Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Upelelezi Kesi Ya Wema Sepetu Wakamilika

juu
Upelelezi wa kesi ya kuchapisha video ya ngono kupitia ukurasa wa Instagram inayomkabili Msanii wa Filamu, Wema Sepetu, umekamilika na itaanza kusikilizwa Februari 21, mwaka huu baada ya kusomewa maelezo ya awali.
 
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Glory Mwendi mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde.

Wakili Glory ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi February 21, 2019

Katika kesi hiyo namba 322 ya mwaka 2018, Wema anadaiwa Oktoba 15 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar alichapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akijua ni kinyume na sheria.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )