Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 16, 2019

Wadau wa madini kuandamana kumpongeza Rais Magufuli

juu
Wadau wa madini na wachimbaji wa mkoa wa Manyara, wanatarajia 
kuandamana Jumamosi ijayo, kwa lengo la kumshukuru Rais John Magufuli 
kwa kukubali kutia saini muswaada wa dharura wa marekebisho ya sheria za
fedha, kupunguza na kufuta kodi zilizolalamikiwa.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara
(Marema), Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi, alisema jana kuwa
 maandalizi ya maandamano hayo yatakayopokelewa na Mkuu wa Mkoa huo,
Alexander Mnyeti, yanaendelea vizuri.

Alisema maandamano yatafanyika umbali wa kilomita tatu na yataanzia 
kwenye lango la Magufuli la kuingia ndani ya ukuta saa 2:00 asubuhi
na kumalizika Saa 4:00 asubuhi.

Baada ya hapo, alisema itasomwa risala ya kumpongeza
Rais Magufuli kudhibiti utoroshwaji madini, ulipaji kodi na kumuunga
mkono.



“Waandamanaji watazunguka migodi ya madini ya Tanzanite hadi kwenye
uwanja wa barafu wa CCM Mji Mdogo wa Mirerani ndipo 
watakapoishia,”alisema.



Mushi alisema maandamano hayo yatawahusisha wachimbaji wote wa madini
 wa mkoa huo kutoka wilaya zote za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang'
na Mbulu.

Alisema lengo kubwa ni kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwakubalia
 ombi lao, hadi wabunge wakapitisha sheria hiyo baada ya mkutano wa
kisekta wa wadau wa madini uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.

 

Alisema kaulimbiu ya maandamano hayo ni “Rais Wetu, Madini Yetu,
Uchumi Wetu” na wadau mbalimbali wa madini wakiwamo wachimbaji,
wamiliki wa migodi na wazamiaji (na Apolo) watashiriki.

"Pia wadau wengine wanaonufaika na madini wakiwamo wafanyabiashara,
madalali na wanunuzi wa madini, watashiriki maandamano hayo
ya kumpongeza Rais Magufuli wetu," alisema Mushi.

Alisema wanaandamana kumpongeza Rais Magufuli, baada ya kupita siku 17
tangu mkutano wake na wadau wa madini kufanyika na kisha kupitishwa
kuwa sheria na bunge.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga
 alisema maandamano kama hayo yanaruhusiwa kufanyika mradi
 wahusika wawe na kibali kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya husika.

Kamanda Senga alisema hivi karibuni yalifanyika maandamano kama hayo
 ya wafugaji na wakulima kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwatetea, hivyo 
hata hayo ya wadau wa madini watayaruhusu wakiomba kibali.

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )