Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 3, 2019

Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

juu
Dar es salaam 
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA)  imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa atagundulika kuwa ana uvimbe, sampuli itachukuliwa kwa njia ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hivyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa uchunguzi wa awali ambao unafanyika leo na kesho na huduma hiyo inatolewa bure.

Akielezea kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti Dkt. Sakafu amesema saratani ya matiti ni namba mbili kati ya saratani zinazowapata wanawake hapa nchini, pia katika vifo vyote vitokanavyo na saratani kwa wanawake Saratani ya matiti ni ya pili.

“Wengi wanafika hospitalini kwa kuchelewa na ugonjwa unakua umefika hatua ya mwisho na hivyo kusababisha matatibabu yake kuwa na changamoto’’. Amesema Dkt. Sakafu.

Kwa upande wake Daktari kutoka MEWATA, Dkt.  Deograsia Mkapa ametaja visababishi vya ugonjwa wa saratani ya matiti kuwa ni kutonyonyesha, kutofanya mazoezi mara kwa mara na uvutaji wa sigara.

Dkt. Mkapa amewashauri wanawake endapo wakiona mabadiliko yoyote kwenye mwili hasa kwenye matiti kuwahi hospitalini kwa ajili ya uchunguzi.

Katika zoezi hilo zaidi ya watu 70 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )