Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 11, 2019

Upelelezi Kesi Ya Amber Rutty Na Mumewe Wakamilika.....Kusomewa maelezo ya awali Machi 7

juu
Upelelezi katika kesi ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary maarufu Kama Amber Rutty na mume wake Said Mtopali umekamilika na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma Machi 7 kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Februari 11, 2019  na Hakimu Mkazi , Augustine Rwezile baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Wakili wa Serikali, amedai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea Maelezo ya awali.

"Kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo, umekamilika hivyo tunaomba terehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea Maelezo ya awali," amedai Nguka.

Nguka baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 7, 2019.

Mbali na Amber Rutty, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Said Mtopali na James Charles maarufu kama 'James Delicious'.

Washtakiwa hao walifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza Novemba 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth na anadaiwa amelitenda kati ama baada ya Octoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Charles au James Delicious akidaiwa kati ya Oktoba 25, 2018 alisambaza video za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamelikana.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )