Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 7, 2019

Watu Wanne Watiwa Mbaroni Jijini Mbeya Kwa Kuingiza Bidhaa Nchini Kinyemela Bila Kulipia Ushuru

juu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne pamoja na gari moja aina ya Toyota Coaster kwa kosa la kuingiza bidhaa nchini kinyume cha sheria.

Ni kwamba mnamo tarehe 06.02.2019 majira ya saa 22:00 usiku huko katika kizuizi cha barabarani kilichopo eneo la Kayuki, Kata ya Mpuguso, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa Doria waliwakamata watu wanne [04] ambao ni:-
  1. MARY ANDEMBWISYE [30] Mfanyabiashara na Mkazi wa Ghana Mbeya
  2. TUMPE ANDEMBWISYE [32] Mfanyabiashara na Mkazi wa Ghana Mbeya 
  3. . ISSA KIBONA [47] Dereva na Mkazi wa Kyela na
  4.  YOHANA ADAM [25] Kondakta na Mkazi wa Rungwe Mission
Watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanaingiza bidhaa nchini bila kulipia ushuru ambazo ni bello 26 za mitumba kutoka nchi jirani ya Malawi. Mzigo huo ulikuwa umepakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T.350 DDR aina ya Toyota Coaster.

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )