Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 7, 2019

Uturuki kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watanzania

juu
Na Genofeva Matemu – JKCI
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Uturuki wameonesha nia ya kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watanzania.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia huduma za matibabu zinazotolewa na taasisi hiyo pamoja na miundombinu iliyopo Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka hospitali ya Medicana iliyopo Bursa nchini Uturuki Prof. Serdar Enir alisema wataalamu kutoka Uturuki wana nia ya kufanya kazi na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ili waweze kuwasaidia wananchi wenye matatizo ya moyo.

“Nimekuja hapa kuangalia huduma mnazozitoa, wataalamu mlionao, miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na aina za mashine zilizopo,  nimeridhika navyo. Hivyo basi tunaenda kujipanga tuone ni namna gani tutashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo”.

“Nchini Uturuki tuna madaktari wa upasuaji wa moyo zaidi ya elfu mbili wakati hapa nchini Tanzania wako wachache, hivyo basi tukija na kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa siku chache tutaweza kuokoa maisha ya watanzania wengi”, alisema Prof. Serdar.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kumekuwa na  mazungumzo ya muda mrefu tangu mwaka 2014 na nchi ya Uturuki ili iweze kuwaleta wataalamu wake wa magonjwa ya moyo hapa nchini.

“Hivi sasa nchi ya Uturuki imeonyesha nia ya kutuma wataalamu wake hapa nchini, na wataalamu wetu watakwende nchini kwao kujifunza, hii itasaidia kuokoa maisha ya watanzania na kubadilishana ujuzi wa kazi”.

“Idadi ya wagonjwa wa moyo wanaosubiri kufanyiwa upasuaji inazidi kuongezeka siku hadi siku, hivyo basi kama tutashirikiana na wenzetu itatusaidia kutoa huduma kwa wakati na hivyo kupunguza msongamano”, alisema Prof. Janabi

Madaktari kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya Asia, Ulaya, Australia, Mashariki ya kati na Mrekani wamekuwa wakifanya kambi maalum za matibabu ya moyo katika Taasisi hiyo  na kuokoa maisha ya watanzania pamoja na  kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wataalamu wa afya.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )