wote wanaopenda kupata burudani ya muziki wa injili kupitia Tamasha la Pasaka wanafikiwa.

Tamasha la Pasaka linatarajiwa kushirikisha  wanamuziki mbalimbali wa nchini Tanzania na nje ya Tanzania.

Msama amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri ambapo mpaka sasa tayari wamekamilisha mazungumzo na mwimbaji mmoja kutoka nje hata hivyo hakumtaja jina lake.

Awali Msama alisema wako katika mazungumza na wanamuziki kutoka Marekani, Uingereza , Afrika Kusini, Nigeria , Kenya na Tanzania pia.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )